Saturday, 23 September 2023
AJALI YA ROLI YAUA WATU 9
WATU tisa wamefariki dunia mkoani Mbeya baada ya dereva wa lori lenye namba za usajili BCE 9384/ABX8675 kushindwa kulimudu gari lake kwenye mtelemko mkali wa Mbalizi na kwenda kuigonga gari ya abiria na yenye namba za usajili T.636 DQY aina ya Mitsubishi Rosa .
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mbeya,Benjamin Kuzaga amesema kuwa tukio hilo limetokea Septemba 22 mwaka huu majira ya saa 11.40 jioni katika eneo la mteremko wa Iwambi wilaya ya Mbeya Vijijini mkoa wa Mbeya .
Kamanda Kuzaga amesema kuwa gari yenye namba za usajili BCE 9384/ABX 8675 aina ya Howo mali ya kampuni ya Horn Afric Motors ltd ya nchini Zambia ikitokea Mbeya kuelekea Tunduma likiendeshwa na dereva Mohamed Abilah (47) Mkazi wa Zambia .
Aidha Kuzaga ameeleza kuwa gari hilo iliigonga kwa nyuma Gari yenye namba za usajili T.636 DQY aina ya Mitsubishi Rosa ikitokea Mbeya mjini kuelekea mbalizi ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva ,Elly Mwakalindile (41)mkazi wa Iyunga na kusababisha vifo vya watu Tisa ambapo kati yao wanaume watano na wanawake wanne.
Aidha kamanda Kuzaga amesema kuwa katika ajali hiyo watu 23 walijeruhiwa kati ambapo kati yao wanaume 13 na wanawake 10 ni majeruhi na wanaendelea kutibiwa katika Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo Mji Mdogo wa Mbalizi na wengine wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.
Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali Teule ya Ifisi Mbalizi ambapo miili ya marehemu 07 imetambuliwa huku miili ya watu 02 ikiwa bado haijatambuliwa.
Chanzo cha ajali hii ni Dereva wa lori kushindwa kulimudu gari lake kwenye mteremko mkali na kwenda kuigonga kwa nyuma Gari ya abiria na kuwa Dereva wa lori amekamatwa na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa madereva ambao wanapita katika Mkoa wa Mbeya kwenye milima na miteremko mikali kuhakikisha wanakagua magari yao kabla ya kuanza safari na wamiliki wa magari wasiruhusu magari yao kuendeshwa na madereva hao ili kuepusha ajali.
Tuesday, 8 November 2022
CHAMA NA AZIZI KI WAPIGWA NYUNDO NA TFF.
Wachezaji Cletous Chama wa Simba sc na Stephane Aziz Ki wa Yanga sc wamefungiwa michezo mitatu na adhabu ya faini ya shilingi milioni tano kwa kosa la kutosalimiana na wachezaji wenzao katika mchezo wa ligi kuu uliozikutanisha klabu zao Oktoba 23 mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 1-1.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na bodi ya ligi kuu nchini imesema kuwa wachezaji hao wamefungiwa kutokana na kuzingatia kanuni ya 41:5(5.4) ya ligi kuu kuhusu udhibiti wa wachezaji.
Kutokana na kufungiwa huku timu za Simba sc na Yanga sc zitaathirika sana kwa sababu wachezaji hao wamekua nguzo kubwa katika klabu hizo hasa katika kujenga mashambulizi na kupelekea kuwa na umuhimu mkubwa katika vikosi vya timu hizo huku Simba sc ikionekana kuathirika zaidi kutokana na kutokua na mbadala mwenye ubora wa kumfikia Chama katika eno analocheza.
Chama ataanza kuitumikia adhabu hiyo kesho ambapo klabu yake ya Simba sc itamkosa itakapocheza mchezo mkali na wa kusisimua dhidi ya Singida Big Stars katika uwanja wa Liti mkoani Singida ambapo tayari klabu ya Simba sc imeshawasili ambapo pia Chama ataikosa michezo mingine dhidi ya Ihefu na Namungo.
Stpehane Aziz Ki yeye ataikosa michezo dhidi ya Kagera Sugar ugenini siku ya Jumatatu pamoja na michezo dhidi ya Singida na ule wa Novemba 22 dhidi ya Dodoma jiji ugenini
Saturday, 5 November 2022
KOSTROMA; DEADLY FIRE IN RUSSIAN BAR STARTES BY FLARE GUN
A fire in a bar in the Russian city of Kostroma has killed at least 13 people.
Authorities say it may have begun when a drunk customer at the nightclub fired a flare gun on the dance floor, Russian media report.
The fire reportedly spread when parts of the lighting rig on the ceiling ignited, quickly filling the room with smoke. It took several hours for it to be extinguished.
A suspect, said to be a local resident, has been arrested.
It took emergency workers several hours to put out the fire, which began at around 02:00 local time (23:00 GMT) in Kostroma, 300 km (180 miles) northeast of Moscow.
Russia's investigative committee said a 23-year-old man had been arrested on suspicion of using a "pyrotechnic" object inside the building which led to the fire.
The director of the company which manages the club has also been arrested.
Tass news agency quoted a law-enforcement source as saying that the suspected perpetrator had admitted responsibility.
"He was spending time with a woman, ordering flowers for her while he held a flare gun. Then he went to the dance floor and fired it," the source said.
The exact number of people inside the club at the time is not known, but 250 people were able to evacuate.
Images of the single-storey building engulfed in flames were shown on Russian state television, which said some safety measures had not been properly observed.
According to BBC Russian, the company which manages the club is owned by a local politician.
In 2009, 159 people died in a nightclub in the Russian city of Perm.
source BBC
Monday, 15 November 2021
AMUUA BINTI YAKE BAADA YA KUKATAA KUOLEWA
Thursday, 11 November 2021
Monday, 11 October 2021
#BADNEWS: AJALI YA BAJAJI YAUA WATATU
Friday, 1 October 2021
BUMBULI ATOA TAMKO LA KISHUJAA:TUNATAKA KUKAA KILELENI
"Kesho tunataka kushinda na kuongeza alama ili tukae kileleni mwa ligi maana kuna watu wanatubanabana pale tunataka kila mtu akae katika nafasi yake'. Bumbuli
Friday, 17 September 2021
AJALI YAUA WANAFAMILIA SITA (6) NA KUJERUHI TISA (9)
Na Amon Mtega ,Mbinga
WATU sita wanaodhaniwa kuwa ni wanafamilia wamefariki Dunia na wengine tisa kujeruhiwa kwa ajali ya gari lililoacha njia na kupinduka katika maeneo ya mteremko wa Kijiji cha Kipololo na Lundumato Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Joseph Konyo amelitaja tukio hilo kuwa limetokea Septemba 16 mwaka huu majira ya saa nane mchana huko katika mteremko mkali wenye urefu wa zaidi ya kilometa 1,wa Kijiji cha Kipololo ambapo gari hilo lenye namba za usajili T.503 DWF Toyota Coaster mali ya Joseph Ferdinand Eugeni wa Dar es salaam liliacha njia kisha kupinduka na kutumbukia kwenye bonde lenye urefu wa takribani mita 120 wakati likielekea Wilaya ya Nyasa kwenye mambo ya kifamilia.
Hata hivyo kamanda Konyo ametoa rai kwa madereva wageni na barabara za mkoa wa Ruvuma kuacha tabia ya kutumia mazoea wanapoendesha vyombo vya moto (Magari)kwa kuwa barabara za Mkoani humo asilimia kubwa zinakona nyingi na miteremko mikali.
Wednesday, 25 August 2021
MMOJA AJINYONGA NA KUACHA UJUMBE KUHUSU BARAKOA
MHITIMU wa Ualimu ngazi ya Astashahada ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Majengo, Kata ya Ichenjezya wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe amejinyonga na kuacha ujumbe akiwasihi wazazi wake kuzingatia matumizi ya barakoa
Monday, 23 August 2021
AJALI YAUA WATUMISHI WATANO WA TRA
Watumishi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kikosi kazi cha Fast Track wamefariki kwa ajali katika eneo la Hanseketwa - Old Vwawa wakati wakifukuzana na gari iliyodhaniwa kubeba magendo.
Sunday, 22 August 2021
ASKOFU GWAJIMA NA MZEE GWAJIMA WAMKABILI WAZIRI DOROTH GWAJIMA
Thursday, 19 August 2021
TANZIA: MWALIMU KASHASHA AFARIKI DUNIA
BWANA ametoa na BWANA ametwaa, jina lake lihimidiwe



































