DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Showing posts with label michezo. Show all posts
Showing posts with label michezo. Show all posts

Wednesday, 9 November 2022

Tuesday, 8 November 2022

November 08, 2022

CHAMA NA AZIZI KI WAPIGWA NYUNDO NA TFF.

 

Wachezaji Cletous Chama wa Simba sc na Stephane Aziz Ki wa Yanga sc wamefungiwa michezo mitatu na adhabu ya faini ya shilingi milioni tano kwa kosa la kutosalimiana na wachezaji wenzao katika mchezo wa ligi kuu uliozikutanisha klabu zao Oktoba 23 mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na bodi ya ligi kuu nchini imesema kuwa wachezaji hao wamefungiwa kutokana na kuzingatia kanuni ya 41:5(5.4) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa wachezaji.

Kutokana na kufungiwa huku timu za Simba sc na Yanga sc zitaathirika sana kwa sababu wachezaji hao wamekua nguzo kubwa katika klabu hizo hasa katika kujenga mashambulizi na kupelekea kuwa na umuhimu mkubwa katika vikosi vya timu hizo huku Simba sc ikionekana kuathirika zaidi kutokana na kutokua na mbadala mwenye ubora wa kumfikia Chama katika eno analocheza.

Chama ataanza kuitumikia adhabu hiyo kesho ambapo klabu yake ya Simba sc itamkosa itakapocheza mchezo mkali na wa kusisimua dhidi ya Singida Big Stars katika uwanja wa Liti mkoani Singida ambapo tayari klabu ya Simba sc imeshawasili ambapo pia Chama ataikosa michezo mingine dhidi ya Ihefu na Namungo.

Stpehane Aziz Ki yeye ataikosa michezo dhidi ya Kagera Sugar ugenini siku ya Jumatatu pamoja na michezo dhidi ya Singida na ule wa Novemba 22 dhidi ya Dodoma jiji ugenini


Monday, 18 October 2021

October 18, 2021

WACHEZAJI WA CLUB YA YANGA WANAPOKEA MSHAHARA MKUBWA KWA MWEZI KULIKO WOTE

10: BAKARY  MWAMNYETO

Mchezaji huyu analipwa kiasi cha Tsh Milion 5 kwa mwezi


9: FEISAL  SALUM

Mchezaji huyu analipwa kiasi cha Tsh Milion 5 kwa mwezi


8: FISTON MAYELE

Mchezaji huyu analipwa kiasi cha Tsh  Milion 5.5  kwa mwezi


7: YANNICK  BANGALA

Mchezaji huyu analipwa kiasi cha Tsh Milion 6  kwa mwezi


6: FARID  MUSSA

Mchezaji huyu analipwa kiasi cha Tsh Milion 7 kwa mwezi


5: DJIGUI  GIARRA

Mchezaji huyu analipwa kiasi cha Tsh Milion 7  kwa mwezi


4: MUKOKO  TONOMBE

Mchezaji huyu analipwa kiasi cha Tsh Milion 8  kwa mwezi


3: DJUMA  SHABAN

Mchezaji huyu analipwa kiasi cha Tsh Milion 9  kwa mwezi


2: KHALID  AUCHO

Mchezaji huyu analipwa kiasi cha Tsh Milion 12  kwa mwezi


1: MA OLANG  MAKAMBO

Mchezaji huyu analipwa kiasi cha Tsh Milion  13 kwa mwezi

Gusa link hiyo kwa ajili ya kupata burudani ya Muziki muda wote wote na Dealplus online radio
                                      https://onlineradiobox.com/tz/dealplus/?cs=tz.dealplus&p=1



October 18, 2021

WACHEZAJI 10 WA CLUB YA SIMBA WANAPOKEA MSHAHARA MKUBWA KWA MWEZI KULIKO WOTE


Hawa ndio wachezaji 10 wa klabu ya simba amabo wanalipwa mshahara mkubwa zaidi kuliko wachezaji wengine 

                                                         10: JONAS  MKUDE  

 Analipwa Tsh milioni    6 kwa mwezi


9: TADEO  LWANGA  

 Analipwa Tsh milioni   6.5 kwa mwezi


8: JOASH  ACHIENG ONYANGO 

 Analipwa Tsh milioni  7 kwa mwezi


7: PAPE  OUSMANE  SAKHO

 Analipwa Tsh milioni   8 kwa mwezi


6: AISH  SALUM  MANURA 

Analipwa Tsh milioni  8 kwa mwezi


5:  RALLY  BWALYA 

 Analipwa Tsh milioni  9 kwa mwezi


4: JOHN RAPHAEL  BOCCO 

Analipwa Tsh milioni  10 kwa mwezi


3:  CHRISS KOPE  MUGALU

 Analipwa Tsh milioni   11 kwa mwezi


2:  MEDDIE  KAGERE 

 Analipwa Tsh milioni  12 kwa mwezi


1: BERNARD  MORRISON

 Analipwa Tsh milioni  12 kwa mwezi

Gusa link hiyo kwa ajili ya kupata burudani ya Muziki muda wote wote na Dealplus online radio
                                      https://onlineradiobox.com/tz/dealplus/?cs=tz.dealplus&p=1

Friday, 15 October 2021

October 15, 2021

WAJUE WACHEZAJI WATANO WA AFRIKA WALIOKARIBIA KUTWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA (Ballon d'Or)


q

Tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo mwaka 1956, ni mwafrika mmoja tu George Weah ambaye sasa ni rais wa Liberia, aliyewahi kutwaa tuzo hiyo, mwaka 1995. Lakini wapo wachezaji kadhaa wa Afrika waliokaribia kabisa kuibeba tuzo hiyo, lakini pengine uwepo wa Lionel Messi (Argentina) anayekipigia PSG aliyetwaa mara 6 na Cristiano Ronaldo (Ureno) wa Manchester United aliyetwaa mara 5 umepunguza fursa kwa waafrika wengi.

a

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

George Weah (kulia) akikabidhi tuzo yake ya Ballon d'Or aliyoitwaa mwaka 1995 wakati huyo akiichezea AC Milan kwa Rais wa Liberia wakati huo, Ellen Johnson Sirleaf. Ilikuwa June, 2013 kwenye mchezo maalumu wa amani. Weah ni Rais wa sasa wa Liberia na muafrika pekee kutwaa Ballon d'Or.

Nyota hawa wawili katika kipindi cha muongo mmoja uliopita wamekuwa watawala wa soka, wakibadilishana hii tuzo wao wawili. Katika miaka 14 iliyopita tangu 2008 ni mwaka 2019 pekee alitwaa Luka Modric wa Croatia na klabu ya Real Madrid, huku mwaka jana haikufanyika, lakini miaka mingine yote wamekuwa wakibadilishana.

Roger Milla, Abedi Pele, Nwanko Kanu, Jay-Jay Okocha, El Hadji Diouf na Yaya Toure haya ni majina makubwa kabisa katika soka la Afrika hakuna shaka kuhusu uwezo wao, lakini katika miongo miwili iliyopita, wafuatao ni wachezaji watano kutoka Afrika ambao walikaribia kabisa kutwaa tuzo hii ya Ballon d'Or

5 Didier Drogba (Ivory Coast)

Drogba

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Didier Drogba ni mchezaji mkubwa Afrika, ana tuzo 4 za mchezaji bora wa Ivory coast na tuzo 2 za mchezaji bora wa Afrika. Mwaka 2006 ulikuwa mwaka mzuri kwa Drogba akitwaa ligi kuu mara mbili mfululizo akiwa na Chelsea akitoa mchango mkubwa kwa timu hiyo. Drogba aliingia 10 bora ya tuzo ya Ballon d'Or na mwaka uliofuata aliingia tano bora licha ya kushindwa kuitwaa tuzo hiyo.

Mwaka 2007, alimaliza nafasi ya nne kwenye Ballon d'Or nyuma ya Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na mshindi wa tuzo hiyo, Kaka. Mwaka huo alikaribia kutwaa tuzo ya dunia lakini alishindwa hata kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, tuzo iliyokwenda kwa Frederic Kanoute, kutoka Mali.

4: Riyad Mahrez (Algeria)

Mahrez

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mahrez ni moja wa vipaji vikali kwenye historia ya soka Algeria, akiiongoza timu yake ya taifa kutwaa kombe la AFCON mwaka 2019.

Nahodha huyo wa Algeria ana kipaji kikubwa cha soka, akionekana kama dhahabu kuwahi kutokea kwenye soka la nchi hiyo. Mbali na kuwika na kutwa amataji akiwa na Manchester City, lakini soka lake la mwaka 2016 liliisaidia kuipa Leicester City taji la kihistoria la Ligi kuu England. Msimu huo alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi hiyo

Kwa mafanikio hayo, Mahrez aliingia 10 bora ya tuzo ya Ballon d'Or na kumaliza nafasi ya 7 ambayo wengi walimtabiria angeingia 5 bora. Hata hivyo kwa nafasi hiyo, ni mafanikio makubwa kwake.

3: Sadio Mane (Senegal)

mane

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Sadio Mane ni miongoni mwa magwiji wa soka Afrika na Senegal. Katika tuzo za Ballon d'Or Mane alimaliza nafasi ya 23 mwaka 2017, nafasi ya 22 mwaka 2018 lakini mwaka 2019 ulikuwa mwaka mzuri aliokaribia kutwaa tuzo hiyo akishika nafasi ya 4. Kama isingekuwa kulikosa kombe la AFCON Senegal ilipofungwa na Algeria kwenye fainali huenda angekuwa mwafrika wa kwanza tangu George Weah kutwaa tuzo huyo ya Ballon d'Or.

Hata hivyo Mane ana muda wa kutwaa tuzo hiyo kama atafanya vyema akiwa na Klabu yake ya Liverpool na timu yake ya Senegal kwenye mashindano mbalimbali yajayo. Anahitaji tu kura za kutosha

2: Mohamed Salah (Egypt)

Salah

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kwa sasa Salah anaonekana kama mchezaji bora duniani, kiwango chake katika misimu mitatu iliyopita akiwa na Liverpool, kinadhihirisha ubora wake na namna anavyoweza kuingizwa kwenye orodha ya magwiji wa soka kutoka Afrika.

Aliiongoza Misri katika kombe la dunia 2018 na amefanikiwa kumaliza kwenye sita bora ya tuzo ya Ballon d'Or mara mbili mfululizo kuanzia mwaka 2018. Mwaka 2018 alishika nafasi ya 5, na mwaka 2019 akawa wanne.

Ana nafasi nyingine msimu mwaka 2022 kutwaa tuzo hiyo ya Ballon d'Or kama ataendelea na kiwango chake cha sasa akiwa na Liverpool pamoja na Misri, ambayo inatarajiwa kuwemo kwneye mataifa matano yatakayofuzu kombe la dunia mwakani.

1: Samuel Eto'o (Cameroon)

etoo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Inawezekana huyu ndiye mchezaji bora wa Afrika kuwahi kutokea, licha ya majina mengine mengi kuwepo kama Roger Milla, Abedi Pele, Nwanko Kanu, Jay-Jay Okocha, El Hadji Diouf na Yaya Toure. Eto'o ameshinda makombe mawili ya AFCON akiwa na Cameroon. Ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara nne, na anatajwa ndiye muafrika aliyekaribia zaidi kutwaa Ballon d'Or.

Katika maisha yake ya soka, ameorodheshwa kwenye tuzo ya Ballon d'Or mara 10, ikiwa ni mara nyingi zaidi kuliko muafrika mwingine yoyote. Kwa mara ya kwanza Eto'o kuingia kwenye orodha hiyo ilikuwa mwaka 2004 alipomaliza wa 15, na katika miaka 8 iliyofuata hakuwa anakosa kwenye orodha ya juu ya wanaowania tuzo hio.

Alimaliza nafasi ya 10 kwenye Ballon d'Or ya mwaka 2005, mwaka 2006 alimaliza wa 7, 2007 akawa wa 30, 2008 wa 17, kabla ya mwaka 2009 akiwa na kiwango kikubwa kabisa kuingia 5 bora. Kufunga na kiwango bora kila mwaka akiwa na nyota kama Ronaldinho, Deco na Messi aliyekuwa anachipukia, E'too wa Barcelona na baadae Inter Milan iliyotwaa ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2010 alikuwa moto wa kuotea mbali. Wengi walimuona kama alistahili kutwaa tuzo hiyo katika wakati wake.

                                                                chanzo. BBC

Gusa link hiyo kwa ajili ya kupata burudani ya Muziki muda wote wote na Dealplus online radio
                                      https://onlineradiobox.com/tz/dealplus/?cs=tz.dealplus&p=1

Friday, 1 October 2021

October 01, 2021

BUMBULI ATOA TAMKO LA KISHUJAA:TUNATAKA KUKAA KILELENI



Kulekea mchezo wa kesho kati ya Yanga na Geita gold afisa habari wa klabu ya Yanga Hassan Bumbuli amesema anaitakia timu hiyo ushindi ili timu yao ikae kileleni.

"Kesho tunataka kushinda na kuongeza alama ili tukae kileleni mwa ligi maana kuna watu wanatubanabana pale tunataka kila mtu akae katika nafasi yake'. Bumbuli 

Thursday, 16 September 2021

September 16, 2021

MASAU BWIRE AFUNGUKA ALIVYOKABIDHIWA MIKOBA YA HAJI MANARA SIMBA



WAKATI jina la Masau Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting likitajwa kuibukia mitaa ya Msimbazi kubeba mikoba ya Haji Manara, kiongozi huyo amefungukia namna mabosi wa Simba walivyompa ofa ili awe ndani ya kikosi hicho.
Kwa sasa nafasi ya Ofisa Habari wa Simba ipo mikononi mwa Ezekiel Kamwaga ambaye anakaimu nafasi hiyo na aliweka wazi kuwa atasepa hivi karibuni kwa kuwa mchakato wa kumtafuta mbadala wake unaendelea.
Akizungumza na Championi Jumatano, Masau alisema kuwa Simba walimfuata zamani ili awe kwenye kitengo cha usemaji lakini alikataa kwa kuwa roho wa Bwana hakumpa ruhusa kufanya hivyo.
“Kuna vitu viwili unaweza kuvichanganya,kwamba mimi pengine nafurahia kwenda kufanya kazi Simba pengine ningekuwa napenda kufanya hivyo ningefanya kazi siku nyingi sana kwa sababu Simba waliwahi kunifuata ili nikafanye kazi pale.
Simba waliwahi kunihitaji siku nyingi tena kwa nguvu lakini bado roho wa Bwana alikuwa hajaruhusu walinifuata sana nilikataa ilikuwa zama za utawala wa Aveva, (Evans) na Kaburu, (Godfrey Nyange) pengine ningekubali mimi pengine Manara, (Haji) asingekuwepo pale.

Thursday, 19 August 2021

August 19, 2021

TANZIA: MWALIMU KASHASHA AFARIKI DUNIA

 

Mchambuzi nguli wa mpira wa miguu hapa nchini Tanzania Alex Kashasha amefariki dunia leo tarehe 19/08/2021 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya kairuki jijini Dar es salaam. Mwalimu kashasha alikuwa mchambuzi wa mpira wa miguu katika televisheni ya taifa na ikumbukwe kuwa mwalimu kashasha alikuwa na mchango mkubwa sana kwenye soka la Tanzania ambapo alikuwa akiwavutia wanasoka wengi kwa ubobezi wake katika tasinia hiyo ya mpira wa miguu. 

BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina lake lihimidiwe 




Wednesday, 18 August 2021

August 18, 2021

Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 18.08.2021: Ronaldo, Kane, Ramsdale, Pogba, Mbappe, Zouma

 

Christiano Ronaldo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Christiano Ronaldo

Wakala wa mshambuliaji wa Juventus Cristiano Ronaldo', Jorge Mendes ameipatia Manchester City ofa ya kumsajili nyota huyo wa Portugal mwenye umri wa miaka 36. (Corriere dello Sport - in Italian) (Corriere dello Sport - in Italian)

Lakini City inasisitiza kwamba bado inamlenga mshambuliaji huyo wa Tottenham na England Harry Kane, 28,. (Mirror)

Baada ya kukosa mazoezi na ushindi dhidi ya City, Kane ataichezea Spurs katika Ligi ya Europa dhidi ya klabu ya Porugal Paços de Ferreira Alhamisi. (Guardian)

Arsenal imeanzisha tena mazungumzo na Sheffield United juu ya makubaliano ya mlinda lango, 23, wa England Aaron Ramsdale, baada ya Blades kusemekana kwamba wamepunguza dau lao kutoka £35m hadi £24m. (The Athletic, subscription required)

Maelezo ya picAaron Ramsdale

Na kocha wa Sheffield United Slavisa Jokanovic amekubali kuwa Ramsdale anataka kujiunga na Arsenal. (Mirror)

Paris St-Germain haijaondoa uwezekano wa uhamisho wa dakika za mwisho wa viungo wa kati raia wa Ufaransa Paul Pogba, 28, kutoka Manchester United na Eduardo Camavinga,10 kutoka Rennes. (L'Equipe - in French)

PSG ina nia ya kumuuza mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 22, kwa Real Madrid msimu huu. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Tottenham inafikiria uhamisho wa mlinzi wa Chelsea Kurt Zouma. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa, 26, pia amehusishwa na uhamisho wa West Ham msimu huu. (Sky Sports)

Kylian Mbappe

CHANZO CHA PICHA,EPA

Atletico Madrid imeiambia Arsenal na Manchester United kwamba beki wa kulia wa England Kieran Trippier, 30, hauzwi. (AS)

Uhamisho wa kudumu wa Martin Odegaard kutoka Real Madrid hadi Arsenal unakaribia huku kukiwa na taarifa kwamba kiungo huyo wa kati, 22 hakushiriki mazoezi na timu ya Real Jumanne. (The Athletic, subscription required)

Wolverhampton Wanderers inajitayarisha kutoa ofa ya £21m kwa Valencia ikimlenga winga wa Ureno Goncalo Guedes, 24. (Birmingham Mail)

Kocha wa Newcastle Steve Bruce anamuwinda kiungo wa kati wa Leicester Hamza Choudhury, 23, kwa mkopo. (Mail)

Martin Odegaard

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mchezaji wa Everton James Rodriguez amekanusha taarifa kwamba anatafuta uhamisho wa kjuelekea Atletico Madrid, baada ya ujumbe wa Twitter wa mchezaji huyo, 30, wa Colombia kuchukuliwa kama kidokezo kwamba anahamia kwa mabingwa wa La Liga. (Liverpool Echo)

Watford inakaribia kukubali kima cha £7.5m kwa ajili ya mlinzi Mbrazil wa klabu ya Torino Lyanco, 24. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Manchester United Andreas Pereira, 25, huenda anakaribia kuondoka Old Trafford huku kukiwa na tetesi kwamba anaelekea Flamengo kufuatia mapendekezo mengi ya mkopo kwa Mbrazil huyo. 

Friday, 13 August 2021

August 13, 2021

KASSIM MAJALIWA NA DKT. MOTSEPE RAIS WA CAF WAJADILIANA KUKUZA MICHEZO TANZANIA

 


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 

 

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo amekutana na Rais wa Shirikisho la Mpira barani Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe na kujadiliana naye masuala muhimu ya kuendeleza michezo nchini.

 

Akizungumza na Dkt. Motsepe ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma leo (Ijumaa, Agosti 13, 2021), Waziri Mkuu amemweleza mikakati ambayo Serikali inatumia ili kuinua kiwango cha soka nchini.

 

“Sisi tumeanza kuboresha michezo nchini chini ya mpango unaohusisha Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia; Ofisi ys Rais TAMISEMI na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mpango huu unalenga kuibua vipaji vya vijana kupitia mashindano ya UMITASHUMTA, UMISETA, Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati,” amesema.

 

Katika mazungumzo yao, walijadiliana suala la kuendelea kutenga bajeti ya kuinua michezo kwa vile nchi nyingi zinashindwa kufanya vizuri kwenye michezo kwa sababu hazitengi bajeti. “Nimemweleza kuwa hapa kwetu kupitia Bunge letu tukufu, tumekuwa tukitenga bajeti hiyo japokuwa tunajua kuwa haitoshelezi mahitaji yote.”

 

“Kuhusu uendelezaji wa michezo nchini, Rais wa CAF ametusihi tuwe na mpango madhubuti wa kupata maeneo ya kufanyia mazoezi, tuwe na viwanja bora vyenye vipimo vya kisasa, jambo ambalo nimemweleza linatekelezwa na shirikisho la soka nchini. Pili, ametutaka tuandae vijana kuanzia umri mdogo, tuwe na taasisi za Serikali na za sekta binafsi zinazofundisha soka, waamuzi, makocha ili tuwaibue akina Samatta wengi zaidi kwani na sisi tunaamini kuwa wapo.”

 

Kwa upande wake, Dkt. Motsepe amesema katika uongozi wake amelenga mambo makuu matatu ambayo ni haja ya sekta binafsi kuwekeza kwenye michezo na kuongeza udhamini; ujenzi wa vituo vya michezo (sports academies) na vituo vya kuendeleza vijana (youth development centres).

 

Amesema chini ya mfuko wa dola bilioni moja (One Billion Dollar Fund), amedhamiria kuimarisha miundombinu ya michezo. Kuna baadhi ya nchi za Afrika zina viwanja vikubwa vya michezo lakini havijakidhi vigezo vya FIFA. Tunataka na wao wafikie viwango vya kimataifa,” amesema.

 

Amesema timu ya Taifa ya Tanzania ina uwezo kuwa timu bingwa barani Afrika kutokana na umahiri walionao hivi sasa na ametumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake za kuunga mkono michezo nchini ambapo wiki ijayo atapokea kombe la CECAFA - 2021 la vijana wenye umri chini ya miaka 23.

 

Ameipongeza Tanzania kwa kuwa nchi ya kuigwa kutokana na wananchi wake wengi kupenda michezo na hasa kunapokuwa na mechi zinazokutanisha vilabu vikubwa nchini kwa vile zinawaleta mashabiki hata kutoka nchi jirani.

 

(mwisho)

 

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

41193 - DODOMA,                      

IJUMAA, AGOSTI 13, 2021