DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Friday, 28 April 2017

AMBER LULU ATOA MAKAVU

Amber Lulu amchana mzazi mwenzake na Young Dee

Mrembo anayepamba video za muziki, Amber Lulu amemtaka mama wa mtoto wa msanii Young Dee kuacha kumfuatilia mpenzi wake huyo kwenye mitandao ya kijamii bali aendelee na kumlea mtoto wake vizuri. 

Amber Lulu amefuguka hayo baada ya tetesi kuenezwa mitandaoni na Mamisa (mzazi mwenzake na Young Dee) kwamba mrembo huyo ndio chanzo cha mahusiano yake na rapa huyo kuharibika hali inayosababisha yeye kushindwa kupata huduma kwa mzazi mwenzake. 

"Mimi namshauri kila siku Mamisa aache kuleta mambo ya kifamilia kwenye mitandao. Young Dee ni msanii na anawatu wengi sana anaojuana nao. Anavyoendelea kuanika mambo ya Young Dee hadharani anazidi kumuharibia. Mimi sina chochote cha kufanya na Young Dee kwa sababu sisi tumeshakuwa marafiki na hakuna mahusiano zaidi ila yeye namshauri aachane na mitandao alee mtoto"- alifunguka Amber Lulu 


Hata hivyo zipo taarifa za awali ambazo zinadai Mrembo Amber Lulu alishawahi kuwa kwenye mahusiano na Paka rapa Young Dee na ukaribu wao ndio unaomtesa mama wa mtoto wa Young Dee.

No comments: