DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Sunday 18 June 2017

MADHARA YA ULAJI WA NYAMA

Ukiangalia historia ya vitabu vitakatifu kama biblia, kabla ya gharika ya nuhu watu walikua hawaruhusiwi kula nyama kabisa, ila waliruhusiwa kula matunda na mboga mboga za kondeni. Sidhani kama mungu aliwakataza kwa bahati mbaya kwani miaka ya sasa tafiti nyingi zinaonyesha watu wanaokula nyama
wanapata magonjwa mengi kuliko wale wasio kula na pia atu wasiokula nyama huishi muda mfupi kuliko wasiokula na hata kwenye historia ya biblia inaonekana watu wa zamani waliishi miaka mingi sana ukilinganisha na walioishi baada ya gharika yaani sisi.
Lakini hata hivyo historia inaonyesha kwamba hata kabla ya gharika la nuhu watu waliasi na kuanza kula nyama nyama.
baadae baada ya gharika mungu aliamua kuruhusu kuliwa kwa baadhi ya nyama na kukataza baadhi ya nyama. Siku moja nilikua naongea na mchungaji mmoja msabato kuhusu sheria zao za kula nyama na vyakula mbalimbali nikagundua kwamba sio sababu za kibiblia tu kwani kuna vitu wasabato hawatumii vitu kama majani ya chai, soda za cocacola na kadhalika lakini kwa sababu za kiafya zaidi.
Leo tutangalia madhara ya kula nyama… lakini kabla ya kuangalia madhara ya nyama kuna makundi makuu mawili ya nyama yaani nyama nyekundu na
nyama nyeupe .

Nyama nyekundu ni ile ambayo ina rangi nyekundu kabla ya kupikwa mfano nguruwe, ng’ombe,mbuzi, na wanyama wote wanaotembea kwa miguu minne.

Nyama nyeupe ni zile ambazo zina rangi nyeupe kabla ya kupikwa mfano kuku, bata, samaki, mbuni na wanyama wote wanaotembea kwa miguu miwili.

Utafiti unaonyesha ulaji wa nyama nyekundu una madhara makubwa sana kuliko ulaji wa nyama nyeupe hata hivyo watu ambao hawali nyama kabisa wako mbali sana na hatari hizi. Lakini kwa kua nyama pia ina faida katika miili yetu basi nyama nyeupe ni salama sana kuliko nyekundu.Hebu tuangalie madhara ya nyama kama ifuatavyo.

Hatari ya kupata magonjwa ya moyo: nyama ina kitu kinaitwa lehemu kitaalamu kama cholesterol, hii hukaa kwenye mishipa ya damu ya binadamu na kusababisha damu kushindwa kupita vizuri..hii husababisha viuongo muhimu vya mwili kama moyo kukosa damu ya kutosha na kuanza kushindwa kazi. Japokua cholesterol ni muhimu kwenye mwili wa binadamu lakini inayotengenezwa na mwili inatosha hii inayoongezeka kutoka kwnye nyama ni hatari sana.[nyama nyekundu ina cholestrol nyingi zaidi]

Kansa ya utumbo mkubwa ; nyama nyekundu ikiliwa inakaa masaa ishirini kwenye mfumo wa chakula wa binadamu tofauti na vyakula vingine. Utafiti unaonyesha limbikizo hilo linaambatana sana na hatari ya kupata ugonjwa wa kansa ya utumbo mkubwa. Lakini madhara ya haya yameonekana kutokuwepo kwa kula nyama nyeupe.

Ugonjwa wa kisukari; utafiti mpya umeonyesha kwamba watu wanaokula nyama na wasiokula nyama baada ya kufuatiliwa kwa muda wa miaka kumi mfulululizo[cohort studies}… watu wanaokula nyama wameonekana kupata ugonjwa wa kisukari sana kuliko wale wasiokula.

Hatari ya kupata ugonjwa wa alzheirs disease; huu ni ugonjwa wa akili ambao huwapata watu wengi uzeeni na dalili yake ikiwa ni kupoteza kumbukumbu kabisa. Wanasayansi wanaamini protini inayopatikana kwenye nyama kwa jina la Tau and beta-amyloid huharibu mishipa ya fahamu ya kwenye ubongo na kuchangia kwa ugonjwa huu.

Ugonjwa wa kifafa; minyoo inyopatikana kwenye nguruwe kitaalamu kama taenia solium hupanda mpaka kwenye ubongo na kuharibu mishipa ya fahamu ya ubongo hali ambayo husababisha kifafa kwa watu ambao hawakuzaliwa nacho kabisa. Halii hii inaweza kuzuiliwa kwa kupika nyama hiyo kwa muda mrefu sana mpaka iive.

Unene uliopitiliza ; nyama nyekundu ina kiwango kikubwa cha mafuta ambacho watu wengi hula mafuta hayo kama yalivyo mfano kwenye nyama ya nguruwe.unene na kitambi ni hatari sana kwana husababisha matatizo mengi
 ya kiafya na kisaikolojia,
vifo vya ghafla vikiwa hatari zaidi kwenye swala la unene.

Nyama tunazokula siku hizi sio nyama halisi tena ; ukiangaliwa nyama ya kuku inayoliwa sana kwenye miji mikubwa na hotel kubwa hapa Tanzania hapa namaanisha kuku sa kisasa, zinakuzwa kwa kemikali nyingi sana ambazo ni hatari kwa mwili wa binadamu na hata ladha yake ni tofauti kabisa na kuku wa kienyeji. Lakini kwasababu wamiliki wa biashara za nyama ni watu wenye fedha nyingi sana duniani ukweli huu hufichwa.
Magonjwa ya wanyama husika; miaka ya sasa dunia imekua inakumbwa sana na magonjwa ambayo yanashambulia wanyama. Yameua watu wengi na mengine hayatibiki kabisa. mfano mafua ya ndege, ugonjwa wa ukimwi ambao historia inasema ulitoka kwa kula nyama ya nyani wa porini, na ugonjwa wa ebola ambao virusi vyake huishi kwenye nyama wa popo.

Mwisho; 
nyama ya nyeupe yaani samaki, kuku, bata na ndege wengine wanaoruhusiwa kuliwa ni salama sana kuliko nyama nyekundu kama mbuzi, ng’ombe, nguruwe na wengine ni hatari sana. Na kama wewe tayari una tazizo la moyo, presha, kisukari na kansa huu ni wakati sahihi wa kuacha kula nyama nyekundu kabisa kwani hizo nyama zitakupeleka kaburini.