DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Wednesday 3 May 2017

MRISHO MPOTO AJIBU SHAMBULIZI

MRISHO MPOTO AJIBU SHAMBULIZI

Msanii Mrisho Mpoto jana  May 2 ameamua kutumia ukurasa wake wa instagram kuandika kuhusiana na wale wanaomtusi na kumponda kutokana na kuonesha kuunga mkono utendaji wa Rais Magufuli.

 Mrisho Mpoto ameeleza kwa nini ameamua kumuunga mkono Rais Magufuli na  amesema ataendelea kumuunga mkono.

“Nimepokea matusi mengi, kebehi, na maneno machafu juu ya mimi kuunga mkono utendaji wa Rais Magufuli, kitu ambacho nakiamini kuna “KUKUBALIANA KWA KUTOKUBALIANA” lakini siyo kumtukana mtu mwingie siyo busara hata kidogo

“Kwakuwa tu hakusema au hakufanya ambacho nafsi yako ilipenda kusikia. Kilichonifanya niandike ujumbe huu ni kuwa nisiwekewe maneno mdomoni yakuwa nimesema Rais Magufuli ni Mungu, kwa wale ambao hawakuangalia sherehe za MEI MOSI jana

“Naomba niseme kuwa hayo maneno siyo kweli na yamebadilishwa kutoka kwenye ukweli wa niliosema, Mimi ni mtu mwenye hofu na Mungu siwezi kusema hivyo, kumekuwa na utamaduni ikitokea mtu anauunga mkono utendaji wa Rais kuna ibukuka kundi la wapinga Maendeleo na kuanza kutukana

“Naomba ijulikane kuwa sababu za kumuunga mkono Rais, yale niliyokuwa nayaongea huko nyuma naona yanafanyiwa kazi hivi sasa!! MRISHO MPOTO mpaka sasa namuunga mkono Rais MAGUFULI, Iwe nachumia tumbo kama inavyosemwa au nimevimbilwa kwa shibe

No comments: