DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Saturday, 25 March 2017

NAPE AINGIA KWA KISHINDO UWANJA WA TAIFA WAKATI TAIFA STARS IKICHEZA

Katika hali ya kushangaza aliyekuwa Waziri wa habari utamaduni michezo na wasanii mheshimiwa nape nnauye amewashangaza wapenzi wa mpira na washabiki waliojitokeza kuishangilia timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars wakati timu hiyo ilipokuwa ikicheza na timu ya taifa ya Botswana Leo jumamosi march 25,2017
   Nape ambaye amejitokeza uwanjani hapo majira ya SAA 16:50 Mara tu baada ya mapumziko ya timu hizo ameonekana kushangiliwa na mashabiki wote waliokuwa uwanjani hapo huku akifanya wengi kusahau kufuatilia matangazo yaliyokuwa yakitolewa na chumba cha matangazo uwanjani hapo kuhusu mechi hiyo
   Nape ambaye ameonekana kwenye jukwaa la VIP juu karibu na mlango wa kuingilia vumba vya kubadilishia nguo amewapungia mashabiki hao mikono huku akipigiwa makofi kwa kishindo kikubwa
Ikumbukwe kuwa hadi wakati huu Tanzania inaongoza kwa gori 1 dhidi ya Botswana gori lililofungwa mapema kabisa na mbwana samatta
Mungu ibariki Tanzania mungu ibariki Afrika

No comments: