Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, (IGPSimon Sirro amewataka ndugu wa Hamza Mohammed kwenda kuuchukua  mwili huo kwakuwa wameshamaliza kuufanyia kazi.

IGP Sirro ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Agosti 28, 2021 wakati Jeshi la Polisi likiwaaga Makamishna wake, Balozi Valentino Mlowola na Robert Boaz amesema tayari wameshaufanyia kazi mwili huo hivyo ndugu zake wanaweza kwenda kuuchukua na wakishindwa mwili huo utazikwa na Halmashauri.

“Hiyo familia ya Hamza inajisikiaje, fikiria wewe ungekuwa baba yake Hamza, mama yake Hamza, mdogo wake ungejisikiaje kuzaa kwako umetuletea balaa Watanzania, kwahiyo naomba Watanzania wengine wasituzalie watoto kama Hamza”- IGP Simon Sirro

Hamza aliuwawa Agosti 25, 2021 kwa kupigwa risasi na polisi dakika chache baada ya kufanya mauaji ya  askari Polisi watatu na mlinzi wa kampuni binafsi karibu na ubalozi wa Ufaransa na daraja la Salenda jijini Dar es Salaam.