DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Wednesday 11 August 2021

SERIKALI IMETOA BILIONI 259.96 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA


 Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa kiasi cha shilingi bilioni 259.96 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Nishati, Mhe. DKt. Medard Kalemani wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Bukome, Kijiji cha Nyakato, Wilayani Chato Mkoani Geita tarehe 10 Agosti, 2021.

Waziri Kalemani amewataka wananchi hao kuchangamkia fursa mbalimbali za ujenzi wa bomba la mafuta litakalopita katika mikoa 8 ya Kagera, Geita, Shinyanga,Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga.



Waziri Kalemani amezitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na usafirishaji, ulinzi, chakula, vinywaji, huduma ya malazi na mafuta kwa ajili ya magari na mitambo. Amezitaja fursa nyingine kuwa ni pamoja na shajala, bidhaa za ujenzi zinazopatikana hapa nchini, shughuli za ujenzi, huduma za mawasiliano na ukodishwaji wa mitambo ya ujenzi.

Dkt. Kalemani ameeleza kuwa Jumla ya shilingi bilioni 28 zinategemea kulipwa kwa wananchi waliopitiwa na bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga nchini Tanzania.

Aidha, Waziri Kalemani amesema, mradi wa ujenzi wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi utaanza kutekelezwa ifikapo Septemba 2021.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, Mkuu wa Wilaya ya Chato Martha Mkupasi amewataka wananchi kutunza miundombinu ya bomba la mafuta ambayo itapita kwenye maeneo yao.


No comments: