DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Showing posts with label kiuchumi. Show all posts
Showing posts with label kiuchumi. Show all posts

Tuesday, 15 November 2022

November 15, 2022

TBS YAKUTANA NA WADAU WA VIWANGO KUHAMASISHA USHIRIKI KATIKA UANDAAJI VIWANGO

 Mkurugenzi wa bodi ya TBS, Dkt. Eliapenda Mariki akifungua warsha ya wadau kuhusu ushiriki katika uandaaji wa viwango iliyofanyika mapema jana Mkoani Morogoro. Baadhi ya washiriki wa warsha ya ushirikishwaji wa wadau katika uaandaji Viwango iliyofanyika mapema jana mkoani Morogoro 


**************************

Na Mwandishi Wetu, Morogoro

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) na wadau katika uandaaji wa viwango wameshauriwa kuongeza juhudi za kuoanisha viwango katika ngazi za kikanda na kushriki kikamilifu katika michakato wa kutayarisha viwango vya kimataifa ili kuziwezesha bidhaa kupenya kwenye masoko ya kimataifa.

Ushauri huo ulitolewa jana na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TBS, Dkt.Eliapenda Mariki, wakati akifungua warsha ya ushirikishwaji wa wadau katika uandaaji wa viwango nchini.

Warsha hiyo iliyofanyika mkoani Morogoro ilienda sambamba na Maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani Kwa mwaka 2022.

Dkt. Mariki alisema viwango vina mchango katika juhudi za dunia katika kufikia malengo endelevu (SDGs) kwani hutoa suluhisho halisi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Dkt. Mariki alisema mojawapo ya sababu zinazofanya bidhaa za nchi zinazoendela ikiwemo Tanzania kushindwa kupenya na kuingia kwenye masoko ya kimataifa ni kushindwa kwa bidhaa hizo kukidhi matakwa ya viwango.

"Wakati mwingine bidhaa hushindwa kuingia kwenye soko la kimataifa au la kikanda kutokana na tofauti za masuala ya matakwa ya kiwango cha bidhaa husika baina ya nchi na nchi na hatimaye" alisema Dkt. Mariki na kuongeza;

"Kwa sababu hii ni dhahiri kuwa iwapo kutakuwa na uoanishaji wa matakwa ya ubora baina ya nchi na nchi na hatimaye kuwa na viwango sawa kikanda na kimataifa, uwanja wa biashara utakuwa umesawazishwa."

Alifafanua kuwa viwango vina mchango mkubwa katika juhudi za dunia za kufikia malengo endelevu ya agenda 2030, kwani hutoa suluhisho halisi katika kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Aliipongeza TBS kwa hatua ya kuwakutanisha wadau ili kuzungumza nao kuhusiana na ushiriki katika uandaaji wa viwango.

"Hii ni hatua muhimu katika msingi wa ushiriki wenye manufaa katika uandaaji wa viwango vya kitaifa, kikanda na kimataifa kwa manufaa ya nchi," alisema Dkt. Mariki.

Madhimisho hayo yalianza kufanyika nchini kuanzia Oktoba 22, mwaka huu kwa shughuli mbalimbali za kuelimisha umma juu ya umuhimu wa kushiriki mchakato wa uandaaji viwango kitaifa, kikanda na kimataifa.

Alisema kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ilibeba ujumbe usemayo;

" Viwango kwa Maendeleo Endelevu." Kwa mujibu wa Dkt. Mariki kauli mbiu hiyo inaendana na malengo ya maendeleo endelevu ambayo yanalenga kuweka usawa kijamii, kujenga uchumi endelevu na kupunguza kasi ya mabadliko ya tabia nchi.

Monday, 3 October 2022

October 03, 2022

UNAFUU WA VIWANGO VIPYA VYA TOZO ZA MIAMALA NA BENKI.


Serikali imetangaza viwango vipya vya tozo vya miamala simu na benki zikiwa zimepita siku chache tangu iahidi kuvipunguza kutokana na malalamiko ya wananchi.
Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba, kupitia gazeti la Serikali la Septemba 30 ambalo Mwananchi imeliona imesema mabadiliko hayo yamefanywa kupitia Sheria ya Mifumo ya Malipo (Sura ya 437) chini ya kifungu cha 46A(2).
Kwa mujibu wa jedwali la marekebisho hayo, kuhamisha Sh100 hadi Sh2,999 ni Sh10, kuhamisha Sh3,000 hadi Sh3,999 ni Sh14, Sh4,000 hadi 4,999 ni Sh27, kutuma Sh5,000 hadi 6,999 ni Sh54, kutuma Sh7,000 hadi Sh9,999 ni Sh56.
Viwango vingine ni kutuma Sh10,000 hadi 14,999 ni 102, kutuma Sh15,000 hadi 19,999 ni Sh195, kutuma Sh20,000 hadi 29,999 ni Sh306, kutuma Sh30,000 hadi 39,999 ni Sh351, kutuma Sh40,000 hadi 49,999 ni Sh419, kutuma Sh50,000 hadi Sh99,999 ni Sh573, kutuma Sh100,000 hadi 199,999 ni Sh707, kutuma Sh200,000 hadi 299,999 ni Sh821.
Nyingine ni kutuma Sh300,000 hadi 399,999 ni Sh838, kutuma Sh400,000 hadi 499,999 ni Sh982, kutuma Sh500,000 hadi 599,999 ni Sh1,245, kutuma Sh600,000 hadi 699,999 ni Sh1,532.
Nyingine ni kutoka Sh700,000 hadi 799,999 ni Sh1,700, kutuma Sh800,000 hadi 899,999 ni 1,500, kutuma Sh900,000 hadi 1,000,000 ni 1,776, kutuma Sh1,000,001 hadi 3,000,000 ni Sh1,875, kutuma Sh3,000,001 na kuendelea 2,000