DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Saturday 21 August 2021

MARUFUKU KUNUNUA CHAPATI ZAIDI YA TANO



Polisi katika wilaya ya Moroto kaskazini mwa Uganda wameanza kuwakamata watu wanaonunua chapati tano au zaidi, wakishuku huenda wanawalisha wezi wa mifugo katika eneo hilo, Uganda Radio Network (URN) inaripoti.

Tumepokea taarifa kwamba wale wanaonunua chapati nyingi wanawapelekea wapiganaji misituni," Micheal Longole, msemaji wa polisi wa Karamoja, alinukuliwa URN.
Alisema kukomesha usafirishaji wa chakula kwa wezi hao huenda kukawalazimu kutoka mafichoni na kuwasilisha silaha zao.

Mwanaharakati wa amani wa eneo hilo Mark Koryang alisema mpango huo hautafaulu "Hawa wapiganaji wanaweza kuishi bila hata kula chapati," alisema. Mkazi mwingine aliiambia URN kwamba maafisa wa usalama walihitaji kufanya kazi na watu wa eneo hilo ili kukabiliana na ukosefu wa usalama katika jimbo hill.

Bunduki 58 zimepatikana katika eneo zima tangu zoezi la upokonyaji silaha lilipoanza mnamo Julai 17, Edrine Mawanda, msemaji wa kitengo cha jeshi anayefanya zoezi hilo, aliiambia URN..

No comments: