DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Showing posts with label udukuzi. Show all posts
Showing posts with label udukuzi. Show all posts

Friday, 16 June 2017

June 16, 2017

WAPELELEZI 10 WANAONGOZA KWA KUFANYA UPELELEZI WA HALI YA JUU TOKA KUANZA VITA YA PILI YA DUNIA HAWA HAPA


10 Of The Most Famous Spies In History

Source: Wikipedia

These spies made a name for themselves at home and abroad for their compelling mixture of sex, scandal and secret dealings. Here are 10 of the most dubious, famous spies in history.

Famous Spies: Mata Hari, German Spy

Source: The Guardian

Possibly one of the most famous spies of all time, Mata Hari was an exotic dancer and high class prostitute in Paris who spied for Germany during World War 1. The Dutch-born Margaretha Geertruida Zelle began her spying career after working as a courtesan to high-ranking military men and politicians. Her courtesan status and Dutch passport (Netherlands was a neutral country) allowed her to, literally, sleep with the enemy and gather intel for the German Military.

Mata Hari’s gig came to a halt in January 1917, when French intelligence intercepted a German Military Attache-encoded radio signal to Berlin which declared that they were receiving amazing information from a German spy codenamed H-21. Mata Hari was identified and arrested in a Paris hotel room on February 13, 1917. She was executed by Firing Squad on September 15, 1917 for espionage.

Source: Stuff You Should Know

The Rosenbergs, Soviet Union Spies

Source: Ielmira

Married couple Julius and Ethel Rosenberg were American Communists who were executed in 1953 for passing nuclear secrets to the Soviet Union. The couple became embroiled in espionage in 1942, when Julius was recruited by the KGB. He was responsible for passing classified reports and designs to the KGB, including a fuze design which was used to shoot down a U-2 in 1960. He was assisted by his brother-in-law, Sergeant David Greenglass, who admitted to passing on classified information through Julius and Ethel (who typed nuclear secrets).

While the degree of Ethel’s involvement was relatively uncertain, prosecutors thought that indicting her would cause her to get Julius to confess. That never happened. The case against them began in 1951 and both were found guilty of conspiracy to commit espionage and executed by electric chair in Sing Sing Prison in 1953. They were the only two American civilians to be executed for espionage during the entire Cold War.

Source: NPR

Famous Spies: Aldrich Ames, Soviet Union Spy

Source: NPR

Former CIA agent Aldrich Ames turned Soviet Union spy in 1985 after being stationed in Ankara, Turkey. He had originally been sent to target Soviet intelligence officers for recruitment, but instead offered up US secrets to the Soviets due to his own financial and emotional woes. Assigned to the CIA’s European office, Ames had access to the identities of CIA operatives in the KGB and Soviet Military, and provided the Soviets with this intel.

This led to the compromise of about 100 CIA agents and the execution of at least 10. It was Ames’ newly-acquired material wealth that did him in. Ames passed two lie detector tests while spying for the Soviet Union, but he couldn’t hide his Soviet-funded half million dollar home, luxury sports car, or thousand dollar phone bills from the CIA. He was eventually caught by the FBI and in 1994 convicted to life in prison.

Giacomo Casanova, Venetian Spy

Source: Wikipedia

The original Casanova was a Venetian spy who wrote a tell-all book called The Story of My Life. The book, however, details mostly his romantic affairs with powerful women, and he tends to gloss over the escapades of his espionage days. What is known that he worked as a lawyer, and between the years of 1774 and 1782 served as a spy for the Venetian Inquisitors of the State. His spying endeavors are hush hush, but he eventually was exiled in 1782 for spreading libel against one of the City patricians.

Famous Spies: Klaus Fuchs, Soviet Union

Source: Wikipedia

In the long list of Soviet spies we find the name of Klaus Fluchs, a German-born physicist with the distinction of being responsible for significant theoretical work on the first fission weapons and early models of the hydrogen bomb. After fleeing Germany during the Nazi regime, Fuchs worked on his PhD in England and made the cut for the British atomic bomb project. In 1943, Fuchs also found his way to Los Alamos, where he was an integral part of the Manhattan project.

During his time in England, Fuchs turned spy and began giving information to the Soviets, reasoning that they deserved to know what the enemy was developing. This passing of information took place over two years, as Fuchs continued to provide information to the KGB on key products including theoretical plans for building a hydrogen bomb, and data that Soviets used to determine the number of bombs the US possessed. He was interrogated in 1946 by the British government and was sentenced to 14 years imprisonment, but only served nine.

Major John André, British Spy

Source: Wikimedia Commons

Major John André was a British Army officer during the American War of Independence who conspired against the Continental Army. He was a well-liked major in colonial society during the British occupation in Philadelphia and New York, but behind closed doors was responsible for assisting American General Benedict Arnold’s attempts to sell the West Point fort in New York to the British. He was caught after traveling through New York in civilian clothes with a fake passport. André’s defense? He never wanted or planned to be behind American lines, and that as a prisoner of war he had the right to escape in civilian clothes. The board was unmoved. André was convicted of being a spy for the enemy, and was hanged on October 2nd, 1780.

Famous Spies: James Armistead Lafayette

Source: Fine Art America

Lafayette was the first African-American double agent and came to prominence during the American Revolution. A slave by William Armistead of Virginia, he was granted permission to volunteer in the army in 1781. His missions included spying on the Brigadier General Benedict Arnold, and his reports were vital in helping defeat the British forces during the Battle of Yorktown.

Frederick Joubert Duquesne, German Spy

Source: List25

Frederick Joubert Duquesne, nicknamed “Black Panther”, was a German spy during both world wars. Fueled by his hatred of the British and their treatment of Boer children and women, he turned to espionage and was responsible for relaying secrets—particularly about Allied weaponry and shipping movements—to the German forces. He is also credited for having sabotaged and sunk the HMS Hampshire in 1916, which was carrying Lord Kitchener to Russia. Duquesne also organized the Duquesne Spy Ring whose 33 conspiring members were sentenced 300 years in prison.

Famous Spies: Virginia Hall, US Spy

Source: NPR

Known by her moniker “Artemis” in Germany, Virginia Hall was a US spy who worked with the Special Operations Executive during World War II in the 1940s and later for a division of the CIA. Her efforts included helping the French Underground in Vichy and the French resistance as a correspondent, and the Gestapo referred to her as “the most dangerous of all Allied spies”. Oh, and she only had one leg – the other was amputated from the knee down.

Source: Blogspot

Shi Pei Pu, Chinese Spy



Source: Back Of The Cereal Box

A clandestine story of sex, scandal and an Opera singing spy occurred in Beijing in 1964. Chinese opera singer Shi Pei Pu met French embassy clerk Bernard Boursicot while teaching English to diplomats’ families, convinced Boursicot that he was a woman dressed as a man, and began a love affair with him that spanned 20 years – even going as far as pretending to have his baby (that he purchased from a hospital).

The affair resulted in Boursicot handing over as many as 150 French embassy documents to the Chinese secret service before returning to France in the early 1980s. Eventually Shi and his “son” were arrested and charged with espionage, serving six years in prison. They were released after 11 months and Shi’s story inspired the play and film, M. Butterfl

Saturday, 3 June 2017

June 03, 2017

FAHAMU HISTORIA YA KONDOMU ILIPOANZIA NA JINSI KONDOMU YAKWANZA ILIVYOGUNDULIWA NA KUTENGENEZWA

Fahamu Historia ya Condom..Ilipoanzia na Jinsi Ilivyogundulika na Kuanza Kutumika kwa Mara ya Kwanza..!!!


KONDOMU ni kifaa/ zana iliyotengenezwa mahususi kuvalisha uume au kuwekwa ukeni wakati wa kujamiiana.Nazo hubana kutokana na umbile la uume au uke.

Kondomu hizi zipo za aina tofauti kutokana na muda na vipindi zilipotengenezwa, nazo ni kama ifuatavyo:-

Awamu ya I – zilizotengenezwa kwa mimea.

Hizi zilitengenezwa mahususi kama kinga dhidi ya maambukizo ya vimelea vya ugonjwa wa kaswende [ugonjwa wa kifaransa]

Awamu ya II – kutokana na utumbo wa kondoo.

Dr. Condom alifahamika kama mgunduzi wa kondomu hizi, naye alikuwa ni dakatari wa Mfalme Charles II.

Alimshauri Mfalme kutumia kama kinga kutokana na magonjwa ya zinaa kutokana na tabia yake ya kuwa na wanawake wengi nje ya ndoa yake.

Awamu ya III – kutokana na mpira

Hizi zilitengenezwa kwa urahisi na kwa wingi na zikawa ndizo pekee zenye uwezo wa kudhibiti mimba hadi miaka ya 1960 vilipogunduliwa na vidonge vya majira.

JE KONDOMU NI SALAMA?

Tunaelezwa kuwa kondomu hutengenezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba haziwezi kuruhusu kitu chochote kupita.

Lakini tafiti mbalimbali zilizofanyika zinaonyesha kuwa kondomu zaweza kuvuja kutokana na mazingira halisi ya utengenezaji wa latex.

Wengine wanadai kuwa ili kuzifanya imara, kondomu zimetengenezwa kwa kupishanisha pande mbili ili kuziba udhaifu wa kila upande.

Hata hivyo watengenezaji wanasahau kuwa mazingira ya matumizi ya kondomu katika ngono hayalingani na majaribio waliyofanya ya kujaza maji au hewa ili kupima kama maji na hewa vinapita.

Katika tendo la ngono ipo misuguano ya namna mbalimbali inayosababisha kubadilisha mazingira ya kondomu na kuidhoofisha.

Kutokana na tafiti hizo imefahamika kuwa kondomu hazina uwezo wa kuzuia mbegu za kiume kupenya wakati wote.

Upana wa kipenyo cha mbegu ni makroni 5 wakati upana wa kipenyo cha kirusi cha ukimwi ni makroni 0.1

Kwa maneno mengine mbegu ya kiume ni kubwa mara 50 ya kirusi cha ukimwi.

Vile vile tafiti zimeonyesha kuwa kondomu haina uwezo wa kuzuia maambukizo ya magonjwa ya zinaa vikiwemo virusi vya ukimwi kwa kiwango cha asilimia mia moja.

Hivyo tunaweza kusema kuwa, kondomu si salama kwa asilimia mia moja.

Kondomu zina kiwango cha kushindwa cha kati ya asilimia 10 na 15 na wengine wanasema hata asilimia 20.

Wasambazaji na wahamasishaji wa matumizi ya kondomu hawapendi kusikia ukweli huo na wanafanya jitihada kubwa ya kuficha ukweli huo.

Matangazo yatolewayo kupitia mabango ya barabarani, katika televisheni, radio na hata magazeti yanawarubuni watu yakiwaaminisha kuwa kondomu humkinga mtumiaji kwa kiwango cha asilimia 100%

Huko ni kukengeusha ukweli na kukiuka maadili ya kitaaluma.

Wengi kama sio wote wateteao matumizi ya kondomu hufanya hivyo kwa sababu ya maslahi ya kifedha na kibiashara.

Tukiongozwa na dhamiri safi, lazima tukiri ukweli uliopo na tuwaeleze watumiaji, ili tusijekuwa sababu ya kifo chao.

Kila kondomu inaposhindwa [itumikapo] kama kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya ukimwi ] humaanisha kifo.

Udhaifu wa kondomu Kiufundi,Matumizi, Kimazingira

Udhaifu wa kiufundi

Wasambazaji wanatueleza kuwa kondomu zilizotoka kiwandani zikiwa na ubora unaotakiwa zikitumika wakati wote na kwa usahihi zina uwezo wa kukinga kwa kiwango hadi cha asilimia 97.

Zisipotumika vizuri zina kiwango cha kushindwa cha asilimia 14.

Kiwango cha kushindwa kwa kondomu kuzuia maambukizo ya magonjwa ya zinaa hutofautiana kutokana na aina ya magonjwa ya zinaa.

Kondomu zaweza kuzuia kwa kiwango fulani maambukizo ya magonjwa ya zinaa yanayosafiri kwa njia ya ute, lakini haziwezi kuzuia magonjwa ya zinaa yanayoambukizwa kwa mgusano wa mwili kama vile "herpes" na "human papillomavirus"; au magonjwa yanayoambukizwa kutokana na vidonda au malengelenge yaliyoko kwenye via vya uzazi kama vile kaswende.

Hali hiyo inatokana na:

Watengenezaji wameruhusu udhaifu wa kiufundi kama zao la kiwandani lililotengenezwa na kazi ya mikono ya binadamu [acceptable quality limit] kwa kiwango Fulani kwa nchi mbalimbali. 

Mfano, Marekani kiwango kilichokubaliwa ni asilimia 99.6 kwa kutoruhusu kondomu kuvuja. 

Uingereza asilimia 97, Uholanzi asilimia 96. 5. Hivyo katika kila idadi ya kondomu itumikayo kwa wakati mmoja kuna kiwango cha kuvuja kati ya asilimia 0.4 (USA); 3% (Britania); 3.5% (Holland).

Kondomu huzeeka

Kwa kadiri zisivyotumika kwa muda mrefu ndivyo hivyo zinaaendelea kuzeeka. 

Kwa hiyo mtumiaji kondomu wa miaka 3 au 4 baada ya kondomu hiyo kutengenezwa yumo katika hatari zaidi kuliko anayetumia kondomu mara tu baada ya kutoka kiwandani.

Utafiti mmoja umeonyesha kuwa kiwango cha kupasuka kwa kondomu kiliongezeka kutoka 3.6% kwa kondomu mpya hadi 18.6% kwa kondomu zilizotumika miaka kadhaa baadaye.

Kondomu hupasuka.

Kiwango cha kupasuka hutegemea aina ya kilainisho kilichotumika na aina ya kondomu. Kwa mujibu wa tafiti 15 zilizofanywa na "Contraceptive Technology" yalionyesha kuwa katika kondomu 25,184 zilizotumika 4.64% zilipasuka.

Ingawaje kondomu za latex zinaonekana kuwa na kiwango kidogo sana cha kupitisha virusi vya ukimwi, hatari kubwa ya matumizi yake imo katika uwezekano wa kondomu kupasuka, kuteleza na kuteleza.

Kwa hiyo hata kama ni virusi vichache tu vinaweza kupenya, kiwango cha maambukizo kitakuwa kikubwa kadiri kondomu zinavyosambazwa kwa wingi na kadiri watu wanavyojihusisha na vitendo vya ngono wakiamini katika matumizi ya kondomu.

Udhaifu katika matumizi

Matumizi mabaya: yaani kutovaa vizuri, kuvaa nje ndani, aina ya ngono, urefu wa muda wa ngono, pia kutokana na uelewa mdogo hasa kwa wasojua kusoma na kuandika na wale wakaao mbali na mijini.

Kuteleza na kuvulika kutokana na hali ya uume kuwa mdindifu au la; upana au wembamba; mrefu au mfupi. 

Pia kutokana na tendo la ngono na hali ya mtumiaji na mazingira ya matumizi. 

Kutokana na umri wa mtumiaji, kama ni mtoto, kijana, mtu mzima au mzee.

Kutumia kondomu ambazo muda wake umepita. Mfano wanaotumia gizani , katika hali ya ulevi, kutokujua kusoma, kuchunguza na kugundua kama muda wake umepita.

Mazingira ya kingono yakishawekwa, watu wanatawaliwa na mihemuko ya juu ya ngono kiasi kwamba hawawezi kuchunguza tarehe ya ukomo wa matumizi ya kondomu.

Ingawa watengenezaji wanashauri kutotumia kondomu iliyobadilika rangi au iliyokauka, tabia za watumiaji hazina nafasi ya kuzingatia ushauri huo.

Lengo la mtumiaji laweza kusababisha matumizi kuwa mabaya. Mtu mwenye virusi vya ukimwi, anajiwekea lengo kwamba hataki kufa peke yake, atafanya jitihada za kutokutumia vizuri ili mwenzake [ambaye anaamini hajaambukizwa] aweze kuambukizwa ili, "nisife peke yangu".

Vilevile katika siku hizi za dawa za kupunguza makali ya kuzaliana virusi vya ukimwi, mtu anaweza kuonekana mwenye afya nzuri kabisa, na anaweza kumshawishi mwenzake kuachana na kondomu kwa vile "wanaaminiana".

Kwa hiyo mambukizi yanaweza kuwa makubwa kutokana na kutowadhibiti wale waliokwisha ambukizwa.

i.udhaifu wa kimazingira

Huu unatokana na hali zifuatazo:- kibinadamu, kimaumbile na Kibinadamu.

Udhaifu wa kondomu waweza kusababishwa na usafirishwaji, yaani muda unaotumika kusafiri kutoka sehemu zinapotengenezwa hadi mahali zinapotumika;

ii. Kimaumbile

Vyombo vya usafirishaji na usalama wa vyombo hivyo;

Kondomu zinazosafirishwa katika meli, zikiwa baharini kwa miezi kadhaa kabla hazijafika katika nchi lengwa na katika hali ya joto ndani ya makontena zinakuwa na kiwango hafifu katika ubora wake

Wednesday, 17 May 2017

May 17, 2017

MDOMO WA MPONZA AFANDE SELE HARMORAPA ATANGAZA KUMNYOSHA

Mdomo wamponza afande sele

Msanii Harmorapa amefunguka na kumkumbusha Afande Sele kuwa hata yeye heshima aliyonayo sasa kwenye muziki haikuja tu kwani hata yeye alianzia chini kama ambavyo yeye ameanzia na baadaye ndiyo akawa msanii mkubwa. 

Harmorapa amefunguka hayo kufuatia rapa huyo mkongwe kumdiss na kusema anabebwa tu na P Funk Majani, hivyo Harmorapa anasema yeye hataki kuongea sana bali anaaziachia kazi zake zimnyooshe Afande. 

Ikumbukwe Afande Sele siku za hivi karibuni amekuwa mara kwa mara akiingia katika kujibishana na kutofautiana na wasanii mbali mbali kutokana na mitazamo yao

Tuesday, 16 May 2017

May 16, 2017

WEMA SEPETU ABADILISHA MUONEKANO TAZAMA PICHA ZA MUONEKANO WAKE MPYA

Tazama muonekano mpya wa Wema Sepetu

Supastaa wa filamu za Kibongo, Wema Sepetu, ametupia picha mpya kwenye akaunti yake ya Mtandao wa Instagram, zikimuonesha akiwa na mwonekano mpya ambapo muda mfupi baadaye, mashabiki zake walianza kutoa maoni yao, wengi wakionesha kufurahishwa na mwonekano wao mpya.

Mashabiki hao wamembatiza Wema kwa jina jipya, wakimuita Malkia wa Instagram Tanzania. Picha hizo zimepigwa na Bernard Atilio.






May 16, 2017

JACK WOLPER AKATAA KUWAHI KUACHWA KATIKA MAISHA YAKE

JACK Wolper “Kwenye Maisha Yangu Sijawahi Kuachwa, Sina Kabisa Record Hiyo"

Msanii wa filamu Jacqueline Wolper amefunguka kuizungumzia ishu ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake, Harmonize. 

Muigizaji huyo amedai hana msongo wa mawazo kutokana na tukio hilo huku akidai hajaachwa kama baadhi ya watu kwenye mitandao wanavyodai. 

“Kuachwa ndio nini? kweli ulilolijua ni kama usiku wa giza,” Wolper alikiambia kipindi cha U Heard cha Clouds FM. “Kwenye maisha yangu sijawahi kuachwa, sina kabisa record hiyo sema sitakagi kufanywa mjinga. Yeye kama amezungumza ishu ya kuachana na mimi, mimi sitaki kulizungumzia kwa sababu na mambo yangu mengi ya umuhimu nafanya,”

Harmonize hivi karibuni alifunguka na kuweka wazi kwamba hayupo tena kwenye mahusiano ya mrembo huyo kutoka tasnia ya filamu huku akishindwa kueleza sababu.

May 16, 2017

ALIYEKUWA MKE WA SUGU AKINUKISHA TENA MTANDAONI

ALIYEKUWA Mke wa Sugu Faiza Ally Akinukisha Tena Huko Instagram

Msanii wa filamu, Faiza Ally ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, amefunguka mengi kuhusu watu wanaomfuatilia kupitia mitandao ya kijamii. 

Faiza Ally 

Muigizaji huyo ambaye alikuwa mke wa mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi aka Sugu, amedai anaumizwa sana na komenti hizo kutoka mitandaoni. 

