DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Monday, 27 March 2017

RAISI MAGUFULI ATOA AGIZO JUU YA MSANII NEY WA MITEGO AAGIZA ACHIWE HURU

Breaking News..Rais Magufuli Aagiza Nay wa Mitego Aaachiliwe,Ataka Pia Wimbo Wake Uendelee Kuchezwa Kwenye Radio Station Kama Kawa,Ampa Masharti Haya


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumuachia huru Rapa Emmanue Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya kukamatwa juzi wilayani Mvomero mkoani Morogoro kisha kusafirishwa jana kupelekwa katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam kwa kile kilichoelezwa kuwa wimbo wake wa WAPO alioutoa hivi karibuni hauna maadili na una maneno ya kichochezi.

Akitoa agizo la Rais Magufuli, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe amesema kuwa Rais Magufuli ametaka Nay aachiwe huru na wimbo wake aufanyie maboresho kwa kuongelea pia kuhusu wauza madawa ya kulevya na wakwepa kodi kisha uendelee kupigwa kwenye vyombo vya habari.

Aidha amesema kuwa, mara tu atakapoachiwa huru, Nay anapaswa kuonana na Waziri Mwakyembe ili ampe maelekezo yaliyotolewa na Rais Magufuli kuhusu wimbo huo.

No comments: