FAHAMU KUHUSU HISTORIA MPIRA WA MIGUU (Soka)
LEO TUANGAZIE KUHUSU HISTORIA YA MPIRA WA MIGUU
UTANGULIZI MAANA YA SOKA.
Mashirikisho tofauti Ya Kandanda Duniani (pichani)
Mpira wa miguu (pia soka au kandanda) ni mchezo unaochezwa na jumla ya wachezaji ishirini na wawili katika timu mbili husika, kila timu ikiwa na wachezaji kumi na mmoja.
Lengo hasa la mchezo huu ni wachezaji kuonyesha uwezo wao wa kuumiliki mpira kwa kutumia miguu na kuuingiza mpira katika wavu wa timu pinzani mara nyingi zaidi.
Matumizi ya mikono ni marufuku isipokuwa kwa mlinda mlango (golikipa) katika eneo maalumu na wakati wa kurudisha mpira baada ya ya kutoka nje ya uwanja.
HISTORIA YA MPIRA WA MIGUU
Mfano wa Mchoro unaoonyesha Mchezaji wa mpira wa miguu, Ugiriki Ya Kale.(karne ya 18-19)
Michezo mbalimbali ya kuchezea mpira inaweza kupatikana katika kila uwanja wa jiografia na historia, Wachina, Wajapani, Wakorea na Waitalia wote walikuwa wakicheza mpira zamani kabla ya enzi zetu.
Wagriki na Waromania walitumia michezo hiyo kuwaandaa wapiganaji kabla ya vita. Hata hivyo, ni nchini Uingereza pekee ambapo umbo la soka la kisasa lilianza kuibuka.
Kuibuliwa kwake kulilianza wakati mashirikisho mawili (Shirikisho la Mpira wa miguu na Mpira wa Ragbi) yalitawanyika, ambapo Shirikisho la kwanza la soka lilibakia nchini Uingereza.
Mnamo Oktoba-1963, Vilabu-11 vya London vilituma wawakilishi katika mkutano wa (Freemason) ili kujadili na kuweka kanuni zilizokubalika kusimamia mechi zilizochezwa kati yao. Mkutano huo ulipelekea kuanzishwa kwa Shirikisho la Kandanda lililoitwa ‘Football Association’
Miongoni mwa kanuni zilizowekwa ni zile za kukataa utumiaji wa mikono kushika mpira na kunyanganya kwa nguvu kama ilivyo kwa mchezo wa ragbi. Hapo ndio mwanzo wa Ragbi kugawanyika na mchezo wa soka.
Miaka minane baada ya kuanzishwa, Shirikisho la Kandanda (FA) lilikuwa na wanachama 50. Shindano la kwanza la kandanda lilianza mwaka huo. Kombe la FA- ambalo lilifuatiwa na lile la Ligi ya Ubingwa miaka 17 baadaye.
Wachezaji wawili wa Kilabu ya Darwin, John Dove na Fergus Suter walikuwa wa kwanza kulipwa kwa mchezo wao. Kitendo hiki kilikuwa mwanzo wa soka ya kulipwa iliyohalalishwa mnamo mwaka wa 1885.
Mwamko huu ulipelekea kuanzishwa kwa Mashirikisho ya kitaifa nje ya Uingereza (Great Britain). Baada ya Shirikisho la Kandanda la Uingereza, Mashirikisho yaliyofuatia ni ya Uskoti (1873), Wales (1875) na Eire (1880).
Kutokana na ushawishi mkuu wa Uingereza katika mataifa ya Dunia, Soka ilizambaa kote duniani. Mataifa mengine yalianzisha Mashirikisho ya Kandanda kufikia 1904 wakati Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) lilipoanzishwa.
Tokea hapo mwanzo, kandanda ya kimataifa imekuwa ikikua licha ya vikwazo mbalimbali. Kufikia 1912, FIFA ilikuwa na uanachama wa mashirikisho 21, idadi iliyoongezeka na kufikia 36 kwa mwaka 1925.
Mnamo mwaka1930, kwa mara ya kwanza katika historia ya soka yalifanyika mashindano ya Kombe La Dunia (FIFA) ambapo ilikuwa na wanachama wapatao-41. Na mshindi wa jumla kwa mwaka huo wa kwanza alikuwa ni (URUGUAY) baada ya fainali kufanyikia nchini humo, na nchi ya Uruguay iliifunga timu ya Argentina mabao 4-2. (pichani chini)
SHIRIKISHO LA KANDANDA DUNIANI (FIFA).
Shirikisho la kandanda Duniani (FIFA) ndilo shirikisho kuu linalosimamia Kandanda duniani (kwa nchi wanachama). Wanachama wake ni mashirikisho ya kandanda ya nchi mbalimbali, ambapo hadi kufikia mwaka wa 2000, FIFA ilikuwa na wanachama wapatao 204 kutoka pembe zote za dunia.
Shirikisho hili huandaa mashindano yote makuu duniani yahusuyo soka la kimataifa. (michuano mikuu hufanyika kila baada ya miaka-4)
Uwanja wa Cape-Town Stadium uliotumika kwa Fainali za FIFA Barani Afrika kwa mara ya kwanza (Nchini Afrika Kusini-2010)
HISTORIA ya kombe la dunia iliandikwa kwa mara ya kwanza mwaka 1928 wakati Rais wa FIFA wakati huo, Jules Rimet alipoamua kuandaa michuano mikubwa zaidi duniani iliyohusisha mataifa mbalimbali, na Ufunguzi wa michuano hiyo ukafanyika miaka miwili baadaye mnamo mwaka-1930 nchini Uruguay na timu-13 zilialikwa kushiriki michuano hiyo.
Kuanzia hapo, FIFA ilifanikiwa kubadilisha miundo na mifumo mbalimbali ya michuano tofauti, ambayo imepelekea kuanzishwa kwa soka la kisasa zaidi.
Timu 32 zinapatikana baada ya mchakato wa mechi zakufuzu ambazo zinashirikisha timu kutoka mataifa 200 duniani kote.
Kabla ya kombe la dunia Mechi ya kwanza ya kimataifa ya soka duniani ilichezwa mwaka 1872 kati ya England dhidi ya Scotland ingawa katika kipindi hicho ilikuwa ni mara chache kwa mchezo wa soka kuchezwa nje ya Uingereza.
Hata hivyo, kuanzia mwaka 1900 mchezo wa soka ulipata umaarufu duniani kote na vyama vingi vya soka vikaanzishwa. Mechi ya kwanza rasmi ya kimataifa kuchezwa nje ya Uingereza ilikuwa kati ya Ufaransa na Ubelgiji ambayo ilichezwa Paris,Mei 1904.
Mchezo huo ulisababisha kuanzishwa kwa Shirikisho la soka duniani (FIFA) Mei 22, 1904.
Itaendelea.........
No comments:
Post a Comment