“Huna hizi komenti huwa nazichukia sana na huenda mkawa mnahisi labda zina nifurahisha, oh nilikua sikuelewi sasa nimekuelewa,  oh wakuseme kwa yote sio malezi, yote yapi unayo yajua wewe kuhusu maisha yangu?.  Oh siku hizi umetulia hivi unanijua mimi mpaka unasema as ni kama mtu anae nifahamu sana?.  Hivi mna jua maana hizi comment kweli?,”  Faiza Ally aliandika Instagram. 

Aliongeza, “Nikikuuliza yapi mengine utajibu nini ? . Chupi au kipande cha tako? ni nini unacho kijua kwenye maisha yangu zaidi ya mavazi ?. Je hayo ndio yanayokupa nafasi ya kunijua mimi ni nani? Guys pls stop that stupid comment on my page I am more than that sawa????? First you all should know kuwa mama ni jukumu so haliingilini na chochote… nikikwambia sifa nilizo nazo kwangu kwenye familia yangu pengine no one of you mnazo au mnaweza kunifikia kwa hivyo nina jisikia vibaya vijitu vya insta visivyo jielewa just be coz vimeona picha za tako na chupi au vimebebwa na mabwana wenye hela au labda vimeolewa basi kujifanya vinaweza kunijaji! Ktk maisha yangu mm ni bora zaidi ya yoyote … sio mwenye digrii wala kiongozi wala mke wala yoyote ! Na to cut long story short sijaanza kumlea tu sasha nimeanza kulea familia in a very young age and i maneji kusomesha Watoto zaidi wa tatu na mmoja Leo yuko form four sawa ?? So I am not only a mom … ni shangazi,ni dada,na mama wa mama Yangu na baba Yangu mzazi… na sikukua na elimu wala sikua na jina la baba wala la yoyote na sijawahi kuwa mdananda kwa namna yoyote …. I AM WHO I AM TODAY BE COURSE OF ME …. nguvu zangu akili,zangu uwezo wangu ndio umenifanya niwe mm bila hata kutegemea ada ya nyumbani… na sibebwi na jibeba !!!! save ur stupid comment kwa wajinga wenzio i am not one them !!!! 😏,”

Monday, 15 May 2017

May 15, 2017

ROSE MUHANDO AMTAJA ANAYEMTISHIA KUMUUA HUYU HAPA

ROSE Muhando Afunguka


MWANAMAMA Rose Muhando ni staa mkubwa wa Nyimbo za Injili Bongo. Rose ana sauti kali, lakini ya kuvutia watu, yenye kupenya vilivyo kwenye ngoma za masikio ya msikilizaji na kuibua hisia na msisimko wa aina yake.

Rose ambaye amezaliwa mwaka 1976 huko Kilosa mkoani Morogoro anajulikana kwa utunzi wa mashairi ya kumtukuza Mungu. Midundo ya nyimbo zake ni za kuchezeka kwenye ‘Disko la Yesu’.

Mbali na sifa hizo, pia ana uwezo mkubwa wa kumiliki jukwaa. Kubwa kuliko ni kwamba ana nyimbo nyingi zinazoimbika kwa watu wa rika mbalimbali bila kujali imani za kidini. Baadhi ya nyimbo zake ni Nibebe, Utamu wa Yesu, Jipange Sawasawa, Chineke, Sitanyamaza, Nipe Uvumilivu, Facebook na nyingine kibao.

KWA NINI ROSE?

Kinachonifanya kuandika makala haya ni mahojiano ya Gazeti la Ijumaa Wikienda na Rose wiki iliyopita ambayo yalijaa maswali mengi hasa nikitaka kujua ni kwa nini Rose amekuwa katika hali aliyokuwa nayo yenye kusikitisha mno?

Rose mwenye umri wa miaka 41 alilieleza Wikienda namna anavyotishiwa kuuawa na mtu aliyekuwa akimlazimisha kufanya mambo asiyoyataka na kwamba hali ni mbaya, akitamani kuhama nchi ili kuinusuru roho yake.

NI KWELI ROSE NI TEJA?

Lengo la mahojiano hayo lilikuwa ni kupata ukweli kuhusiana na skendo inayomtafuna Rose juu ya kuwa teja. Madai yalikuwa ni kwamba Rose anatumia madawa ya kulevya ambayo yamemfanya kuwa mgonjwa, kukongoroka na kudhoofu mwili kiasi cha kutokuwa na tofauti na mateja wengine mitaani.

AANGUA KILIO

Kabla ya kujibu swali hilo, mara tu baada ya Wikienda kujitambulisha, Rose alianza kuangua kilio kwa uchungu na sauti ya juu akilalamika kuwa anaumwa sana na ameshahangaika na maisha haya bila msaada wowote na kwamba ameshatumika sana kutajirisha watu.

Ili mahojiano hayo yafanyike kwa utulivu, ilibidi kumtuliza kwanza Rose aliyeonesha kuwa na jazba mno.

Baada ya kutulia kidogo huku akiendelea kulia kwa kwikwi na kuombwa kunyamaza kila dakika, aliulizwa kinachomsibu ambapo alisema kuwa, anateswa na Ugonjwa wa Typhoid (Homa ya Matumbo) na mwili kuuma na kukosa nguvu hivyo kujiuguza mwenyewe nyumbani kwake, Ipagala, nje kidogo ya Mji wa Dodoma bila msaada.

ATISHIWA KUUAWA

Rose akasema muda mrefu sasa amekuwa akitishiwa kuuawa huku akipokea kichapo cha polisi ambacho humsababisha kuzimia, kwa kile alichodai kukataa kulala kwa maana ya kufanya ngono na mtu huyo.

Kwa mujibu wa Rose, amefikia hapo alipo kwa sababu alikataa kutekeleza jambo hilo kwa kuwa mhusika ni mume wa mtu na kwamba hata kama angekuwa si mume wa mtu, lakini huwa hana muda na mambo hayo.

Rose, bila kumtaja mhusika, anasema kuna mtu aliwahi kumsaidia kuingia studio kurekodi baadhi ya albamu zake, kwa sharti la kulala naye, lakini alipokataa ndipo manyanyaso na vitisho dhidi yake kutoka kwa mtu huyo vikaanza.

ANYANG’ANYWA MALI

Kwa mujibu wa Rose, mtu huyo aliwahi kudiriki kumnyang’anya mali zake, yakiwemo magari na vitu vingine vya thamani.

Rose alikaririwa: “Kwa kuwa anafahamiana na polisi, wakuu wa vituo vya polisi na viongozi wa dini, inakuwa rahisi kunisingizia mambo mengi machafu.

“Situmii madawa ya kulevya na sitatumia. Kama aliona ndiyo skendo itakayo-nimaliza, najua atashindwa, anayefanya hivyo ni mtu anayetaka kunimaliza, alitaka niwe mtu wake wa ngono na kumfanyia kazi, nikakataa.

“Sijawahi kujiingiza kwenya madawa ya kulevya na anavyozungumza, nasikitika kwa sababu anaiumiza familia yangu kisaikolojia.

“Mimi ni mama wa watoto watatu (Gift, Nicolas na Maximilian) na nina ndugu zangu, nasingiziwa mambo hayo kwa sababu sina mtetezi lakini ni vyema akajua mtetezi wangu ni Mungu.

“Lakini hii yote ni kwa kuwa nimekataa kulala naye. Napigwa hadi nazimia, wanaume walinizalisha na kunitelekeza, wameniumiza sana, afadhali ningefanyiwa mambo hayo na wanawake wenzangu, sasa natishiwa kifo, natamani hata kuhama nchi, hivi kweli akiona ninaishi nchini Kenya, ndiyo furaha yake?

“Lakini Mungu yupo na mbingu zitafunguka. Amekuwa akinizushia maneno makali, wakati mwingine nashinda porini, nikitetea maisha yangu.

“Kiukweli nimechoka jamani, acheni nipumzike, lakini namuachia Mungu, mbingu zitafunguka.”

MASWALI SAKATA LA ROSE

Baada ya hayo ndipo yakaibuka maswali juu ya sakata la Rose. Kama Ijumaa Wikienda tukawa tunajiuliza;

Je, ni nani huyo mwenye ubavu wa kutishia kutoa uhai wa binadamu mwenzake, achilia mbali Rose ambaye ni staa mkubwa kwenye jamii? Ni kosa gani alilolitenda Rose ambalo adhabu yake ni kifo?

Je, sababu ni hiyo pekee ya kumkataa kimapenzi au kuna sababu nyingine? Na je, mwanamke kumkataa mwanaume adhabu yake ni kifo? Nani kasema? Anamtishia kivipi? Kwa simu? Uso kwa uso? Wakiwa wapi?

Rose anasema amechoka kupelekwa kwenye vituo vya polisi ambako huko huwa anapigwa hadi anazimia, je, ni vituo gani vya polisi vilivyomfanyia hivyo ambavyo anaogopa kuvitaja kwa usalama wake?

Mara kadhaa Rose amekuwa akiripotiwa akidaiwa kutapeli watu kwa kuchukua fedha kisha kuingia mitini na kushindwa kufika kwenye matamasha. Kuhusu hilo Rose anahoji mbona hawajawahi kumfikisha mahakamani na aka-hukumiwa kama siyo kumchafua? Kama ni kweli huwa anatapeli, ina maana kesi zote wahusika humsamehe au hazifikishwi mahakamani?

HAPA KUNA TATIZO

Hapa kuna tatizo kubwa ambalo Rose anapaswa kuwa wazi ili kupata ufumbuzi na kumfanya aishi kama binadamu wengine na siyo kukimbilia porini ili kunusuru roho yake kama anavyosema. Ikumbukwe kuwa kila binadamu ana haki ya kuishi na siyo kuwindwa.

Saturday, 13 May 2017

May 13, 2017

HANSCANA ATUPIWA LAWAMA NA BABY J ADAIWA KUPOTEZEA MUDA

Baby J: Hanscana ni chanzo cha ukimya wangu

Msanii  wa muziki wa bongo fleva mwenye makazi yake Zanzibar, Baby J ameweka wazi kwamba amekuwa kimya kuachia kazi mpya hivi karibuni baada ya kuharibiwa video yake na 'director' Hanscana hivyo kwa sasa yupo jikoni kuandaa kazi nyingine nzuri.

Baby J amefunguka hayo kwenye Planet Bongo ya EATV na kusema kwamba alishindwa kuachia video aliyofanya na muongozaji huyo kwa sababu hakupenda jinsi ambavyo video ilivyokuwa imehaririwa kana kwamba ilifanywa kwa haraka haraka huku akiongeza kwamba haikuwa kama jinsi alivyotaka ndiyo sababu akaamua kuipiga chini.

"Ni kweli najua mashabiki zangu wamenimiss na wanataka kunisikia lakini siwezi kuwapa kitu ambacho siyo bora, hata wakiwa mbele za watu washindwe kusema kama wao ni mashabiki zangu kwa nini? kwa sababu naachia kazi mbovu? ndio maana nikaamua kukaa kimya. Video niliyofanya na Hanscana sikuipenda, hai ku-editiwa kama nilivyotaka sijui alikuwa na haraka au vipi. haikuwa mbaya lakini kwangu sikuipeda hivyo mashabiki zangu niwaombe wanisubiri siku siyo nyingi Mungu akijaalia nitaachia tuu kazi nzuri"- Baby J

Thursday, 11 May 2017

May 11, 2017

AFANDE SELE ATOA MFANO WA BOB MARLEY KUJIBU WAZIRI MWAKYEMBE

Afande Sele ‘amjibu’ Mwakyembe, atumia mfano wa Bob Marley

 Afande Sele

Jana, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aliwataka wasanii nchini kuacha kuimba nyimbo za kisiasa kama wanataka kufika mbali kimuziki na kupata mafanikio zaidi.

Sasa leo Afande Sele ametenga muda wake na kuandika ujumbe huu, “Kama Serekali ya Jamaica ingepiga marufuku wasanii wa nchini kwao wasiimbe nyimbo za siasa, basi siku kama leo tusingeshuhudia dunia ikiungana kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kaka yetu mkuu Robert Nesta Marley, ‘Baba Ziggy’, heshima na umaarufu wake havikujengwa kwa tungo za mapenzi, kujisifia na blah blah nyingine bali kwa siasa ambayo ndio maisha yenyewe nami kwa kumuenzi huyu nabii wangu siku kama leo natamani kuropoka kwa sauti kuu….,”


May 11, 2017

P DIDDY ANDIKA REKODI AONGOZA KWA UTAJIRI

P Diddy aongoza orodha ya matajiri wa Hip Hop

P Diddy hakamatiki kwa mkwanja wake. Forbes imemtaja rapper huyo kuwa na utajiri wa dola milioni 820 na kumfanya kuendelea kuongoza orodha ya mastaa watano wa Hip Hop wenye mkwanja mrefu zaidi duniani.

Rapper huyo ameendelea kuingiza fedha hizo kutokana na biashara zake nyingi ikiwemo Cîroc Vodka, Revolt TV, na ziara yake iliyoanza mwaka jana ya “Bad Boy Family Reunion Tour.” Naye Jay Z anashika nafasi ya pili katika orodha hiyo akiwa na kiasi cha dola milioni 810.

Utajiri huo wa Jay Z umetokana na kampuni zake za Tidal, Roc Nation, Roc Nation Sports na dili nyingine kupitia filamu anazofanya kupitia kampuni ya Weinstein Company. Katika kusherehekea hilo, Diddy kupitia mtandao wa Instagram, ameweka picha yake akiwa na Jay Z na kuandika, “We push each other… We inspire each other… #BlackExcellence.”

Wengine waliopo kwenye orodha hiyo ni Dr. Dre ($740) million, Birdman ($110) million na Drake ($90) million. Kwa mwaka jana orodha hiyo iliongozwa na Diddy akifuatiwa na Dr. Dre, Jay Z, Birdman na Drake.

May 11, 2017

FAHAMU HISTORIA YA BOB MARLEY

miaka 36 tangu kifo cha Bob Marley, fahamu historia yake

Bob Marley

Siku ya leo, ni miaka 36 tangu kufariki dunia kwa Mfalme wa muziki wa Reggae, Bob Marley toka nchini Jamaica.

Historia fupi

Robert Nesta “Bob” Marley alizaliwa February 6 mwaka 1945 na mama mweusi aliyeitwa Cedella Booker na baba wa Kizungu aliyeitwa Norvall Marley. Wakati akiwa mdogo, marafiki zake walimpa jina la utani kama ‘Tuff Gong’.

Alianza muziki miaka ya 1960 akiwa na kundi lake la kina Wailing Wailers, ambalo alilianzisha akiwa na marafiki wawili, Peter Tosh na Bunny Wailer. Mwaka wa 1962, Bob Marley na kina Wailing Wailers wakafanikiwa kurekodi nyimbo zao mbili za kwanza zilizoitwa “Judge Not” na “One Cup of Coffee”.

Bob alimuoa Bi. Rita Anderson mwaka 1966 na akajiunga na kundi akiwa kama mwitikiaji. Kwa pamoja wamefanikiwa kupata watoto watano. Mmoja kati ya hao ni Ziggy Marley, ambaye pia ni mwimbaji wa reggae maarufu.

Mwaka wa 1974, pamoja na kundi la Wailers kutengana, Bob Marley aliendelea kuita bendi yake jina la Bob Marley and the Wailers na kujiunga upya na wanachama wapya huku wakindelea kupiga muziki kama kawaida. Mwaka wa 1975, Bob Marley akatoa wimbo wake wa kwanza ambao ulimpa umaarufu duniani kote, ulijulikana kama “No Woman No Cry”.

Baadhi ya nyimbo zake kali ni pamoja na “I Shot the Sheriff”, “Could You Be Loved”, “Stir It Up”, “Jamming”, “Redemption Song”, “One Love” na, “Three Little Birds”.

Bob Marley alifariki katika hospitali ya Cedars of Lebanon Hospital huko mjini Miami, Florida, kwa tatizo la melanoma (kansa ya ngozi).

May 11, 2017

DIAMOND AMSHUKURU PROF JAY

KAULI ya Msanii Diamond Baada ya Profesa Jay Kusimama Bungeni na Kumtetea Kuhusu Kudaiwa Kodi ya Milioni 400 na TRA


Mwimbaji wa Bongofleva Diamond Platnumz ambaye juzi aliandikwa na gazeti la NIPASHE kwamba anadaiwa shilingi milioni 400 za kodi na TRA, amepost kipande cha video fupi ambacho Mbunge wa Mikumi Joseph Haule ‘Profesa Jay‘ amemuongelea bungeni. 

Kwenye video hiyo, Profesa Jay amesema;"Juzi Msanii Diamond alikua analalamika TRA wamempelekea kodi ya Milioni 400, unaweza kujiuliza anadaiwa milioni 400 kwa kiasi gani alichoingiza?‘ 

"Downloads zinazofanyika mnaweza kuona Wasanii sasa hivi wanabanwa, TRA wanatamani kuvuna kutoka kwa Wasanii kitu ambacho bado hawajakipandikiza, tumekua na ule msemo kama wa zamani kwamba shamba likiwa na bangi ni lako lakini likiwa na dhahabu ni la serikali… tunataka kuchuma kitu ambacho hatujakipanda, inabidi Serikali ianze kuwekeza na kuwajenga Wasanii kutoka shule za msingi mpaka Chuo kikuu" 

Baada ya maneno hayo ya Profesa Jay kwenye video, Diamond Platnumz aliichukua video hiyo na kuandika; 

 "Ndio Maana kwenye Jimbo lako sikuja kupiga kampeni bro…kwakuwa niliijua mapema thamani na umuhimu wa Uwepo wako kwenye hilo jengo"


Wednesday, 10 May 2017

May 10, 2017

RAMA DEE AKANA KUWA NA BIFU NA ADAMU JUMA AENDELEZA MSIMAMO WA KUMSIFU HASCANA

Rama Dee: Sina beef ila Hanscana ni Zaidi ya Adam Juma

Msanii wa muziki, Rama Dee amedai kauli yake “Hanscana ni muongozaji mkali wa video kuliko Adam Juma” siyo kama alimkosea heshima muongozajii huyo mkongwe wa video za muziki.

Muimbaji huyo amedai alitaka kumwambia ukweli muongozaji huyo ili kama anaweza kubadilka abadilike.

“Sikujenga beef na Adam Juma, nilisema kitu ambacho nakiona,” Rama Dee alimjibu mmoja  kati ya mashabiki wake ndani ya Kikaangoni EATV.  “Kwanini nimwambie kwa siri, hakuna cha siri, mtu akizungua unamwambia moja kwa moja,”

Aliongeza, “Mimi sina beef na mtu, mimi nafikiri mtu akiambiwa ukweli anatakiwa kutulia siyo na wewe unanza kutafuta namna ya kujitetea,”

Muimbaji huyo amedai hataki kuzungumzia zaidi mahusiano yake na Adam Juma kwa kuwa tayari ameshamalizana naye.

Hata hivyo kauli hiyo ya ‘Hanscana ni mkali kuliko Adam Juma’, ilipingwa na wadau mbalimbali katika mitandao ya kijamii wakidai muimbaji huyo amemkosea heshima Adam Juma.

May 10, 2017

PROF JAY AMUOKOA STEVE NYERERE

Steve Nyerere: Prof. Jay ameanza kunielewa

Mchekeshaji na muigizaji wa bongo 'movie' Steve Nyerere amefunguka mengine mapya kwa kudai hana haja tena ya kuendelea kutukanana na watu wasiojielewa kwa kuwa ameshajitokeza mkombozi wake mwenye akili na kutambua kilio chake kinamaana gani.

Steve amesema hayo baada ya kile kinachoaminika kuwa Mbunge wa Mikumi, Mhe. Joseph Haule kusimama mbele ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwatetea wasanii kwa ujumla kwa kuitaka serikali kuwekeza fedha za kutosha katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ili wizara hiyo iweze kuwekeza katika sanaa na kuacha kuwatumia wasanii katika chaguzi na kampeni mbalimbali kisha kuwaacha kama makarai ya kujengea maghorofa na vitu vingine lakini nyumba ikakamilika yanawekwa uvunguni hayatakiwi wala kuthaminiwa hata kuonekana kwa wageni wa aina yoyote wale.

"Mwenye akili anaanza kuelewa nalilia nini kwenye sanaa yetu..Sina haja ya kutukanana ni wajinga wanao tukana. Ukweli unadumu kuliko kitu chochote, ukweli huzaa amani..Asante Mhe. Haule kwa kuongea ukweli". Alisema Steve kupitia ukurasa wake wa instagram

May 10, 2017

NANDY APATA USUMBUFU KUTOKA KWA WANAUME

Nandy: Wanaume wananisumbua sana

MWANADADA anayefanya poa na ngoma yake ya One Day, Faustina Charles ‘Nandy’ amekiri kuwa anapata usumbufu mkubwa kutoka kwa wanaume wakware ambao wanahitaji penzi lake, lakini bila mafanikio.

Akipiga stori na Za Motomoto News, Nandy alifunguka kuwa amekuwa akikumbana na vishawishi mbalimbali kwa ahadi kedekede ili tu waweze kutimiza azma yao lakini anajitahidi kupambana na hali hiyo sababu ameshajifunza kupitia kwa wenzake.

“Usumbufu ni mkubwa mno kwa kweli, lakini siwezi kuwataja majina hata hao vigogo wanaonisumbua, mimi ni msichana ninayejielewa na wanaume wengi wamekuwa wakihaha kutaka kuonja penzi langu, wanagonga mwamba,” alisema.

May 10, 2017

DIAMOND AACHWA KWENYE ORODHA MPYA YA WASANII AFRIKA WANAOPIGA MKWANJA HII HAPA ORODHA KAMILI

WAFAHAMU Wasanii Wanaoingiza Pesa Nyingi Afrika Kwa Mujibu wa Forbes

Jarida la Forbes Africa la mwezi May 2017 limeandaa list ya wasanii 10 wanaoingiza pesa nyingi zaidi Africa. 

List hiyo ambayo inaongozwa na msanii wa Nigeria, Akon na nafasi ya pili ikichukuliwa na producer na msanii wa Afrika Kusini, Black Coffee imendaliwa kwa vigezo vya thamani ya endorsement wanazozipata, umaarufu, viwango vya show zao wanazofanya, mauzo, tuzo, watazamaji wao kwenye chaneli za YouTube, kutokea kwenye magazeti, kuwa na ushawishi mkubwa kuliko wengine, uwekezaji na uwepo wao katika mitandao ya kijamii. 

1.AKON 

Akon anaingia kwenye list hii kutokana na mauzo ya albumu zake akribani milioni 35 zilizouzwa kila pande ya dunia, kingine kikubwa ni kwamba Akon ameshajinyakulia grammy tano huku akiwa ameingiza ngoma 45 katika chati za ya Billboard hot 100. 

2. BLACK COFFEE, AFRIKA KUSINI 

Maarufu sana kutokana na tuzo ambazo amewahi kujishindia kama BET, wengi wanamfahamu kwa jina kamili la Nkosinathi Maphumulo , kubwa zaidi Black Coffee, ameingia kwenye albumu mpya ya Drake ‘More Life’ ambayo inafanya vizuri sokoni. 

3. HUGH MASEKELA 

Alizaliwa Witbank, Mashariki mwa Johannesburg, Hugh Masekela ashafanya takriban albumu 43 ambazo zote hizo aliwahi kuperforme na wasanii wakubwa kama Marvin Gaye, Stive Wonder, Miriam Makeba na wengine kibao. 

4. DON JAZZY, NIGERIA 

Ni msanii pia ni producer kutoka nchini Nigeria ambaye amejibebea umaarufu kutokana na mafanikio makubwa katika game ya muziki Afrika mpaka Marekani ambapo alifanikiwa kuja na label yake ya  Mavins ambayo nayo imebeba vichwa vingi vikubwa vinavyofanya vizuri Afrika, Do Jazzy alianza tasnia ya muziki tangu yuko mdogo kanisani mpaka kufikia hatua hii aliyokuwa nayo sasa. Pia msanii kutoka kwenye label yake ya Mavins, Tiwa Savage alisaini katika label ya Jay Z, Roc Nation. 

5. TINASHE, ZIMBABWEAN-AMERICAN 

Maarufu na ngoma kama ya “2 On aliyomshirikisha School Boy” pamoja na “How long” ya Davido, Tinashe ni mchanganyiko Mzimbwabwe pamoja na America, vilevile ni mwandishi mzuri wa nyimbo, muimbaji, muigizaji pamoja na dancer. Alishashinda tuzo kibao kupitia wimbo wake wa “2 On”. Tinashe aliingia kwenye listi ya kuwa mwanamke wa kwanza kutokea katika jarida la Play Boy bila kukaa utupu. 

6. JIDENNA, NIGERIAN-AMERICAN 

Mzee wa Classic, anajulikana kama Jidenna Theodore Mobisson, mbali na kuwa maarufu katika tasnia ya muziki, Jiddena angekuwa ni moja ya masound Engineer, amejizolea umaarufu na ngoma yake ya Classic Man, Yoga, Long Live Chief na zingine kibao. 

7. WIZKID, NIGERIA 

Moja ya wasanii wa Afrika wanaofanya vizuri duniani na kugusa kila mioyo ya wapenda muziki, ameingia kwenye tuzo nyingi kubwa duniani kupitia wimbo wa “One Dance” alioshirikishwa na Drake pamoja na “Come Closer” anayotamba nayo kwa sasa. 

8. DAVIDO, NIGERIA 

Ni mmoja kati ya wasanii ambao wamepigana sana kufikia hatua ambayo yupo nayo sasa akiwa na ngoma nyingi kali na kutengeneza njia kibao kwa muziki wa Afrika kuchomoza zaidi. Alishapiga kolabo na msanii kutoka Bongo, Diamond platnumz. 

9. SARKODIE, GHANA 

Alianza kama underground rapper katika tasnia ya muziki wa kiafrika mpaka kufikia hatua ya mghana wa kwanza kushinda tuzo ya BET, maarufu na ngoma “No kissing Baby”, “Pain Killer”. 

10. OLIVER MTUKUDZI, ZIMBABWE 

Albumu 65 zikiwa kwenye tasnia yake ya muziki, katika miaka yake 41 ya muziki, nyimbo zake zimekuwa zikichezwa duniani kote, maarufu zaidi masikioni mwa mashabiki na kibao cha “Neria”

Tuesday, 9 May 2017

May 09, 2017

MASOGANGE AJIPELEKA MWENYEWE KISUTU KUJISALIMISHA

Masogange ajisalimisha Kisutu

Msanii, Agnes Gerald maarufu kama Masogange 

Dar es Salaam.  Msanii, Agnes Gerald maarufu kama Masogange (28) amejisalimisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kabla ya Masogange kujisalimisha mahakama ilitoa hati ya kumkamata baada ya kushindwa kuhudhuria mara mbili kwenye kesi hiyo inayomkabili.

Hatua hiyo ya kutaka kukamatwa kwa Masogange  ilikuja baada ya upande wa mashtaka  kuomba mahakama  kutoa hati ya kumkamata kutokana na mshtakiwa huyo pamoja na wadhamini wake kutofika mahakamani, licha ya kupewa onyo.

Hivyo Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri alikubali maombi hayo na kutoa hati ya kumkamata Masogange.

Hata hivyo, Masogange leo (Jumanne) amefika mahakamani hapo mapema.

Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam.

May 09, 2017

BASAGA ATANGAZA UJIOMPYA AWAONYA WALIOSEMA AMEPOTEA,BAADA YA BADILISHA POZI SASA ANATAFUTA BAUNSA

Msanii anaetamba na wimbo Wa badilisha pozi aliofanya na becka amemtoa hofu nay Wa mitego baada ya kuwepo na tetesi kwa muda mrefu kuwa amekuwa akimnyima amani rais Wa manzese kwa kuwa amemtake over na hata hivyo amekuwa akiandika mistari ambayo inaonekana kumlenga moja kwa moja nay Wa mitego

Basaga amesema hayo kwenye interview wakati akijibu maswali matano ya mwandishi wetu kama ifuatavyo;

1:kwanini umekuwa kimya kwa muda'

"Ni kweli nimekuwa kimya kwa muda hii ni baada ya kutoa Wimbo na becka Wa badilisha pozi ambayo ulifanya vizuri hivyo ikanibidi nitulize akili ilikuandaa Wimbo mngine ambao utakuwa mkubwa na utanifikisha mbali zaidi ambapo hata hivyo nimefanya ngoma kama 4 ambazo mmoja utatoka hivi karibuni mambo yakikaa sawa kwani kwa sasa kila kitu kiko tayari kuanzia audio hadi video lakini siwezi sema nimefanya na nani au hizo zingine nimefanya na nani lakini zote nimefanya na wasanii wakubwa nawaomba mashabiki zangu awajiandae kunipokea upya".

2:vipi kuhusiana na bifu lako na nay Wa mitego.!!?

" nay sina tatizo nae kabisa sema tu watu wengi wanasema mimi na bifu nae kwa kuwa nimemchana kwenye nyimbo zangu kadhaa lakini hii ni vina tu  so namuomba awe na amani na kingine watu husema na bifu nae kwa kuwa tunafanya Muziki unaofanana so nay mdogo wangu kuwa na amani sina tatizo na wewe.

3:NI MSANII GANI ANAKUPA CHANGAMOTO KIBONGO BONGO..!?

"Naweza kusema kwa namna moja ama nyingine hakuna Msanii ambae ananipa changamoto kwa sababu Muziki sahivi ni ushindani hivyo kila mmoja hufanya vizuri pale anapopata nafasi na Pamoja na kuwa ushindani umekuwa mkubwa lakini naamini kwa huu Wimbo wangu Mpya utakao toka hivi karibuni 'NATAFUTA BAUNSA' utakuwa ni kiboko yao nakuja kutake over na najua utageuza upepo na utakuwa changamoto kubwa kwa wasanii ambao wanafanya vizuri sahivi."

4:CHANGAMOTO GANI AMBAZO UMEKUWA UKIKUMBANA NAZO..!??

"changamoto zipo nyingi zipo ambazo mtu mwenyewe unaweza kuzimudu na ambazo huwezi mfano usumbufu kutoka kwa watoto Wa kike na nyingine ambazo huwezi kuzitatua wewe kama wewe kama unavyojua wasanii Wa bongo hatuna ushirikiano na ndiyo maana namshukuru mungu kwanza na mashabiki wangu kwa ujumla kwani naamini bila wao siwezi na Mimi kufanya lolote so big up kwa mashabiki wangu kokote wrote walipo."

5:NINI WASANII GANI AMBAO TAYARI ULISHAFANYA NAO KAZI NA NI WAPI AMBAO UNAFIKIRIA KUFANYA NAO KAZI...!!!?

"Ambao nilishafanya Kazi ni wengi mno mfano becka ambayo tayari ilishatoka,Ben Paul,20percent,na wengine wengi ambaonitatoa Kazi hizo muda ukifika,na wasanii ambao nafikiria kufanya NAO Kazi ni johmakini,jmoe,fidq,youngkiller pamoja na darasa ambao ndani ya Mwana huu naamini hizo Kazi zitakuwa tayari."

5:NINI AMBACHO UNGEPENDA KUWAMBIA MASHABIKI ZAKO.

" cha kwanza mimi nawashukuru kwa support yao kwangu ambayo wamekuwa wakiionyesha kwa Kazi zangu niwaombe waipikee na hii Kazi Mpya ambayo sitasema nimemshirikisha nani lakini hivyo nawaachia kama surprise pili niwaombe wanipigie kura ili niweze kushinda tuzo za nyumbani nako tokea njombe kama Msanii bora Wa hip hop na Wimbo bora Wa mwaka unaweza kunipigia kura kama ifuatavyo:

Naomba Kura yako NYOTA AWARDS NJOMBE 2016/17..

MWANAMUZIKI BORA WA KIUME

Andika (sms) B30  kwenda 0719 009443 (Mara 3 kwa siku)

WIMBO BORA WA HIP HOP (Badilisha Pozi)

andika E27 kwenda 0719 009443 (Mara 

3 kwa siku

Kwahiyo jumla unakua umenipigia kura 6


May 09, 2017

RAY C AKATAA KUTOKA MBUNGE ASEMA HAJAWAHI NA HAITATOKEA

RAY C Afungukia A -Z Kuhusu Kutoka na Mbunge..111


Sexy lady mkongwe wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amefunguka kuwa hajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi mbunge yoyote nchini kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakieneza ubuyu.

Ray C aliliambia Wikienda kuwa, mbali na kufahamiana na wabunge mbalimbali nchini, lakini hata siku moja hajawahi kujiingiza kwenye uhusiano na mheshimiwa yeyote kama inavyovumishwa.

“Kwanza kwa sasa mambo ya mapenzi nimeyaweka kando, niko bize na muziki wangu, akili na hisia zangu zote nimezielekezea kwenye kazi. Muziki ndiyo kila kitu kwangu,” alisema Ray C.

May 09, 2017

DOGO JANJA AMTOA KIKI KWA HARMORAPA

DOGO Janja Amwagia Sifa Harmorapa..!!!


Msanii wa bongo fleva mwenye 'hit song' ya 'Kidebe' Dogo Janja amefunguka kwa kusema anamkubali rapa chipukizi Harmorapa kwa kuonesha uthubutu wake katika muziki licha ya watu kumkatisha tamaa kwa kumwambia hajui kitu lakini hakurudi nyuma.

Dogo Janja amebainisha hayo kupitia kipindi cha eNewz kwa kudai kilichomfanya amkubali msanii huyo ni kutokana na kumuona ana moyo wa ujasiri wa kupambana muda wote katika kufikia mafanikio yake ya kimuziki bila ya kujali watu wanasema kitu juu yake.

"Harmorapa ni mtu ambaye nimetokea kumkubali mimi kama mimi ....Ni mtu ambaye amejaribu kuonesha uthubutu..Stape ambayo ameenda ndiyo imenifanya mimi nimkubali zaidi, alianza wimbo wa kwanza watu wakamtisha tamaa, vunja moyo lakini hakuvunjika moyo. 'Dude' la pili akajaribu halafu likawa kali mimi nikasema huyu anahitaji vitu vichache tu vya kuongezeka kwa kuwa anaonekana na moyo wa uthubutu na anapenda kujifunza zaidi". Alisema Dogo Janja

Pamoja na hayo Dogo Janja amesema siyo kweli kwamba Harmorapa anabebwa na 'kiki' kuliko muziki wake ila watu wenyewe ndiyo wanamfanya kituko ili azidi kuonekana 'kiki.'