Ndoa ya Nuh Mziwanda Kufungwa Upya
Ni siku moja tu imepita tangu staa wa Bongo Fleva Nuh Mziwanda kupitia account ya Instagram kupost picha ya mtoto wake aliyebarikiwa katika ndoa yake, inadaiwa ndoa hiyo kuingia katika mvutano.
Inasemekana kuwa ndugu wa Nuh Mziwanda hawakuridhia ndoa ya ndugu yao iliyofungwa miezi kadhaa iliyopita kwa kuwa Nuh alibadili dini kufuata dini ya mke wake ambapo kupitia U-heard ya XXL ya Clouds FM April 28 2017 mtangazaji Soudy Brown ameinasa sauti ya mke wa Nuh Mziwanda akimzungumza mama mkwe wake:
“Nilimwambia mama unachelewa, mwambie aniache. Na anajua kuwa mimi sijaolewa na mwanawe, ila anajua nimezaa tu na mwanawe. Kwenye sherehe ya harusi hakuwepo, alikuwa kwenye msiba. Yule mama ni mzee wa Kanisa, alikuwa anataka niende kanisani nibadili dini ndio niolewe.” – Mama ANYA
No comments:
Post a Comment