SAMATTA AIONGOZA TAIFA STARS KUPATA USHINDI WA BAO 2-0 DHIDI YA BOTSWANA LEO
Timu ya Tanzania "Taifa Stars" imefanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Timu ya Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika leo Jijini Dar es salaam.
Mchezo huo uliochezwa leo kwenye dimba la Uwanja wa Taifa ilifanikiwa kutoka na ushindi huo baafa ya Mshambuliaji wa Kimataifa anayecheza soka la kulipwa nchini Ubelgiji Mbwana Samata kufunga magoli yote.
Dakika ya pili ya kipindi cha Kwanza Samata aliweza kuipatia Stars goli la kuongoza lililodumu mpaka mapumziko huku kila timu ikionekana kutafuta goli kwa udi na uvumba.
Kipindi cha pili kinaanza ambapo Botswana wanafanya mabadiliko lakini wanshindwa kutumia nafasi walizozipata.
Katika dakika ya 87, Mbwana Samata anaiandikia Stars goli la 2 kwa faulo ya nje ya 18 akiupiga mpira huo moja kwa moja ambapo mpala dakika 90 zinamalizika Stars 2-0 Botswana.
Stars wanatarajiwa kucheza tena Jumanne dhidi ya Burundi ikiwa ni muendelezo wa mechi za kirafiki za kimataifa.
Kiungo
wa Timu ya Taifa Stars, Himid Mao akiruka juu sambmba na Beki wa
Botswana kuwania mpira wa juu, katika Mchezo wa kirafiki wa rekodi za
FIFA, uliochezwa jionu ya leo katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es
salaam leo. Taifa Stars imeshinda bao 2-0.
Beki wa kati wa Botswana , Mosha Galemonthale akimchezea vibaya Mbwana Sammata.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakwembe akisalimiana na Nahodha wa Timu ya Taifa "Taifa Stars", Mbwana Ally Samatta kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Timu ya Taifa ya Botswana, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.
No comments:
Post a Comment