DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Tuesday, 8 November 2022

CHAMA NA AZIZI KI WAPIGWA NYUNDO NA TFF.

 

Wachezaji Cletous Chama wa Simba sc na Stephane Aziz Ki wa Yanga sc wamefungiwa michezo mitatu na adhabu ya faini ya shilingi milioni tano kwa kosa la kutosalimiana na wachezaji wenzao katika mchezo wa ligi kuu uliozikutanisha klabu zao Oktoba 23 mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na bodi ya ligi kuu nchini imesema kuwa wachezaji hao wamefungiwa kutokana na kuzingatia kanuni ya 41:5(5.4) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa wachezaji.

Kutokana na kufungiwa huku timu za Simba sc na Yanga sc zitaathirika sana kwa sababu wachezaji hao wamekua nguzo kubwa katika klabu hizo hasa katika kujenga mashambulizi na kupelekea kuwa na umuhimu mkubwa katika vikosi vya timu hizo huku Simba sc ikionekana kuathirika zaidi kutokana na kutokua na mbadala mwenye ubora wa kumfikia Chama katika eno analocheza.

Chama ataanza kuitumikia adhabu hiyo kesho ambapo klabu yake ya Simba sc itamkosa itakapocheza mchezo mkali na wa kusisimua dhidi ya Singida Big Stars katika uwanja wa Liti mkoani Singida ambapo tayari klabu ya Simba sc imeshawasili ambapo pia Chama ataikosa michezo mingine dhidi ya Ihefu na Namungo.

Stpehane Aziz Ki yeye ataikosa michezo dhidi ya Kagera Sugar ugenini siku ya Jumatatu pamoja na michezo dhidi ya Singida na ule wa Novemba 22 dhidi ya Dodoma jiji ugenini


No comments: