ASKOFU GWAJIMA AWAVUTA KITALE NA
Published Under habari
Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Ministries, Josephat Gwajima amesema Jumapili hii atatembelewa na wachekeshaji Kitale ‘Mkudesimba’ pamoja na Stan Bakora.
Gwajima amekuwa akitamka mara kadhaa kwamba anavutiwa na wachekeshaji hao ambao wamekuwa maarufu kutokana na vichesho vyao ambavyo vilikuwa vinarushwa kupitia redio ya EFM.
Jumamosi hii mchungaji huyo ambaye amekuwa akizuru katika vituo mbalimbali vya redio kutoa pole kuhusiana na tukio la RC Makonda kuvamia kituo cha Clouds Media siku chache zilizopita, ametoa taarifa ya kutembelewa kanisani kwake na wachekeshaji hao.
“Tutakuwa na ugeni wa waigizaji na wachekeshaji wawili rafiki yangu Mkude Simba (Kitale) na Stan Bakora watapata nafasi ya kuperform live pia, kwa niaba ya familia ya Ufufuo na Uzima tunawakaribisha. Ufufuo na uzima tunasapoti vipawa mbalimbali ambavyo watu wamepewa na Mungu,” aliandika Gwajima Instagram.
Askofu huyo amekuwa gumzo katika mitandao ya kijamii hivi karibuni baada ya kutajwa kwenye sakata la dawa za kulevya na RC Makonda.
No comments:
Post a Comment