DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Showing posts with label news. Show all posts
Showing posts with label news. Show all posts

Thursday, 11 May 2017

May 11, 2017

RAMA DEE AIMEZEA MATE NAFASI KINANA

Rama Dee: Nataka nafasi kama ya Kinana, CCM

Rama Dee

Msanii wa muziki wa R&B, Rama Dee amedai kama akiingia kwenye uongozi basi anataka nafasi za juu huku akiitolea mfano nafasi ya Abdulrahman Kinana ya Ukatibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kipenda Roho’ amedai hataki nafasi ndogo ndogo ambazo kila mtu anaweza kuipata kama akiamua.

“Nitagombea ubunge mimi?, mimi nataka kuwa juu ya watu, napenda nafasi kama ya Kinana, nataka nafasi kubwa, kama katibu mkuu wa chama,” Rama Dee alimjibu mmoja ya mashabiki wake ndani ya Kikaangoni cha EATV.

Pia alisema Mh Rais  Magufuli akiamua kumteua  nafasi ya Uwaziri atakubali kwa sababu hawezi kukataa kazi aliyopewa na rais wa nchi.

Monday, 1 May 2017

May 01, 2017

CHINA WAGEUKA VIGEUGEU NA WASALITI

China wageuka wasaliti

Rais Donald Trump na Rais Xi jinping

Rais wa Marekani, Donald Trump amemsifu rais wa China, Xi jinping kwa kuiunga mkono Marekani na jitihada zake za kupambana na mpango wa Nuklia wa Korea kaskazini.

Trump amesema kupata ushirikiano huo wa kupambana na Pyongyang ilikuwa muhimu kuliko kuishinikiza Beijing kuhusu masuala ya biashara.

Rais Donald Trump amesema aliamini kuwa Rais Xi alikuwa akiishinikiza Korea kaskazini, ikitaka, mazungumzo yafanyike kuhusu silaha za Nuklia za Kim Jong Un

''Rais wa China, Rais Xi, ninaamini amekuwa akimshinikiza pia.lakini mpaka sasa, pengine hakuna kilichotokea na pengine kimetokea. Hili lilikua kombora dogo, halikuwa kombora kubwa, halikuwa jaribio la Nuklia, ambalo alitegemewa kulitekeleza siku tatu zilizopita, tutaona nini kitakachoendelea''

Trump ametahadharisha kuwa mgogoro wowote wa kijeshi na Korea kaskazini unaweza kugharimu maisha ya mamilioni ya watu.

Aliyasema hayo kwenye mahojiano na chombo cha habari cha CBS cha Marekani ambapo alizungumzia hali ya mvutano iliopo kati ya nchi yake na Korea kaskazini.

Trump amesema rais wa Korea kkaskazini , Kim Jong Un ameendelea kubaki kwenye utawala wa Korea kaskazini, ingawa wamekuwepo wale ambao wangeweza kumpinga

''alikuwa kijana mdogo wa miaka 26 au 27 hivi, alipochukua mamlaka kutoka kwa baba yake, baba yake alipofariki. Ni wazi kuwa anakabiliana na watu wenye nguvu zao, majenerali na wengine.Katika umri huo mdogo, aliweza kuchukua madaraka.Watu wengi, nina uhakika, walijaribu kuyachukua madaraka hayo, pengine, mjomba wake au mtu mwingine yeyote.hivyo ni wazi kuwa ni kijana mwerevu, lakini tuko kwenye hali ambayo hatuwezi kuifumbia macho, hatuwezi kuruhusu kilichokuwa kikiendelea kwa miaka mingi kiendelee''

Siku ya jumapili,Kiongozi huyo wa Marekani alizungumza na Mawaziri wakuu wa Thailand na Singapore kujadili namna ya kuishinikiza Serikali ya rais wa Korea kaskazini, Kim Jong.

Sunday, 30 April 2017

April 30, 2017

RAIS MAGUFULI AFANYA IBADA LEO

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 

OFISI YA RAIS,

IKULU,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Aprili 2017, ameungana na waumini wa dini ya Kikristo kusali ibada ya Jumapili katika Kanisa la Kiaskofu, Jimbo Katoliki la Moshi  ,Parokia ya Kristo Mfalme na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Moshi Mjini, Dayosisi ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro na kuwataka waumini wa makanisa hayo na Watanzania kwa ujumla kuendeleza amani iliyopo nchini kwa kuwa ndio chachu ya Maendeleo.

Rais Magufuli amesema hatua zinazochukuliwa na Serikali ya awamu ya Tano zina lengo la kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ya taifa linalomuamini MUNGU.

'' Napenda muniamini kuwa mimi nipo kwa niaba yenu, najua huu Urais si wangu, Urais mnao ninyi mlioamuwa nitumike kama mtumishi kwa wakati huu, nawaomba sana muendelee kuniweka katika sala zenu ili kazi hii ya Urais isinipe kiburi, nikawe mtumishi wa watu'' Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewashukuru waumini wa makanisa hayo mawili na watanzania kwa ujumla kwa kusimama pamoja kuliombea Taifa amani iliyowezesha wananchi kupiga kura kwa amani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na kutokana na sala zao Mwenyezi MUNGU akamuwezesha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha, Rais Magufuli ametoa msaada wa mifuko 100 ya Saruji kusaidia maendeleo ya kanisa Katoliki na Shilingi Milioni Moja kwa Kwaya ya Kanisa hilo ili irekodi nyimbo zake, halikadhalka katika Kanisa la KKKT, Mheshimiwa Rais ametoa mifuko 150 ya Saruji kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya Kanisa hilo na Shilingi milioni Moja kwa Kwaya ya Kanisa hilo.

Nae Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Jenista Mhagama amemuunga mkono Rais Magufuli kwa Kuchangia Mifuko hamsini ya Saruji ambapo Mkuu wa Mkoa wa kilimanjaro Mhe. Said Meck Sadick amechangia mifuko hamsini ya Saruji na Shilingi laki Tano.

Kwa upande wake Askofu wa Jimbo Katoliki la Moshi ,Parokia ya Kristo Mfalme Askofu Isaac Amani amemshukuru Rais Magufuli kwa uwamuzi wa kusali kanisani hapo na kuwataka waumini wa kanisa hilo na Tanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea yeye pamoja na Serikali yake ili iweze kuwatumikia Watanzania katika kuwaletea maendeleo na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya mfano kwa Bara la Afrika.

Kwa upande wake Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania - KKKT, Askofu Dr Fredrick Shoo amewataka waamini wa kanisa hilo na watanzania kwa ujumla kutokuwa na hofu kwa mambo yanayofanywa na Rais hususani katika kupambana na maovu, dhuluma na ufisadi vikiwemo na badala yake Watanzania wabadilike na kujijengea mazoea ya kufanya kazi halali na kuwa waaminifu na kuwa wazalendo kwa Taifa lao.

Aidha, Askofu Shoo amemuomba Dkt Magufuli kuangalia uwezekano wa kupunguza kodi hususani kwa taasisi za kidini zinzotoa huduma za kijamii zikiwemo zile za Elimu na Afya.

Akijibu Maombi hayo Rais Dkt Magufuli amewaeleza waamini na watanzania kwa ujumla kuwa Serikali inathamini michango ya huduma za kijamii zinazotolewa na Taasisi za dini na kuahidi kuliangalia suala hilo.

Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU.

Moshi, Kilimanjaro.

30 Aprili, 2017.

Saturday, 29 April 2017

April 29, 2017

KOREA YAICHEZEA MCHEZO MCHAFU MAREKANI

Korea Kaskazini Yafanya Magumashi ya Makombora

Korea Kaskazini imelaumiwa kwa kuonyesha silaha bandia katika maonyesho ya hivi karibuni ya ubabe wake wa kijeshi.

Afisa wa zamani wa masuala ya ujasusi anasemna baadhi ya bunduki na makombora yaliyotumiwa kwenye maonyesho hayo yalikuwa bandia.

Michael Pregent alikiambia Kituo cha Runinga cha Fox kuwa baadhi ya bunduki zilizokuwa kwenye maonyesho hayo zilikuwa ni za bandia (magumashi). Lakini maonyesho kama hayo kuonyesha ubabe wa kijeshi yametumiwa kwa miongo kadhaa.

Kwa sasa msukosuko ni mkubwa kati ya Marekani na Korea Kaskazini. Hii ni baada ya rais wa Marekani, Donald Trump kuapa kuwa ni lazima atakabiliana na vitisho vya Korea Kaskazini.

“Sio kuwa Korea Kaskazini inafikiri kuwa itashinda Marekani lakini kile itafanya ikiwa itashambuliwa,” Pregent alisema.

Silaha hizi bandia zilitengenezwa kukwepa mashambulizi ya angani na kuwachanganya marubani ya jeshi kushambulia vifaru bandia baada ya vifaru halali

Wasanii wa jeshi la Ufaransa nao walichora mito bandia na mitaro ili kuwachanganya marubani wa ndege za vita. Ujanja kama huo pia ulitumiwa wakati wa vita vya pili vya Dunia

Miti hii ilipakwa rangi hadi kifanana na silaha ya kurusha makombora. Lengo lilikuwa ni kuwachanganya maadui kuhusu ni wapi kulikuwa na adui. Aina hii ya silaha bandia zilitumika karne za 18 na 19.

Sunday, 26 March 2017

March 26, 2017

MAKABURI 22 YAFUKULIWA TZ

MAKABURI 22 YA WATU WENYE UALBINO YAFUKULIWA

Published Under habari

Chama cha watu wenye ualbino Tanzania (TAS) kimelaani vikali vitendo vya ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ualbino vinavyoendelea kujitokeza nchini hali inayowafanya waishi kwa hofu kubwa katika nchi yao. 

Inaelezwa kuwa tangu kuibuka kwa mauaji ya watu wenye ualbino mwaka 2007 takribani makaburi 22 nchini  Tanzania yamefukuliwa na watu wasiojulikana.

Chama hicho kimeiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Pombe Magufuli kuweka mkazo katika mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi kama ilivyoonesha nguvu za kutosha katika vita ya dawa za kulevya na pombe aina ya viroba. 

Akizungumza juzi kwenye kikao cha viongozi wa chama watu wenye ualbino kutoka mikoa ya kanda ya Ziwa ambayo ni Mara,Mwanza na Shinyanga na wanachama wengine Afisa mahusiano na habari TAS taifa Josephat Torner vitendo vya kufua makaburi ya watu wenye ualbino yanatishia amani yao 

Torner alisema wanaiomba serikali kuelekeza nguvu katika masuala ya mauaji na ufukuaji wa makaburi ili kuwafanya watu wenye ualbino waishi kwa amani ndani ya nchi yao. 

“Katika suala la mauaji ya watu wenye ualbino ambao wamekuwa wakiishi kwa hofu tunaomba serikali hata kuwataja kwa majina wanunuzi hao kama ilivyotokea kwenye masuala ya vita ya dawa zakulevya na uuzaji bombe aina ya viroba”,alisema Torner. 

Aidha alisema wanalaani kitendo cha kufukuliwa kwa kaburi la Nelson Msogole (50) aliyekuwa akiishi mji wa Songwe baada ya kufariki tarehe 28/3/2011 na kaburi lake kuonekana kufukuliwa tarehe 20/3/2017na watu wasiojulikana. 

“Matukio haya yanaendeshwa kwa usiri hivyo tunahoji kwanini imeshindikana ikiwa kwenye dawa za kulevya wameweza kutaja na kumepiga hatua?”,alihoji Torner. 

Alisema Tangu kuanze kuibuka mauaji ya watu wenye ualbino mwaka 2007 makaburi 22 nchini yamekwisha fukuliwa katika mikoa ya Mbeya ,Tabora,Mwanza,Mara ,Kagera,Rukwa, na Shinyanga. 

Aliiomba serikali ya awamu ya tano iweke mikakati ya uelewa kwenye jamii kwani huenda hawana uelewa na watuhumiwa wakibainika waadhibiwe kwa mujibu wa sheria. 

“Hiki ni kipimo cha serikali ya awamu ya tano kwa sauti ya wanyonge kwani kuna baadhi ya watu wanaishi kwenye nchi yao kwa hofu na unyonge na kuondolewa utu wao hivyo tuna imani serikali itaweka nguvu kubwa kuliko kipindi cha nyuma”,aliongeza Torner. 

Naye Mwenyekiti wa chama hicho kutoka mkoani Mwanza Alfredy Kapole alisema mkoa wa Mwanza unaongoza kwa mauaji ya vifo vya albino zaidi ya 17 vimetokea tangu mwaka 2007 hivyo aliiomba serikali kuweka ulinzi mkubwa kwa watu hao kwani wanakiuka katiba ya nchi kwani kila mtu anastahili kuishi. 

Mwenyekiti wa chama hicho kutoka mkoani Mara Joseph Sinda alisema kitendo cha kufukua kinawafanya waishi kwa hofu kubwa na kuitaka serikali ijaribu kuchunguza chanzo chake ni nini na kuthibiti kama kwenye madawa ya kulevya na pombe aina ya viroba walivyofanya ili waweze kuishi kwa amani. 

Mwanaharakati kutoka mkoani wa Shinyanga Eunice Zabroni aliiomba serikali wawaimarishie ulinzi na elimu itolewe kwani wanaishi kwa hofu kwa kukosekana ulinzi imara kuanzia ngazi ya vitongoji,vijiji kata na wilaya hadi mkoa. 

Katikati ni Afisa mahusiano na habari wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS )Josephat Torner akizungumza wakati wa kikao cha viongozi na wanachama wa chama hicho ambapo walilaani vitendo vya ufukuaji wa makaburi ya watu wenye ualbino.Kulia ni Mwenyekiti TAS mkoa wa Mara  Joseph Sinda,kushoto ni mwenyekiti TAS mkoa wa MwanzaAlfred Kapole -Picha zote na Suzy Butondo-Malunde1 blog

Afisa mahusiano na habari wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania (TAS )Josephat Torner ambapo alisema chama hicho kinaiomba serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na rais John Magufuli kuongeza kasi katika mapambano dhidi ya ukatili wa watu wenye ualbino

Baadhi ya wanachama wa chama cha watu wenye ualbino nchini Tanzania wakiwa katika kikao hicho.

Friday, 24 March 2017

March 24, 2017

MADAKTARI WAPEWA SIKU 60

WAKENYA WATOA SIKU 60 KWA MADAKTARI WA TANZANIA

Published Under habari

Chama cha madaktari nchini Kenya kimewataka madktari kutoka Tanzania kusubiri baada ya miezi miwili ndipo waende nchini humo kwa ajili ya kufanya kazi ambayo imetangazwa kwa madaktari wa Tanzania kama fursa.

Hayo yamethibitishwa na Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dkt. Obadia Nyongole katika kipindi cha Hot Mix cha EATV na kusema kuwa taarifa hiyo imetoka kutoka chama cha madktari cha Kenya na kuwataka watanzania kusubiri kwanza watimiziwe malipo yao na serikali ya nchi hiyo

Dkt. Obadia ameendelea kusema kwamba pamoja na chama hicho cha madaktari cha Kenya kufurahi kuona watanzania wamejitolea kwenda kuwasaidia katika mgogoro unaoendelea bado kinaona kuwa ni sawa na kwenda kuwazibia wazawa fursa za kazi kitu ambacho kitaweza kusababisha vita vya kitaaluma.

Katika hatua nyingine Obadia ameongeza kwamba pamoja na kuwa si jambo la kushangaza serikali kusaidia wasomi wake kupata ajira nchi tofauti tofauti, fursa ya madaktari 500 kwenda Kenya kwa upande wao bado wana hofu nayo.

“Fursa hii haijaja wakati muafaka, imekuja mapema mno kwani mgogoro bado upo unaendelea nchini Kenya. Vitisho ni vingi wanaamini na bado madaktari hao hawana imani kama serikali yao itaweza kutekeleza ahadi, tunawasiliana na madaktari wenzetu dunia nzima, hata kenya tunawasiliana nao, chama cha madaktari Kenya hawana shida lakini pia wasiwasi wao ni  mwezi Mei kutakuwa na zaidi ya wanafunzi 1400 wanao hitimu watakuwa hawana ajira” Obadia alisema.