DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Thursday 11 May 2017

AFANDE SELE ATOA MFANO WA BOB MARLEY KUJIBU WAZIRI MWAKYEMBE

Afande Sele ‘amjibu’ Mwakyembe, atumia mfano wa Bob Marley

 Afande Sele

Jana, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aliwataka wasanii nchini kuacha kuimba nyimbo za kisiasa kama wanataka kufika mbali kimuziki na kupata mafanikio zaidi.

Sasa leo Afande Sele ametenga muda wake na kuandika ujumbe huu, “Kama Serekali ya Jamaica ingepiga marufuku wasanii wa nchini kwao wasiimbe nyimbo za siasa, basi siku kama leo tusingeshuhudia dunia ikiungana kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kaka yetu mkuu Robert Nesta Marley, ‘Baba Ziggy’, heshima na umaarufu wake havikujengwa kwa tungo za mapenzi, kujisifia na blah blah nyingine bali kwa siasa ambayo ndio maisha yenyewe nami kwa kumuenzi huyu nabii wangu siku kama leo natamani kuropoka kwa sauti kuu….,”


No comments: