DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Saturday, 5 November 2022

MAANDALIZI KUELEKEA TAMASHA LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO

 


 

Makamu wa raia wa Jamhuri ya muunganowa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la 41 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) lililopangwa kufanyika kwa siku tatu mfululizo Novemba 10-12,2022 kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.

 

Katika kikao cha kamati ya maandalizi kilichofanyika mjini Bagamoyo kikiongozwa na katibu mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi kufanya maandalizi ya mwishoni ikiwemo kupanga ratiba za uendeshaji wa tamasha lenyewe kwa kipindi chote cha siku tatu.

 

Katika kikao hicho katibu mkuu amesema tamasha la msimu huu ambalo litakua la 41 tangu kuanzishwa kwake litakua na washiriki wengi zaidi ikiwemo vikundi mbalimbali vya Sanaa kutoa ndani na mataifa mengine, nakuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wizara.

 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdalla amesema hali ya usalama kwa wilaya hiyo ni swari na kwamba ulinzi utaimarishwa kipindi chote cha tamasha, akiwataka wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani kujitokeza na kuwa tayari kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

 

“Mbali ya kuwa wageni watakuja kwa ajili ya Tamasha lakini pia Bagamoyo ni eneo lenye fursa mbalimbali hasa za kiutalii hivyo ni fursa kwao wageni kujionea pia wenyeji tujiandae kuwapokea”. Alisema DC Zainab.

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa wasanii wanaofanya mziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Mike Francis Mwakatundu amesema tamasha la kimataifa la Sanaa na utamaduni Bagamoyo limesaidia kutambulisha idadi kubwa ya wasanii kimataifa pia kufahamiana na wasanii wa mataifa mengine.

 

“Kwa sisi wasanii limekua linatusaidia sana kututambulisha kimataifa na kutuwezesha kukutana na wasanii wengine, mfano kwenye tamasha la msimu huu tayari tuna wasanii kutoka Burundi,Canada,India, Ufarasa na maeneo mengine tunavyo kutana hapa tunabadilishana uzoefu kwa kila msanii kwa eneo lake”.Alisema Mwakatundu


No comments: