Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka chadema kubadilika na kuanza kufanya siasa za hoja, zenye kutoa kipaumbele maendeleo ya wananchi na Taifa badala ya siasa hizi za kuhimiza ghasia, vurugu na kueneza uongo na chuki nchini.
Pia chama hicho kimemtaka Mnyika kuacha upotoshaji na kumlisha maneno Rais ambayo hakuyasema au kuingilia mwenendo wa kesi ya Mbowe mahakamani .
Hayo yameelezwa na katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Shaka Hamdu Shaka alipoulizwa kuhusu tuhuma alizozitoa katibu mkuu wa chama hicho John Mnyika mapema dhidi Rais Samia.
Shaka amesema katika maelezo ya Rais Samia aliyoyatoa wakati wa mahojiano na kituo cha BBC Swahili cha nchini Uingereza yaliyofanyika Ikulu ya Dar es Salaam alisema hakuna mahali Demokrasia imeminywa nchini na ndio maana vikao vya kikatiba vya vyama mbalimbali vya siasa nchini vinaendelea. Aidha alisisitiza siasa zenye mrengo wa vurugu na ghasia hizo hazina nafasi na wala hazitavumiliwa kwani hiyo sio demokrasia. Hivyo Mnyika aache kumlisha maneno Rais Samia.
"Chadema waache vioja vya kudai demokrasia imeminywa na hawaruhusiwi kufanya mikutano wala vikao wakati wameendesha operesheni haki, chadema kidigitali na vikao mbalimbali vya ndani bila bugudha yoyote. Lakini cha ajabu tena (leo) Mnyika ameendelea kuuingilia uhuru wa mahakama jambo ambalo linaoonyesha jinsi alivyo na papara na jazba Mnyika zinazvyomzidisha hofu kadri anavyolalamika." Alisema Shaka
"Bahati mbaya ni kwamba hawana desturi ya kufanya mikutano, vikao au operesheni zao za kisiasa kwa amani na kwa kufuata taratibu na sheria hivyo wabadilike.
No comments:
Post a Comment