Serikali ya Zimbabwe imeanza kufungua makanisa,lakini kwa waumini tu waliopatiwa chanjo ya corona ndio watakaoruhusiwa kushiriki ibada.
Kufuatia wimbi la tatu la uviko 19 nchi hiyo ilipiga marufuku mikusanyiko ya watu ambayo ilihusisha pia huduma za ibada
Mamlaka za Afya zilisema hali ilikuwa mbaya zaidi tangu wimbi la tatu la ugonjwa huo lianze
Serikali ya nchi hiyo pia imejaribu kuongeza matumizi ya chanjo za Covid-19 kwa kuondoa posho kwa wafanyikazi wa umma ambao hawajachanjwa na kuwazuia kutumia usafiri wa bure kwenda kazini.
Hadi kufikia jana Jumatano Agosti 11, 2021, Wazimbabwe milioni 1.9 walikuwa wameshapokea dozi zote mbili za chanjo za Uviko 19.
No comments:
Post a Comment