DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Saturday 6 May 2017

MAMA YOUNG KILLER AMPIGIA MAKOFI DIAMOND

Mama Young Killer afunguka haya kumuhusu Diamond

Kitendo cha Diamond Platnumz kuamua kumshirikisha rapa Young Killer kwenye moja kati ya nyimbo zake zinazokuja kimemfurahisha mama mzazi wa rapa huyo.

Wiki chache zilizopita Diamond alisema kuna moja kati ya project zake ambazo zinakuja amemshikisha rapa huyo kijana huku akimmwagia sifa kwa uwezo mkubwa aliouonyesha kwenye project hiyo.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii, Young Killer amesema mama yake alifurahishwa sana na kitecho cha mkali hiyo wa ‘Marry You’ kutamka hadharani jinsi anavyoukubali muziki wa mtoto wake.

“Hiki kitendo kimenifanya nimuone Diamond Platnumz ni binadamu na ni mtu ambaye anastahili kuwepo sehemu ambayo yupo. Ni tukio ambalo limenitia faraja kiukweli hata mama yangu alivyosikia alifurahia sana na kumshukuru kwa kitendo ambacho amenifanyia,” alisema Young Killer.

No comments: