DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Saturday, 25 March 2017

DAWA YA JINO KAMA UNASUMBULIWA NA MENO

Acha Kuteseka na Maumivu ya Jino Tumia Mbinu Hii..!!!

 Afya


Maumivu ya meno huwa makali sana na huweza kukusababisha hata kushindwa kufanya kazi nyingine endapo yatakuwa ya muda mrefu.

Mbaya zaidi unaweza usilale kabisa endapo utapatwa na maumivu ya jino usiku kama hauna uvumilivu unaweza kutoka usiku huo huo na kukimbia hospitali kwenda kung'oa.

Hata hivyo, hapa ninayo orodha za vyakula na viungo ambavyo huweza kusaidia kupambana na matatizo ya meno.

Jino linalouma au fizi zilizovimba: Ponda ponda tangawizi mbichi kisha itie chumvi. Weka kwenye jino linalouma au fizi ilipovimba.

Saga majani makavu ya 'mint' kutengeneza unga wake, kisha tia chumvi na weka kwenye jino linalouma.

Saga karafuu kuwa unga. Weka kiasi cha unga huo kwenye jino linalouma. Pia kama una mafuta ya karafuu, chukua nyuzi za pamba (cotton wool) chovya kwenye mafuta hayo na weka pamba hiyo kwenye jino linalouma.

Tiba hizi tunazo majumbani kwetu tunamoishi lakini tumekuwa hatujui kuwa ni tiba, badala yake huwa tunakimbilia kung'oa meno yanayouma.

No comments: