Ukimfaham Makonda Hutaacha Kumpenda. Hata Wapinzani Wake Mkimpata Mtampenda Sana...!!!
Huyu Ndugu Makonda. Ni vile wengi hawamfaham. Kama akiwa rafiki yako, akiwa chini yako hutaacha kumpenda. Ni mtu ambaye unapompa maelekezo anasikiliza. Anafanya kwa namna ambayo unataka iwe.
Bwana makonda ni mtu ambaye kama amelala ukamwamsha kuwa tukachote maji ndoo mbili mbili atakuuliza kwa nini tusichote nne? Au ukichota mbili ukapumzika yeye ataendelea kuchota zaidi. Kwa nini usimpende. Ni aina ya mtu ambaye when you tell him. Jump! He will ask "how high? Kwa unyenyekevu kabisa. Ukimwambia akimbie mita 100 atakimbia 1000.
Ungemuuliza Marehem Sitah angekwambia. Ungemuuliza Riziwan angekwambia kuwa This man ni mtiifu sana. Ni msikivu unapompa maelekezo hufuata bila kusita, bila kuuliza uliza. Ni kwa nini usimpende?
Akiwa rafiki yako. Ikatokea ukamfahamisha kwa baba yako. Atamheshimu baba yako, atampenda na kumjali.wakat wewe hupigi simu mpaka uwe na shida. Yeye atapiga simu na kumuuliza " mzee habari za asubuh?umeaamkaje hajambo na mama? Haya mi nlikuwa nawasilimia tu. Mungu awabariki" kwa nini mzee wako asimpende? Asitaman awe mtoto wake?
Jamaa anachapa kazi. Akipewa kazi anafanya hasa. Ni aina ya watu ambao husemwa "amesifiwa kukimbia kapitiliza hadi kwao" anafanya kazi kwa kujituma sana.
Sasa mtu wa hivi kwa nini asipendwe?kwa nini asiaminiwe?ni mwaminifu na mtiifu. Haulizi maswali. Anasema hewala baba ntafanya. Vijana wengine wanahoji. Wanasema hili haliwezekani. Wakati yeye haamini kama kuna jambo ataambiwa haliwezekani.kwa nini asipendwe?
Kila chama ili kisimame kinahitaji akina yeye. Hawa ni watu wa muhimu sana katika ujenz wa chama na hata serikalini. Hutumika na watawala sehemu yoyote il duniani wanakuwepo. Hawa hutenda kwa uaminifu yale watawala wanayotaka yatokee.ni waaminifu sana. Adolf hitler alikuwa nao, idd amini alikuwa nao, bokassa alikuwa nao, djamen alikuwa nao, nyerere alikuwa nao, mandela alikuwa nao. Kila kiongozi anakuwa nao. Ni watu muhimu sana kushikilia itikadi.
Ni vile hamjamfaham makonda mkimfaham hata ninyi mtampenda. Mtatamani kumsajili awe kwenu. Trust me kama ingekuwa kunafanyika usajili basi angekuwa anagombaniwa kwa dau kubwa sana.
Hayo ni maoni ya mmoja wa wasomaji wetu
No comments:
Post a Comment