DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Saturday, 29 April 2017

Q CHIEF AONESHA JEURI

Q Chief: Sitaki kukurupuka kusaini label yoyote

Ikiwa ni miezi 3 toka msaniii wa muziki wa bongo fleva, Q Chief aachanae na label yake ya zamani, QS J Mhonda Entertainment, bado hajasaini mkataba na label yoyote.

Muimbaji huyo ambaye anajipanga kuachia wimbo wake mpya hivi karibuni, ameiambia Bongo5 kwamba, hataki kukurupuka kusaini mkataba na label yoyote.

“Namshukuru Mungu mambo yanaenda vizuri nikiwa nje ya label,” alisema Q Chief. “Label nyingi niko nazo kwenye mazungumzo na namshukuru Mungu mambo yanaenda vizuri na kikubwa zaidi sitaki kukurupuka kusaini label yoyote tu halafu baadae nijutie,”

Aliongeza, “Kama unavyoona bado niko peke yangu, pamoja na watu wangu wa karibu ambao wananisaidia lakini mambo yanaenda. Kuna label nyingine iliniambia nifanye kazi kwanza halafu tuone mambo yatakuwaje,”

WCB ya Diamond ni moja kati ya label ambazo zilionyesha dalili za kumchukua muimbaji huyo mkongwe.

No comments: