DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Showing posts with label kijamii. Show all posts
Showing posts with label kijamii. Show all posts

Saturday, 5 November 2022

November 05, 2022

SERIKALI HAITASITA KUWACHUKULIA SHERIA WAKWEPA KODI PANGO LA ARDHI-DKT KIJAZI.

 

Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Allan Kijazi amewataka wadaiwa sugu wa kodi ya Pango la Ardhi kulipa kodi hiyo kabla ya Serikali kuanza kuchukua hatua za kisheria kwani wale watakao endelea kukaidi agizo hilo wako hatarini kupoteza milki ya ardhi zao.

Dkt. Kijazi amesema suala la kulipa kodi ya ardhi ni la kisheria hivyo kuwataka wananchi wote kuzingatia matakwa ya kisheria kwa kulipa kodi hiyo na kuwakumbusha kuwa Serikali imetoa msamaha wa riba kwa walipa kodi sugu na mwisho wa msamaha huo ni Disemba mwaka huu.

Dkt. Kijazi amesema hayo leo tarehe 4, Novemba 2022 Jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa  kikao kazi kati ya Benki ya CRDB na wasimamizi wa kodi wa Wizara ya Ardhi kutoka mikoa yote nchini kujadili namna bora ya ushirishaji wa CRDB katika makusanyo ya kodi ya pango la Ardhi.

Katibu Mkuu Dkt. Kijazi amesema madeni ya kodi ya Ardhi ni takribani Bil.70 na kusisitiza kuwa hata kama msamaha wa riba ya kodi ya ardhi kukoma Disemba mwaka huu bado wataendelea kudai malimbikizo ya kodi ya ardhi kwa wale watakaoendelea na kumilki ardhi bila kulipa kodi.

Aidha Kiongozi huyo wa Wizara ya Ardhi amesisitiza Taasisi za Umma kuona ya haja ya kulipa kodi ya pango la ardhi kwani kwa sasa malimbikizo hayo yanazihusisha pia taasisi za umma na binafsi na uzoefu unaonesha kiwango kinachokusanywa kidogo kulinganisha na uhalisia kwa idadi ya walipa kodi.

Dkt. Kijazi pamoja na mambo mengine amesisitiza suala la elimu kwa umma kwa wananchi ili kuwajengea uelewa wa masuala ya ulipaji kodi ili waweze kushiriki kikamilifu na kuona umuhimu wa kulipa kodi ya ardhi.

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB Gerald Kamugisha amesema kimsingi Benki yake iko tayari wakati wowote kufanya kazi na Serikali katika suala la ukusanyaji kodi na tayari kuna matawi kama 50 yanayofanya kazi na Wizara ya Ardhi katika kuhakikisha miamala ya ukusanyaji kodi inafanyika kupitia matawi hayo yaliyoko Dar es Salaam na Pwani.

Kamugisha ameongeza kuwa CRDB imeendelea kukua mwaka hadi mwaka na imeongweza wigo wa huduma zake hadi nje ya Nchi kwani tayari ina matawi Burundi na inakusudia kufungua matawi yake Nchini Kongo.

Kamishna wa Ardhi Nchini Bw. Mathew Nhonge amesema Wizara ya Ardhi Pamoja na kuwa mtandao mkubwa ukusanyaji kodi ya ardhi mpaka ngazi ya Halmashauri Wizara imeona ni vyema kutumia taasisi na mitandao ya simu ili kupunguza gharama kwa walipa kodi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hiyo katika ofisi za serikali.

Kamishna Nhonge ameongeza kuwa Wizara ya ardhi pia kwa kufanya hivyo inapanua wigo wa wa ukusanyaji kodi ndio maana inaenda mbali zaidi kuboresha mtandao wa ukusanyaji kodi kwa kutumia taasisi za fedha kama Benki na mawakala wa mitandao ya simu Pamoja na Benki.   

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi katika juhudi zake za kuongeza mapato ya Serikali kupitia kodi ya Ardhi inajipanga kushirikisha taasisi za kifedha ikiwemo CRDB na baadhi ya makampuni ya simu ili kurahisisha wigo wa ukusanyaji kodi ya pango la Ardhi nchini.



November 05, 2022

MAANDALIZI KUELEKEA TAMASHA LA KIMATAIFA LA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO

 


 

Makamu wa raia wa Jamhuri ya muunganowa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Mpango anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la 41 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSuBa) lililopangwa kufanyika kwa siku tatu mfululizo Novemba 10-12,2022 kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.

 

Katika kikao cha kamati ya maandalizi kilichofanyika mjini Bagamoyo kikiongozwa na katibu mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi kufanya maandalizi ya mwishoni ikiwemo kupanga ratiba za uendeshaji wa tamasha lenyewe kwa kipindi chote cha siku tatu.

 

Katika kikao hicho katibu mkuu amesema tamasha la msimu huu ambalo litakua la 41 tangu kuanzishwa kwake litakua na washiriki wengi zaidi ikiwemo vikundi mbalimbali vya Sanaa kutoa ndani na mataifa mengine, nakuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wizara.

 

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdalla amesema hali ya usalama kwa wilaya hiyo ni swari na kwamba ulinzi utaimarishwa kipindi chote cha tamasha, akiwataka wakazi wa wilaya hiyo na maeneo jirani kujitokeza na kuwa tayari kupokea wageni kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.

 

“Mbali ya kuwa wageni watakuja kwa ajili ya Tamasha lakini pia Bagamoyo ni eneo lenye fursa mbalimbali hasa za kiutalii hivyo ni fursa kwao wageni kujionea pia wenyeji tujiandae kuwapokea”. Alisema DC Zainab.

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa wasanii wanaofanya mziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Mike Francis Mwakatundu amesema tamasha la kimataifa la Sanaa na utamaduni Bagamoyo limesaidia kutambulisha idadi kubwa ya wasanii kimataifa pia kufahamiana na wasanii wa mataifa mengine.

 

“Kwa sisi wasanii limekua linatusaidia sana kututambulisha kimataifa na kutuwezesha kukutana na wasanii wengine, mfano kwenye tamasha la msimu huu tayari tuna wasanii kutoka Burundi,Canada,India, Ufarasa na maeneo mengine tunavyo kutana hapa tunabadilishana uzoefu kwa kila msanii kwa eneo lake”.Alisema Mwakatundu


Tuesday, 1 November 2022

November 01, 2022

WACHAPWA VIBOKO 48 NA MIAKA 120 JELA

 


 Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita imewahukumu watu watatu kifungo cha miaka jela miaka 120 na kuchapwa viboko 48 kila mmoja baada ya kutiwa hatiani kwa makosa manne ya unyanganyi wa kutumia silaha.

Hata hivyo, ingawa kila mshatakiwa amehukumiwa miaka 30 jela na viboko 12 kwa kila kosa, kwa makosa manne waliyoshtakiwa nayo, kila mshatakiwa atatumikia kifungo cha miaka 30 na viboko 12, kwa makosa yote kwa kuwa vifungo hivyo vitatumikiwa vyote kwa pamoja.

Hukumu ya kesi hiyo namba 26 ya mwaka 2021 imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Samuel Maweda baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi na vielelezo vilivyotolewa na upande wa Jamhuri.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kuiba mali mbalimbali zikiwamo fedha taslimu, simu, kompyuta mpakato ‘laptop’ pamoja na kujeruhi kwa kutumia panga.

Awali wakili wa Serikali Winfrida Ernest aliieleza mahakama kuwa washtakiwa hao, Emanuel Matulanya (20) Musa Soro (20) na Philipo Lucas (18) wanashtakiwa kwa makosa manne ya unyanganyi wa kutumia silaha kinyume na kifungu namba 287 cha sheria ya adhabu.

Walipotakiwa kujitetea washtakiwa hao waliiomba mahakama kuwapunguzia adhabu kwa kuwa ni kosa la kwanza huku mshatiwa wa pili Musa Soro akiomba apunguziwe adhabau kwa kuwa ana mke na mtoto mmoja wanaomtegemea.

Friday, 19 November 2021

November 19, 2021

RC KUNENGE AKERWA NA MIGOGORO YA ARDHI


MKUU wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amekasirishwa na kuendelea kwa migogoro ya wakulima na wafugaji licha ya kuwa na sheria za kukabili migogoro hiyo hali inayofanya viongozi kutumia muda mwingi kusuluhisha na kuacha kufanya shughuli za maendeleo.

Kunenge ameyasema hayo mjini Kibaha wakati wa mkutano wa mashauriano kuhusu Mpango wa kukabiliana na migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa ardhi kwa kutumia mfumo wa ranchi ndogo kwenye mkoa huo.

Amesema migogoro hiyo iishe na ibaki historia na mkoa hauwezi kuwafumbia macho watendaji na wataalam ambao wataonekana kuwa wanashiriki kwenye migogoro hiyo ambayo imesababisha viongozi kutofanya shughuli nyingine na kubaki kusuluhisha migogoro hiyo.

Naye mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdala amesema kuwa migogoro hiyo ni kero kubwa sana ambapo wakati wanaitatua wanapigiwa simu na baadhi ya vigogo.

Abdala amesema wafugaji hao wamekuwa wakitumika na baadhi ya watu wenye uwezo ambao ndiyo wanaowakingia kifua na kusababisha wafugaji kukosa haki zao.

Kwa upande wake mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete amesema  changamoto kubwa ni wafugaji wavamizi kuingia kwenye maeneo bila ya kufuata sheria.


Monday, 15 November 2021

November 15, 2021

AMUUA BINTI YAKE BAADA YA KUKATAA KUOLEWA



Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia ndugu watatu wa familia Moja Kwa kumpiga Hadi kumuua Binti wa miaka 17 aliyejulikana Kwa jina la Mbaru Juakali mkazi wa Lufugu wilayani Uvinza Kwa kukataa kuolewa Kwa ahadi ya mahari ya Ng'ombe 13.

Akithibitisha kutokea Kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP James Manyama amesema tukio hilo limetokea Jumatano Novemba 10,2021 ambapo Binti huyo alipigwa sehemu mbalimbali za mwili wake Kwa fimbo wakimlazimisha kuolewa bila ridhaa yake.

Kamanda Manyama amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Kulwa Juakali(40),mkulima na mkazi wa Lufugu ambaye ni baba mzazi ,Shija Juakali (44), mkulima na mkazi wa Lufugu ambaye ni baba mkubwa na Majiba Juakali (29), mkulima na mkazi wa Lufugu ambaye ni baba mdogo wa Binti huyo.

Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na utakapokamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani Kwa hatua za kisheria zaidi.

Saturday, 13 November 2021

November 13, 2021

TAHADHARI DHIDI YA NYOKA KIPINDI HIKI CHA JOTO


KUTOKANA NA MAWIMBI YA JOTO NA JOTO KUBWA KWA SASA KATIKA AFRIKA MASHARIKI, NYOKA HASA CORBRA WANATAFUTA KIMBILI KATIKA MAENEO YENYE BARIDI KAMA NDANI YA NYUMBA.



VIDOKEZO VYA USALAMA

1. Epuka kuacha madirisha wazi kwa muda mrefu sana. Cobras na Mambas wanaweza kufikia urefu ambao ni wa juu sana.

2. Epuka kuacha milango yako ya mbele wazi kwa hewa safi wakati wa jioni. Watambaji hawa ni WAIZI kabisa (wametulia sana). Hutawasikia au kuwaona wakiingia ndani ya nyumba yako.

3 Kabla ya kukaa chini ya mti ambao una kivuli hicho cha baridi, angalia matawi kwamba hakuna nyoka wanaovizia kwenye matawi.

4. Angalia kitanda chako na mazingira yako kabla ya kwenda kulala, cobras wanajulikana kwa kujificha chini ya shuka.

5. Epuka mtindo wa zamani wa kupenda kutulia nje ya nyumba, ukitumia magodoro na kanga jioni. Watambaji wengi ni wa usiku (huwinda usiku na hufanya kazi vizuri zaidi)

6. Sio tu nyoka wanaweza kukuuma, lakini pia adui wa zamani wa mwanadamu; centipede (Mosithaphala), ambayo ni ya haraka na yenye sumu kali.

7. Futa vichaka kuzunguka nyumba yako. Wanavutia panya na panya ambao ni vitafunio vinavyopendwa zaidi vya mlo hatari zaidi wa nyoka.

8. Nunua unga wa kufukuza nyoka na uimimine kuzunguka uwanja wako. Hakika utapunguza uwezekano wa nyoka kutembelea nyumba yako kwa 90%.

Jihadharini na kukabiliana na nyoka wanaoingia ndani ya nyumba zenu. Baadhi ya nyoka wanaweza kuuawa kwa urahisi, wengine kama black mamba ni jogoo sana. Wakitishiwa, watakukimbiza kwa kasi ya kutisha na kukupa kuumwa mara kadhaa wakiwa bado kwenye kufukuza; na waathiriwa walioumwa wanaweza wasiishi kuona dakika arobaini zinazofuata. Kwa hivyo, kuwa mwangalifu sana unapojaribu kuua nyoka hao.

Kaa vizuri na uwe salama. Ni msimu wa nyoka. Kuna joto sana na wana shughuli nyingi na hufadhaika na kukasirika haraka sana.

Endelea kushiriki kwani unaweza kuokoa maisha.

Tafadhali uwe na siku njema!!!

Monday, 1 November 2021

November 01, 2021

WAWILI MKOANI RUVUMA WASAKWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUUA WAKE ZAO

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Pili Mande akizungumza na baadhi ya waandishi wa Habari wa mkoa huo kufuatia wanaume wawili kuua wake zao kwa wivu wa kimapenzi.

Na Amon Mtega, Ruvuma

JESHI la polisi mkoani Ruvuma linawasaka watu wawili katika matukio tofauti kwa tuhuma za kuwashambulia kwa vipigo wake zao na kuwasababishia vifo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Pili Mande amelitaja tukio la kwanza limetokea Oktoba 31 mwaka huu majira ya mchana huko katika Mtaa wa Mateka manispaa ya Songea.

Mande amesema kuwa inadaiwa kuwa Marehemu huyo ambaye jina lake limehifadhiwa kabla ya kifo chake alikuwa kwenye sherehe nyumba ya jirani yao akiwa amesimama na mwanaume mwingine kwenye sherehe hiyo na ndipo alipokutwa na mme wake ambaye naye jina limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi zaidi.

Amesema kuwa baada ya kukutwa na mume wake huyo akiwa amesimama na mwanaume mwingine alianza kumshambulia kwa kumshushia kipigo katika maeneo mbalimbali ya mwili na kumsababishia Bandama kupasuka jambo ambalo lilipelekea kuvuja kwa damu nyingi hadi kifo kutokea.

Baadhi ya waandishi wa Habari wa Mkoani Ruvuma wakimsikiliza kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Pili Mande wakati akizungumzia juu wanaume wawili kuua wake zao kwa wivu wa kimapenzi.

Kamanda  Mande alifafanua kuwa inadaiwa mtuhumiwa baada ya kumshushia kipigo mke wake na kugundua kuwa ameua alimchukua mtoto wake na kwenda kumtelekeza kwa baba yake mzazi ambaye jina lake limehifadhiwa  kisha baadae alikimbia na kutokomea kusikojulikana.

Aidha kaimu kamanda Mande amelitaja tukio la pili kuwa limetokea Oktoba 28 mwaka huu majira ya usiku huko katika kijiji cha Mageuzi Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma ambapo mwanamke mmoja ambaye jina lake halikutajwa mwenye umri wa miaka 33 inadaiwa kuwa alipigwa na shoka kichwani kutokana na mume wake kumtuhumu kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na wanaume wengine.

Alieleza kuwa wapenzi hao walikuwa wametengana lakini siku ya tukio bwana alimlaghai mpenzi wake wa kike kwa kumywesha pombe kisha kwenda nae nyumbani kwake ambako baadae alimshambulia kwa kumpiga na shoka kichwani na kumsababishia kifo.

Mtuhumiwa baada ya tukio hilo inadaiwa kuwa aliuza mahindi na maharage ambayo alipata nauli kisha alikimbia na kutokomea kusiko julikana na polisi inaendelea kumsaka.

Jeshi la polisi kutokana na matukio hayo kukithiri mkoani humo limekemea na kulaani vikali kwa mtu yeyote atakayebainika kumshambulia kwa kumpiga mke wake au mume wake atachukuliwa hatua kali za kisheria bila kujali wadhifa wake kwa kuwa mashambulio hayo yanaleta madhara makubwa kwa familia na jamii kwa ujumla na si vinginevyo.

Katika hatua myimgine kaimu kamanda Mande amesema kuwa kwa wale wanaomiliki silaha kinyume cha sheria amewataka wajisalimishe wenyewe kwenye vituo vya polisi vilivyopo jirani kuanzia Novemba mosi hadi Novemba 30 mwaka huu

Wednesday, 20 October 2021

October 20, 2021

MUME AMBAKA MKEWE HADI KIFO

 Tukio hilo la kusikitisha limetokea katika pori la Mfyome wilaya ya Iringa Vijijini mkoani Iringa ambapo mwili wa marehemu ulikutwa eneo hilo huku pembeni kukiwa na kamba ya asili ya kufungia kuni pamoja nguo zake zikiwemo nguo za ndani huku shingoni akiwa na alama za kucha.



Akizungumza na matukio daima, Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Mfyome Richard Alyoce, amesema kuwa alipata taarifa za tukio hilo majira ya saa tatu asubuhi akiwa nyumbani kwake ambapo aliongozana mara moja na mtoa taarifa mpaka eneo la tukio.

''saa tatu asubuhi nikiwa nyumbani kwangu alikuja kijana akaniambia kuna eneo fulani nilikuwa nafanya usafi wa shamba nimemuona mtu jinsia ya kike kama kalala chini, nikamuuliza unahisi atakuwa amekufa? akasema ndio nahisi ameshafariki, nikamuita mwenyekiti wa kitongoji husika maana ndio eneo lake, tukaambatana mpaka eneo la tukio na tukamkuta aliyelala pale ni mwananchi aitwaye Salome Kisayo(43) huku pembeni kukiwa na kamba pamoja na nguo zake za ndani huku maeneo ya shingo kukiwa na kucha pamoja na alama za kukabwa'' alisema Richard

Mwenyekiti amesema kuwa walitoa taarifa polisi ambapo walipofika waliuchukua mwili mpaka hospitali ya mkoa, kwa ajili ya uchunguzi zaidi na baada ya hapo walikabidhiwa kwa ajili ya kwenda kuzika. Pia ameeleza kuwa mume wa marehemu aitwaye Belatus Kindole(60)  alitoweka walipokuwa mochwari ambapo mpaka sasa hajulikani alipo na simu zake hazipatikani.

''huyu mume kwanza kabla ya mimi kupata hizi taarifa alikuja kwangu juzi jumapili akaniambia anamtafuta mkewe salome, na alikuwa na barua ya kitongoji na mimi nikamuandikia barua nyingine ili aweze kwenda vijiji vingine na polisi kutoa taarifa, lakini mpaka inafika hiyo saa tatu asubuhi siku niliyopata taarifa kuja kushuhudia hili tukio nilimpigia simu baada ya kuona ni mke wake yule aliyekuwa anamtafuta, lakini ilimchukua kama lisaa hivi kufika hapa,  tukawa tupo wote mpaka tunaenda mochwari pamoja lakini kufika kule alikaa kidogo na akaondoka , tulipojaribu kumpigia simu zake zilikuwa hazipatikani mpaka muda huu tunaozika hayupo na hatujui yupo wapi'' alisema Mwenyekiti

Hata hivyo Richard amesema kuwa chanzo cha ugomvi wa marehemu na mumewe ni wivu wa kimapenzi ambapo mume hakutaka mkewe aende hata kwa jirani kusalimia kwani wangemfundisha tabia mbaya na hivyo aliona kufanya hivyo labda kutamfanya akae kwa amani na pia walikuwa wakipelekana mpaka polisi.

Na kwa upande wake Diwani wa kata ya Kihwele Felix Waya amesema kuwa hilo ni tukio la kwanza kutokea katika eneo hilo na limewashangaza sana na amewataka wananchi kutoa taarifa kwa uongozi kama kuna jambo lolote linawakwaza hata kama ndani ya ndoa na sio kujichukulia sheria mkononi. 

Nao ndugu wa marehemu wamewashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa ushirikiano walioutoa kwenye msiba huo mpaka kumpumzisha mpendwa wao katika safari yake ya mwisho na kuwaomba waendeleze  ushirikiano huo.


Monday, 18 October 2021

October 18, 2021

MWALIMU ATIWA MBARONI KWA KUMNG'OA JINO MWALIMU MWENZAKE KWA KICHAPO

 


Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mkuyuni aliyefahamika kwa majina ya Mussa Hasira   Tarafa ya Mkuyuni Morogoro vijijini anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro  tuhuma za kumpiga hadi kumng'oa jino la juu  Mwalimu mwezake, Witnes Makoti huku chanzo kikiwa bado hakijulikani.

Kamanda wa Polisi wa Polisi Morogoro, Fortunatus Musilimu ametbibitisha kushikiliwa Kwa mtuhumiwa huku akisema kuwa tukio hilo limetokea  Oktoba 15 mwaka huu shuleni hapo ambapo alimpiga kwa kutumia Fimbo, Ngumi na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili.

Gusa link hiyo kwa ajili ya kupata burudani ya Muziki muda wote wote na Dealplus online radio
                                      https://onlineradiobox.com/tz/dealplus/?cs=tz.dealplus&p=1


October 18, 2021

MWANAFUNZI AOZESHWA KWA MAHARI YA NGURUWE MMOJA NA TSH. 330,000.

 

MKAZI wa Kitongoji cha Mabatini, wilayani Nkasi mkoani Rukwa, Kennedy Fumpa (37), amekamatwa kwa tuhuma za kumuoa mwanafunzi wa darasa la tatu baada ya kulipa mahari ya Sh. 330,000 pamoja na nguruwe mmoja. mwandishi wa matukio daima anaripoti tokea Rukwa

Mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 11 (jina linahifadhiwa), alikuwa darasa la tatu na alilazimika kuacha shule baada ya bibi yake aliyekuwa akimlea kupokea mahari hiyo hivi karibuni na mjukuu wake kuhamia kwa mwanamume huyo ili wakaanze maisha ya ndoa ya mume na mke. 

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Godfrey Kalungwizi alisema serikali ya kijiji ilipata taarifa kutoka kwa uongozi wa shule kuwa mwanafunzi huyo amekuwa mtoro shuleni kwa muda mrefu ndipo jitihada za kumtafuta zikaanza.

Alisema baada ya jitihada za uongozi wa kijiji kumtafuta mwanafunzi huyo na kumbana bibi aliyekuwa anamlea, alieleza kuwa alikwisha pokea mahari na mjukuu wake huyo tayari amekwisha olewa.

"Baada ya kufuatilia tulibaini kuwa bibi huyo alimuoza mjukuu wake kwa mahari ya Sh. 400,000, ambapo alipokea Sh. 330,000 taslimu na mnyama aina ya nguruwe mwenye thamani ya Sh. 70,000 na kukamilisha kiwango cha mahari alichopangiwa na kumchukua mwanafunzi huyo," alisema.

Naye Mwalimu Mkuu wa shule aliyokuwa akisoma mwanafunzi huyo, Josephat Joseph, alisema alikuwa haudhurii masomo na kwamba akaorodheshwa katika wanafunzi watoro wa muda mrefu mpaka uongozi wa shule ulipotoa taarifa kwenye serikali ya kijiji na kukamatwa akiwa tayari ameolewa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Peter Lijualikali, alithibitisha tukio hilo na kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo Oktoba 15 na kwamba polisi wanaendelea na uchunguzi na utakapokamilika watafikishwa mahakamani. Alisema kisichokubalika ni kumbadilisha mtoto wa kike na nguruwe hivyo sheria ya kumlinda mtoto ipo lazima ifuate mkondo wake.

Gusa link hiyo kwa ajili ya kupata burudani ya Muziki muda wote wote na Dealplus online radio
                                      https://onlineradiobox.com/tz/dealplus/?cs=tz.dealplus&p=1

Thursday, 14 October 2021

October 14, 2021

TBS YAIFUNGIA JUISI YA CERES NA KUIONDOA SOKONI KWA MADAI YA KUWA NA SUMU NDANI YAKE

 

Kutokana na juisi ya tufaa ‘Apple’ iliyotengenezwa na kampuni ya Afrika Kusini ya Ceres kudaiwa kuwa na kiwango cha juu cha sumu, Tanzania inaungana na mataifa mengine saba kuiondoa sokoni.

Akizungumza leo Oktoba 14, 2021 Mkurugenzi wa udhibiti ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Lazaro Msasalaga amesema suala hilo linafanyiwa kazi.

Amesema kila bidhaa inayoingia nchini hupimwa na hivyo ikiwa itabainika toleo hilo lipo ndani ya nchi itaondolewa haraka na utaratibu mwingine wa kuichunguza utafanyika.

“Tunalifanyia kazi, toka jana tunakusanya taarifa tuone kwamba ziliingizwa na nani kama zipo na iwapo tutazibaini utaratibu utafanyika kubaini ziliingizwa lini na nani anahusika,” amesema Msasalaga.

Amesema juisi za Ceres ni salama na hazina shida isipokuwa mtu hatakiwi kununua toleo tajwa ambapo wao ‘TBS’ wanalifuatilia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 11 na Jumuiya ya soko la pamoja la nchi za mashariki na kusini mwa Afrika (COMESA) imetaja matoleo sita yaliyotolewa kati ya Juni 14 na 30 kwa Barcode 6001240200018 (Ceres Apple 4x6x200ml).

Comesa imesema miongoni mwa maeneo ambayo yameathirika zaidi na toleo hilo ni DRC Congo, Seychellies, Zambia na Zimbabwe :Chanzo Mwananchi 

gusa link hiyo hapo chini kupata radha na burudani ya mziki wa kila aina kwa muda wote

                                           http://stream.zeno.fm/0vpamwqrg98uv


Sunday, 3 October 2021

October 03, 2021

NAFASI ZA KAZI LEO, WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA VYUO ROUND YA TATU 2021/22

🎓 PDF - TCU: WALIOCHAGULIWA 3RD ROUND VYUO ZAIDI YA KIMOJA 2021/22.


▪️TCU THIRD ROUND MULTIPLE SELECTIONS PDF File
✳ KUSHEA NI KUJALI, SHARE MAGROUP MENGINE TAFADHALI!
▪️Kama Uliomba Vyuo Vingi, Download PDF (361 Pages) Hii Ucheki Jina Lako Kirahisi Zaidi!

KU-DOWNLOAD PDF FILE, Bonyeza Hapa👇🏽
https://www.ajiraleo.com/2021/10/pdf-file-tcu-third-round-multiple.html

🇹🇿 LIVE UPDATES: CHEKI SELECTIONS ZA VYUO VYOTE 2021/22 + UPDATES MUHIMU ZA HESLB, TCU, RITA na NACTE.
Link=> https://bit.ly/3D7fFWc

🇹🇿 JESHI: NAFASI 250 MPYA ZA AJIRA MPYA SERIKALINI - JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI TANZANIA.
Link=> https://bit.ly/3AQkRvS

🇹🇿 UHAMIAJI: NAFASI 350 MPYA ZA AJIRA MPYA SERIKALINI - JESHI/IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA.
Link=> https://bit.ly/3im8tg6

🇹🇿 UHAMIAJI: NAFASI 350 MPYA ZA AJIRA MPYA SERIKALINI - JESHI/IDARA YA UHAMIAJI TANZANIA.
Link=> https://bit.ly/3AQkRvS

🇹🇿 JESHI: NAFASI 700 MPYA ZA AJIRA MPYA SERIKALINI - JESHI LA MAGEREZA TANZANIA.
Link=> https://bit.ly/3kHEyjT

KUCHEKI NAFASI NYINGINE MPYA ZA AJIRALEO, BONYEZA HAPA 👉🏽http://bit.ly/2JLrIQk

NOTE: IKIWA LINK HAIFUNGUKI/INASUMBUA, SAVE NAMBA YA ALIYEZITUMA.

🙏🏼SAIDIA WANAOTAFUTA FURSA NA AJIRA, SHARE MAGROUP MENGINE TAFADHALI!

Friday, 1 October 2021

October 01, 2021

MTOTO WA MIAKA (3) AFARIKI DUNIA KWA KUDONDOKEWA NA MATOFALI.


Mtoto mwenye umri wa miaka ( 3) aliyejulikana kwa jina la Agness Charles mkazi wa wilaya ya Meatu Mkoa Simiyu amefariki dunia baada ya kudondokewa na matofali ya nyumba yao.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Kamishna Msaidizi Richard Abwao amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa limetokea septemba 29 mwaka huu majira ya saa 2:00 usiku katika kijiji cha Mwanzangamba kata ya Mwanyahina Tarafa ya Kimali Wilayani Meatu.

Abwao amesema kuwa tukio hilo limetukia kufuatia tembo wawili kubomoa nyumba aliyolala mtoto huyo wakati wakiwa wanatafuta chakula aina ya viazi vikavu maarufu kama "michembe" baada ya kugundua kuwa ndani ya nyumba hiyo kuna chakula wanachohitaji.

Amesema mama mtoto huyo alikuwa wa kwanza kumuokoa na kumpeleka hospitali ya wilaya ya Meatu mara baada ya tembo hao kuondoka hata hivyo walikuta tayari ameshafariki.

Mwili wa marehemu umefanyiwa uchunguzi na daktari katika hospitali ya wilaya ya Meatu na kukabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu linatoa wito kwa wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya hifadhi kuendelea kuchukua tahadhari zinazotolewa na wataalam ili kudhibiti tembo kuingia vijijini.

Friday, 24 September 2021

September 24, 2021

AJALI YAUA MWANDISHI WA HABARI

 

Mwandishi wa habari wa ITV /RadioOne  mkoa wa Songwe Gabriel Kandonga amefariki dunia leo alfajiri  septemba 24,2021 kwa ajali ya gari iliyotokea maeneo ya Karasha karibu na shule ya msingi Mlowo Mbozi wakati wakielekea Mkwajuni.