DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Showing posts with label kitaifa. Show all posts
Showing posts with label kitaifa. Show all posts

Saturday, 23 September 2023

September 23, 2023

AJALI YA ROLI YAUA WATU 9

 


 

WATU tisa wamefariki dunia mkoani Mbeya baada ya  dereva wa lori lenye namba za usajili BCE 9384/ABX8675 kushindwa kulimudu gari lake kwenye mtelemko mkali  wa Mbalizi na kwenda kuigonga gari ya abiria na yenye namba za usajili T.636 DQY aina ya Mitsubishi Rosa .

 Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mbeya,Benjamin Kuzaga amesema kuwa tukio hilo limetokea Septemba 22 mwaka huu majira ya saa 11.40 jioni  katika eneo la mteremko wa Iwambi wilaya ya Mbeya Vijijini  mkoa wa Mbeya .

Kamanda Kuzaga amesema kuwa gari  yenye namba za usajili BCE 9384/ABX 8675 aina ya Howo mali ya kampuni ya Horn Afric Motors ltd ya nchini Zambia ikitokea Mbeya kuelekea Tunduma likiendeshwa na dereva Mohamed Abilah (47) Mkazi wa Zambia .

Aidha Kuzaga ameeleza kuwa gari hilo iliigonga kwa nyuma Gari yenye namba za usajili T.636 DQY aina ya Mitsubishi Rosa ikitokea Mbeya mjini kuelekea mbalizi ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva ,Elly Mwakalindile (41)mkazi wa Iyunga na kusababisha vifo vya watu Tisa ambapo kati yao wanaume watano na wanawake wanne.

Aidha  kamanda Kuzaga amesema kuwa katika ajali hiyo watu 23 walijeruhiwa kati  ambapo kati yao wanaume 13 na wanawake 10 ni majeruhi  na wanaendelea kutibiwa katika  Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo Mji Mdogo wa Mbalizi na wengine wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

 Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali Teule ya Ifisi Mbalizi ambapo miili ya marehemu 07 imetambuliwa huku miili ya watu 02 ikiwa bado  haijatambuliwa.

Chanzo cha ajali hii ni Dereva wa lori kushindwa kulimudu gari lake kwenye mteremko mkali na kwenda kuigonga kwa nyuma Gari ya abiria na kuwa Dereva wa lori amekamatwa na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa madereva ambao wanapita katika Mkoa wa Mbeya kwenye milima na miteremko mikali kuhakikisha wanakagua magari yao kabla ya kuanza safari na wamiliki wa magari wasiruhusu magari yao kuendeshwa na madereva hao ili kuepusha ajali.

Saturday, 5 November 2022

November 05, 2022

SERIKALI HAITASITA KUWACHUKULIA SHERIA WAKWEPA KODI PANGO LA ARDHI-DKT KIJAZI.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi amewataka wadaiwa sugu wa kodi ya Pango la Ardhi kulipa kodi hiyo kabla ya Serikali kuanza kuchukua hatua za kisheria kwani wale watakao endelea kukaidi agizo hilo wako hatarini kupoteza milki ya ardhi zao.

Dkt. Kijazi amesema suala la kulipa kodi ya ardhi ni la kisheria hivyo kuwataka wananchi wote kuzingatia matakwa ya kisheria kwa kulipa kodi hiyo na kuwakumbusha kuwa Serikali imetoa msamaha wa riba kwa walipa kodi sugu na mwisho wa msamaha huo ni Disemba mwaka huu.

Dkt. Kijazi amesema hayo leo tarehe 4, Novemba 2022 Jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa  kikao kazi kati ya Benki ya CRDB na wasimamizi wa kodi wa Wizara ya Ardhi kutoka mikoa yote nchini kujadili namna bora ya ushirishaji wa CRDB katika makusanyo ya kodi ya pango la Ardhi.

Katibu Mkuu Dkt. Kijazi amesema madeni ya kodi ya Ardhi ni takribani Bil.70 na kusisitiza kuwa hata kama msamaha wa riba ya kodi ya ardhi kukoma Disemba mwaka huu bado wataendelea kudai malimbikizo ya kodi ya ardhi kwa wale watakaoendelea na kumilki ardhi bila kulipa kodi.

Aidha Kiongozi huyo wa Wizara ya Ardhi amesisitiza Taasisi za Umma kuona ya haja ya kulipa kodi ya pango la ardhi kwani kwa sasa malimbikizo hayo yanazihusisha pia taasisi za umma na binafsi na uzoefu unaonesha kiwango kinachokusanywa kidogo kulinganisha na uhalisia kwa idadi ya walipa kodi.

Dkt. Kijazi pamoja na mambo mengine amesisitiza suala la elimu kwa umma kwa wananchi ili kuwajengea uelewa wa masuala ya ulipaji kodi ili waweze kushiriki kikamilifu na kuona umuhimu wa kulipa kodi ya ardhi.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Gerald Kamugisha amesema kimsingi Benki yake iko tayari wakati wowote kufanya kazi na Serikali katika suala la ukusanyaji kodi na tayari kuna matawi kama 50 yanayofanya kazi na Wizara ya Ardhi katika kuhakikisha miamala ya ukusanyaji kodi inafanyika kupitia matawi hayo yaliyoko Dar es Salaam na Pwani.

Kamugisha ameongeza kuwa CRDB imeendelea kukua mwaka hadi mwaka na imeongweza wigo wa huduma zake hadi nje ya Nchi kwani tayari ina matawi Burundi na inakusudia kufungua matawi yake Nchini Kongo.

Kamishna wa Ardhi Nchini Bw. Mathew Nhonge amesema Wizara ya Ardhi Pamoja na kuwa mtandao mkubwa ukusanyaji kodi ya ardhi mpaka ngazi ya Halmashauri Wizara imeona ni vyema kutumia taasisi na mitandao ya simu ili kupunguza gharama kwa walipa kodi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo katika ofisi za serikali.

Kamishna Nhonge ameongeza kuwa Wizara ya ardhi pia kwa kufanya hivyo inapanua wigo wa wa ukusanyaji kodi ndio maana inaenda mbali zaidi kuboresha mtandao wa ukusanyaji kodi kwa kutumia taasisi za fedha kama Benki na mawakala wa mitandao ya simu Pamoja na Benki.   

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika juhudi zake za kuongeza mapato ya Serikali kupitia kodi ya Ardhi inajipanga kushirikisha taasisi za kifedha ikiwemo CRDB na baadhi ya makampuni ya simu ili kurahisisha wigo wa ukusanyaji kodi ya pango la Ardhi nchini.



November 05, 2022

MAANDALIZI KUELEKEA TAMASHA LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO

 


 

Makamu wa raia wa Jamhuri ya muunganowa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la 41 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) lililopangwa kufanyika kwa siku tatu mfululizo Novemba 10-12,2022 kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.

 

Katika kikao cha kamati ya maandalizi kilichofanyika mjini Bagamoyo kikiongozwa na katibu mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi kufanya maandalizi ya mwishoni ikiwemo kupanga ratiba za uendeshaji wa tamasha lenyewe kwa kipindi chote cha siku tatu.

 

Katika kikao hicho katibu mkuu amesema tamasha la msimu huu ambalo litakua la 41 tangu kuanzishwa kwake litakua na washiriki wengi zaidi ikiwemo vikundi mbalimbali vya Sanaa kutoa ndani na mataifa mengine, nakuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wizara.

 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdalla amesema hali ya usalama kwa wilaya hiyo ni swari na kwamba ulinzi utaimarishwa kipindi chote cha tamasha, akiwataka wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani kujitokeza na kuwa tayari kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

 

“Mbali ya kuwa wageni watakuja kwa ajili ya Tamasha lakini pia Bagamoyo ni eneo lenye fursa mbalimbali hasa za kiutalii hivyo ni fursa kwao wageni kujionea pia wenyeji tujiandae kuwapokea”. Alisema DC Zainab.

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa wasanii wanaofanya mziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Mike Francis Mwakatundu amesema tamasha la kimataifa la Sanaa na utamaduni Bagamoyo limesaidia kutambulisha idadi kubwa ya wasanii kimataifa pia kufahamiana na wasanii wa mataifa mengine.

 

“Kwa sisi wasanii limekua linatusaidia sana kututambulisha kimataifa na kutuwezesha kukutana na wasanii wengine, mfano kwenye tamasha la msimu huu tayari tuna wasanii kutoka Burundi,Canada,India, Ufarasa na maeneo mengine tunavyo kutana hapa tunabadilishana uzoefu kwa kila msanii kwa eneo lake”.Alisema Mwakatundu


Tuesday, 1 November 2022

November 01, 2022

WACHAPWA VIBOKO 48 NA MIAKA 120 JELA

 


 Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka jela miaka 120 na kuchapwa viboko 48 kila mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa makosa manne ya unyanganyi wa kutumia silaha.

Hata hivyo, ingawa kila mshatakiwa amehukumiwa miaka 30 jela na viboko 12 kwa kila kosa, kwa makosa manne waliyoshtakiwa nayo, kila mshatakiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 na viboko 12, kwa makosa yote kwa kuwa vifungo hivyo vitatumikiwa vyote kwa pamoja.

Hukumu ya kesi hiyo namba 26 ya mwaka 2021 imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Samuel Maweda baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi na vielelezo vilivyotolewa na upande wa Jamhuri.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuiba mali mbalimbali zikiwamo fedha taslimu, simu, kompyuta mpakato ‘laptop’ pamoja na kujeruhi kwa kutumia panga.

Awali wakili wa Serikali Winfrida Ernest aliieleza mahakama kuwa washtakiwa hao, Emanuel Matulanya (20) Musa Soro (20) na Philipo Lucas (18) wanashtakiwa kwa makosa manne ya unyanganyi wa kutumia silaha kinyume na kifungu namba 287 cha sheria ya adhabu.

Walipotakiwa kujitetea washtakiwa hao waliiomba mahakama kuwapunguzia adhabu kwa kuwa ni kosa la kwanza huku mshatiwa wa pili Musa Soro akiomba apunguziwe adhabau kwa kuwa ana mke na mtoto mmoja wanaomtegemea.

Tuesday, 4 October 2022

October 04, 2022

WALAKA WA MWIJAKU KWA MASANJA

Vijana oeni wanawake wasio na tamaa za kijinga kushiriki mapenzi na kila mtu kizembe - Mwijaku.
Muhtasari
• Mwijaku alimpa pole mchungaji Masanja Mkandamizaji kwa skendo inayomhusisha mkewe kimapenzi na katibu wa kanisa aliyejiua.
Mwijaku alimpa pole mchungaji Masanja Mkandamizaji kwa skendo inayomhusisha mkewe kimapenzi na katibu wa kanisa aliyejiua.
Mwijaku ampa pole Masanja MkandamizajiBaada ya sakata la kujitoa uhai kwa katibu katika kanisa la Feel Free lake mchekeshaji ambaye sasa ni mhubiri Masanja Mkandamizaji, sasa watu wengi wamezamia skendo hiyo na kutolea maoni mseto.
kumbukwe zogo zima la katibu huyo kujitoa uhai liligeuka changamano hata zaidi baada yake kuacha barua ambayo alimuandikia mkewe mchungaji Masanja Mkandamizaji na kudhihirisha kwamba anampenda sana na yeye alikuwa analijua hilo na ndio maana wivu wa mapenzi umemfanya kujisafirisha jongomeo.
Baada ya tarifa hizo za mkewe baba mchungaji kutoka kimapenzi na mama kanisa, Masanja alizungumzia suala hilo na kuahidi kuzidi kumpenda mkewe hadi pumzi zake za mwisho licha ya skendo ya kimapenzi na marehemu katibu wa kanisa lao.
Mtangazaji Mwijaku pia hajaachwa nyuma kwani amelizamia na kumwambia Mchungaji pole za dhati kwa matukio yanayozunguka kanisa lake pamoja pia na mke wake kutoka kimapenzi na katibu wa kanisa.
Mwijaku ametumia fursa hiyo kutoa onyo kali kwa watu watakaojaribu kufanya mzaha wa kumtongoza mkewe kuwa atawapiga bomu vibaya sana.
Pia aliwashauri vijana kuoa wanawake wasiokuwa na tamaa za kijinga kama mkewe katika kile kilionekana anamkashfu mke wa Masanja kwa kuhusishwa kimapenzi na katibu wa kanisa lake

Monday, 3 October 2022

October 03, 2022

KATIBU WA KANISA AJIUA KISA MZOZO WA MAPENZI NA MKE WA MCHUNGAJI

Katibu wa kanisa alijiua na kuacha barua iliyokuwa inazungumziwa uwepo wa kimapenzi na mke wa mchungaji Masanja Mkandamizaji.

Muhtasari
Katibu wa kanisa la Masanja alijiua kutokana na kile kilitajwa kuwa ni mzozo wa kimapenzi baina yake na mke wa Mchungaji huyo.
Masanja alimwandikia mke wake ujumbe kuwa atasimama na yeye mpaka pumzi yake ya mwisho na hatomuacha hata baada ya sakata hilo kutokea.
Katibu wa kanisa la Masanja alijiua kutokana na kile kilitajwa kuwa ni mzozo wa kimapenzi baina yake na mke wa Mchungaji huyo.
Masanja alimwandikia mke wake ujumbe kuwa atasimama na yeye mpaka pumzi yake ya mwisho na hatomuacha hata baada ya sakata hilo kutokea.


Wikendi iliyopita kulikuwepo na uvumi wa sakata la kujitoa uhai kwa katibu katika kanisa la Feel Free la aliyekuwa mchekeshaji na mchungaji Masanja Mkandamizaji kutoka Tanzania.
Taarifa zilisema kuwa katibu huyo alijitoa uhai kutokana na kujulikana kwa skendo ya kutoka kimapenzi na mama wa kanisa ambaye ni mkewe mchungaji Masanja Mkandamizaji.
Ujumbemrefu uliovujishwa kutoka kwa marehemu aliuachana kabla ya kifo chake unaelezea kwa mapana sababu za kujitoa uhai katika sakata ambalo sasa limejumuisha mambo mengi likiwemo suala la kuchepuka na mama kanisa. Barua hiyo alionekana kumwandikia mwanamke mmoja ambaye bado haijabainika kama kweli ni mkewe Masanja.
Asante Kwa kunipenda Kipindi chote hakika umenipa Upendo ambao umeacha alama moyoni mwangu ambao kila nikijaribu kuifuta nimeshindwa sioni upendo wako wa Mwanzo hivyo nimebaki Kuumia MOYONI kwa kukosa,” sehemu ya barua hiyo ilisoma.Mchekeshaji Mkandamizaji ambaye kila Jumapili huwa anahubiri katika kituo cha Wasafi, hakuhudhuria kipindi hicho kutokana na suala hilo tata ambalo linazidi kuchemka haswa kwenye mitandao ya kijamii.Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Masanja Mkandamizaji alipakia video yenye picha ya pamoja na mkewe wakionekana katika mkao wa kuomba na kusujudu vile na kuachia ujumbe changamano ambao wengi waliuambatanisha na sakata hilo la kujitoa uhai kwa katibu katika kanisa lake. Baada ya watu zaidi ya laki mbili ufurika pale na kuachia maoni mbali mbali, mchungaji Mkandamizaji aliifuta post ile lakini kuna baadhi ya wale waliobahatika kuinakili na ilikuwa na maneno.
"Kila kazi ina gharama yale, acha tulipe gharama ya tulichoitiwa . nakupenda mpaka pumzi yangu ya mwisho mke wangu. Hili nalo litapita Tuombeeni nasi tunaomba, mtetezi wetu yu hai". .Mkandamizaji aliandika.Katika maneno haya, wengi walionekana kukisia kuwa mchungaji huyo alikuwa anatia roho ya kiume kusimama na mke wake wakati wa kipindi hiki kigumu ambacho kimezua timbwiri la kumsaliti mume wake na mfanyikazi wa kanisa.
October 03, 2022

UNAFUU WA VIWANGO VIPYA VYA TOZO ZA MIAMALA NA BENKI.


Serikali imetangaza viwango vipya vya tozo vya miamala simu na benki zikiwa zimepita siku chache tangu iahidi kuvipunguza kutokana na malalamiko ya wananchi.
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, kupitia gazeti la Serikali la Septemba 30 ambalo Mwananchi imeliona imesema mabadiliko hayo yamefanywa kupitia Sheria ya Mifumo ya Malipo (Sura ya 437) chini ya kifungu cha 46A(2).
Kwa mujibu wa jedwali la marekebisho hayo, kuhamisha Sh100 hadi Sh2,999 ni Sh10, kuhamisha Sh3,000 hadi Sh3,999 ni Sh14, Sh4,000 hadi 4,999 ni Sh27, kutuma Sh5,000 hadi 6,999 ni Sh54, kutuma Sh7,000 hadi Sh9,999 ni Sh56.
Viwango vingine ni kutuma Sh10,000 hadi 14,999 ni 102, kutuma Sh15,000 hadi 19,999 ni Sh195, kutuma Sh20,000 hadi 29,999 ni Sh306, kutuma Sh30,000 hadi 39,999 ni Sh351, kutuma Sh40,000 hadi 49,999 ni Sh419, kutuma Sh50,000 hadi Sh99,999 ni Sh573, kutuma Sh100,000 hadi 199,999 ni Sh707, kutuma Sh200,000 hadi 299,999 ni Sh821.
Nyingine ni kutuma Sh300,000 hadi 399,999 ni Sh838, kutuma Sh400,000 hadi 499,999 ni Sh982, kutuma Sh500,000 hadi 599,999 ni Sh1,245, kutuma Sh600,000 hadi 699,999 ni Sh1,532.
Nyingine ni kutoka Sh700,000 hadi 799,999 ni Sh1,700, kutuma Sh800,000 hadi 899,999 ni 1,500, kutuma Sh900,000 hadi 1,000,000 ni 1,776, kutuma Sh1,000,001 hadi 3,000,000 ni Sh1,875, kutuma Sh3,000,001 na kuendelea 2,000

Friday, 19 November 2021

November 19, 2021

MHE. SAMIA AWEKA HISTORIA KIGOMA, ASIKILIZA KERO ZA WANANCHI KWA BALOZI WA SHINA


Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mhe. Samia Suluhu Hassan amezungumza na Mwenyekiti wa shina (Balozi) Namba moja, katika Kata ya Kumunyika, Wilaya ya Kasulu, mkoani Kigoma Ndg. Juma Ahmed Rugina na kumpongeza kwa kuongoza shina hilo kwa miaka ishirini.

Balozi Mzee Rugina amezungumza na Mwenyekiti na Rais Mhe. Samia leo tarehe 19 Novemba, 2021 kupitia simu ya mkononi ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndg. Daniel Chongolo ambaye ametembelea shina hilo na kukagua uhai na uimara wa chama kwenye ngazi za mashina na kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo hayo.

Katika mazungumzo hayo, Balozi Rugina amempongeza Mwenyekiti na Rais Mhe. Samia kwa kuendelea kufungua fursa za maendeleo kwa wananchi wa Kasulu na mkoa wa Kigoma kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara, afya na elimu ambapo amesema miaka ya nyuma wakati kama huu mifugo yao na vitu vingine vilikuwa vinauzwa kwa ajili ya michango ya kuchangia ujenzi wa madarasa, tofauti na mwaka huu ambapo fedha zote Mhe. Rais Samia amezitoa.

Aidha katika hatua nyingine, Balozi Rugina amemuomba Mwenyekiti na Rais Mhe. Samia kusaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa karavati katika maeneo hayo, pamoja na  kadi za uanachama kwa wakereketwa wote wa CCM wa shina hilo pamoja na mashina mengine wilayani Kasulu na Mkoa wa Kigoma ambapo katika shina hilo kuna wanachama 64 na wakereketwa wengi wasio na kadi.

Kufuatia maombi hayo ya Balozi Rugina, Mwenyekiti Mhe. Samia amemuagiza Katibu Mkuu kushughulikia changamoto hiyo huku changamoto ya karavati akimuelekeza Mkuu wa Wilaya Kanali Isack Antony Mwakisu kushughulikia kwa haraka.

Wakati huo huo, Rais Samia amemuomba balozi huyo kuwahamasisha wanachama wake na wananchi kwa ujumla, kushiriki kwenye mambo ya maendeleo kikamilifu ikiwemo kuhakikisha wanachanjwa chanjo ya kujikinga dhidi ya Uviko 19.

Pamoja na kutembelea mashina, Katibu Mkuu ametembela na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani Kasulu ikiwemo mradi wa ujenzi wa Chuo cha Veta Kasulu, na ujenzi wa Shule ya Sekondari Mayonga.

Katibu Mkuu Ndg. Chongolo pamoja na Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa, wapo Kigoma kwa ziara ya siku mbili kwa lengo la kukagua utekelezaji wa ilani ya uchaguzi na kuhamasisha uhai wa mashina wa chama ngazi za Mashina.


Imetolewa na;

Said Said Nguya

Afisa Habari

Ofisi ya Katibu Mkuu

CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM).

Thursday, 14 October 2021

October 14, 2021

TBS YAIFUNGIA JUISI YA CERES NA KUIONDOA SOKONI KWA MADAI YA KUWA NA SUMU NDANI YAKE

 

Kutokana na juisi ya tufaa ‘Apple’ iliyotengenezwa na kampuni ya Afrika Kusini ya Ceres kudaiwa kuwa na kiwango cha juu cha sumu, Tanzania inaungana na mataifa mengine saba kuiondoa sokoni.

Akizungumza leo Oktoba 14, 2021 Mkurugenzi wa udhibiti ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Lazaro Msasalaga amesema suala hilo linafanyiwa kazi.

Amesema kila bidhaa inayoingia nchini hupimwa na hivyo ikiwa itabainika toleo hilo lipo ndani ya nchi itaondolewa haraka na utaratibu mwingine wa kuichunguza utafanyika.

“Tunalifanyia kazi, toka jana tunakusanya taarifa tuone kwamba ziliingizwa na nani kama zipo na iwapo tutazibaini utaratibu utafanyika kubaini ziliingizwa lini na nani anahusika,” amesema Msasalaga.

Amesema juisi za Ceres ni salama na hazina shida isipokuwa mtu hatakiwi kununua toleo tajwa ambapo wao ‘TBS’ wanalifuatilia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 11 na Jumuiya ya soko la pamoja la nchi za mashariki na kusini mwa Afrika (COMESA) imetaja matoleo sita yaliyotolewa kati ya Juni 14 na 30 kwa Barcode 6001240200018 (Ceres Apple 4x6x200ml).

Comesa imesema miongoni mwa maeneo ambayo yameathirika zaidi na toleo hilo ni DRC Congo, Seychellies, Zambia na Zimbabwe :Chanzo Mwananchi 

gusa link hiyo hapo chini kupata radha na burudani ya mziki wa kila aina kwa muda wote

                                           http://stream.zeno.fm/0vpamwqrg98uv


Sunday, 10 October 2021

October 10, 2021

WATANZANIA MILIONI 7 WANAUGUA UGONJWA WA AFYA YA AKILI.

 

WATANZANIA MILIONI 7 WANAUGUA UGONJWA WA AFYA YA AKILI

Na Hamida Ramadhan,Dodoma 

KAIMU Mkurugenzi wa Magonjwa yasiokuwa ya kuambukiza kutoka Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Njinsia wazee na watoto Dkt.Shedrack Makubi amesema Takwimu zinaonyesha Tanzania  kuna wagonjwa wa afya ya akili Milion 7.

Akiongea leo na waandishi wa habari wakati akitoa tamko kuhusu maadhimisho ya afya ya akili Duniani na siku ya kupinga matumizi ya unywaji pombe uliopitiliza Dkt Makubi amesema magonjwa ya akili ni mzigo mkubwa katika Taifa ambapo Takwimu zinaonyesha kuwa katika jangwa la Sahara asilimia 13 wanaugonjwa wa afya ya akili.

"Tuko katika sehemu mbaya  kama Takwimu zinavyoonyesha Milioni 7 ya watanzania wanaugua ugonjwa wa afya ya akili wakati Tanzania tuko milioni 60 ni ukweli usiopingika tuko sehemu mbaya," amesema Dkt Makubi. 

Naye Mkurugenzi wa Hospitali yaTaifa ya Magonjwa ya akili Mirembe Inocent Mwombeki akiongea kwa niaba ya Waziri wa Afya Dkt  Doroth Gwajima kuhusu maadhimisho  hayo amesema kuwa upatikanaji wa huduma za magonjwa ya akili nchini bado sio wakuridhisha Kutokana na kuwepo kwa hospitali Moja tu nchi nzima ambayo ni hospitali ya kitaifa ya mirembe  iliyopo jijini Dodoma.

"Utoaji wa huduma hizi inaonekana kuwa hafifu Kutokana na Watu kusafiri kutoka maeneo mbalimbali nchini kufuata huduma  jijini Dodoma huku uwezo wa huspitali hiyo ukiwa na vitanda vya wagonjwa 590 pekeee," amesema Dkt Mwombeki

Aidha ameeleza changamoto nyingine zinazoikabili hospitali hiyo nipamoja na uchakavu wa miundombinu hasa ya  majengo kutokanana hospitali hiyo kuwa ya muda mrefu huku akiitaja  changamoto nyingine nipamoja na kuwarejesha wale waliopata nafuu kwenye jamii 

Naye Mary Katanga mwakilishi kutoka Compation ametoa wito kwa serikali  izidi kiboresha mifumo ya afya ya akili kwani kila kitu kinaanzia katika afya ya akili .

Amesema uelewa juu ugonjwa wa afya ya akili bado ni mdogo hasa kwa wao wanao wahudumia jamii ya watu wa chini.


Gusa link hiyo hapo chini kupata radha na burudani ya mziki wa kila aina kwa muda wote

                                           http://stream.zeno.fm/0vpamwqrg98uv

Sunday, 3 October 2021

October 03, 2021

NAFASI ZA KAZI LEO, WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO ROUND YA TATU 2021/22

🎓 PDF - TCU: WALIOCHAGULIWA 3RD ROUND VYUO ZAIDI YA KIMOJA 2021/22.


▪️TCU THIRD ROUND MULTIPLE SELECTIONS PDF File
✳ KUSHEA NI KUJALI, SHARE MAGROUP MENGINE TAFADHALI!
▪️Kama Uliomba Vyuo Vingi, Download PDF (361 Pages) Hii Ucheki Jina Lako Kirahisi Zaidi!

KU-DOWNLOAD PDF FILE, Bonyeza Hapa👇🏽
https://www.ajiraleo.com/2021/10/pdf-file-tcu-third-round-multiple.html

🇹🇿 LIVE UPDATES: CHEKI SELECTIONS ZA VYUO VYOTE 2021/22 + UPDATES MUHIMU ZA HESLB, TCU, RITA na NACTE.
Link=> https://bit.ly/3D7fFWc

🇹🇿 JESHI: NAFASI 250 MPYA ZA AJIRA MPYA SERIKALINI - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANZANIA.
Link=> https://bit.ly/3AQkRvS

🇹🇿 UHAMIAJI: NAFASI 350 MPYA ZA AJIRA MPYA SERIKALINI - JESHI/IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA.
Link=> https://bit.ly/3im8tg6

🇹🇿 UHAMIAJI: NAFASI 350 MPYA ZA AJIRA MPYA SERIKALINI - JESHI/IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA.
Link=> https://bit.ly/3AQkRvS

🇹🇿 JESHI: NAFASI 700 MPYA ZA AJIRA MPYA SERIKALINI - JESHI LA MAGEREZA TANZANIA.
Link=> https://bit.ly/3kHEyjT

KUCHEKI NAFASI NYINGINE MPYA ZA AJIRALEO, BONYEZA HAPA 👉🏽http://bit.ly/2JLrIQk

NOTE: IKIWA LINK HAIFUNGUKI/INASUMBUA, SAVE NAMBA YA ALIYEZITUMA.

🙏🏼SAIDIA WANAOTAFUTA FURSA NA AJIRA, SHARE MAGROUP MENGINE TAFADHALI!

Monday, 20 September 2021

September 20, 2021

TAHADHARI YATOLEWA KWA WANAONUNUA VITU HIVI KUTOKA NCHI ZA NJE

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo, amewataka Watanzania kutunza mazingira kwa kununua bidhaa rafiki zisizokuwa na kemikali zitokanazo na gesi haribifu zinazoweza kumong’onyoa tabaka la ozoni.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo
Jafo alibainisha hayo mwishoni mwa wiki wakati wa kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Kuhifadhi Tabaka la Ozoni.
Katika maadhimisho hayo Waziri Jafo, alifanya ziara ya kukagua maduka ya bidhaa za mitumba za viyoyozi na majokofu yanayotumia gesi haribifu na kusababisha kuharibu tabaka hilo.

Katika ziara hiyo alitoa elimu kwa mafundi mchundo wanaojihusisha na uuzaji na utengenezaji wa bidhaa za mitumba ya majokofu pamoja na viyoyozi vinavyotumia gesi.
Alisema ozoni ni tabaka la hewa ambalo liko katika anga la juu la pili linalofahamika kitaalamu kama stratosphere ambalo linaweka aina ya tabaka ama tambara angani na kuzuia mionzi mikali ya jua inayoweza kuleta athari katika afya za binadamu na viumbe hai kuja moja kwa moja duniani.

Alisema uharibifu wa tabaka la ozoni unasababisha madhara mbalimbali duniani ikiwamo kuongezeka kwa kiwango cha joto pamoja na kuleta mabadiliko ya tabia ya nchi jambo ambalo ni hatari kwa afya ya binadamu na viumbe hai.
"Wafanyabishara wengi wamekuwa wakiuza majokofu ya mtumba yanayotumia gesi R22 na kuharibu mazingira… uzeni mitungi ya gesi kuanzia R200 na kuendelea," alisisitiza.

Alitoa wito kwa vijana wanaojishughulisha na masuala ya ufundi wa viyoyozi na majokofu ya mtumba kutumia aina ya gesi inayoruhusiwa na viwango vya kimataifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Remidius Mwema, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anthony Mtaka, alisema Dodoma inakuwa kwa kasi na kwamba kuna haja ya kutengeneza jukwaa la pamoja litakalosaidia kutoa elimu kwa wananchi.
“Ni kweli wananchi wamekuwa wakinunua majokofu ya mtumba ambayo yameonekana kuwa na madhara na hiyo yote inatokana na kutokuwa na uelewa juu ya madhara hayo, lakini sasa kama tutakuwa na jukwaa la pamoja la kutoa elimu juu ya madhara ya bidhaa hizi za mtumba nina imani bidhaa hizo za mtumba hazitanunuliwa,” alisisitiza Mwema.
Mmoja wa mafundi anayejishughulisha na ufundi wa viyoyozi vya mtumba, Matukuta Juma, alisema kutokana na ushauri huo watahamasisha wengine kutumia mitungi ya gesi inayokubalika na kuiomba serikali kuwapunguzia bei gesi ambayo haiharibu mazingira.