DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Thursday 16 September 2021

MASAU BWIRE AFUNGUKA ALIVYOKABIDHIWA MIKOBA YA HAJI MANARA SIMBA



WAKATI jina la Masau Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting likitajwa kuibukia mitaa ya Msimbazi kubeba mikoba ya Haji Manara, kiongozi huyo amefungukia namna mabosi wa Simba walivyompa ofa ili awe ndani ya kikosi hicho.
Kwa sasa nafasi ya Ofisa Habari wa Simba ipo mikononi mwa Ezekiel Kamwaga ambaye anakaimu nafasi hiyo na aliweka wazi kuwa atasepa hivi karibuni kwa kuwa mchakato wa kumtafuta mbadala wake unaendelea.
Akizungumza na Championi Jumatano, Masau alisema kuwa Simba walimfuata zamani ili awe kwenye kitengo cha usemaji lakini alikataa kwa kuwa roho wa Bwana hakumpa ruhusa kufanya hivyo.
“Kuna vitu viwili unaweza kuvichanganya,kwamba mimi pengine nafurahia kwenda kufanya kazi Simba pengine ningekuwa napenda kufanya hivyo ningefanya kazi siku nyingi sana kwa sababu Simba waliwahi kunifuata ili nikafanye kazi pale.
Simba waliwahi kunihitaji siku nyingi tena kwa nguvu lakini bado roho wa Bwana alikuwa hajaruhusu walinifuata sana nilikataa ilikuwa zama za utawala wa Aveva, (Evans) na Kaburu, (Godfrey Nyange) pengine ningekubali mimi pengine Manara, (Haji) asingekuwepo pale.

No comments: