DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Monday, 19 June 2017

TIBA YA TATIZO LA HARUFU MBAYA KINYWANI

Harufu mbaya mdomoni inaweza kuwa kero kwako au kwa wengine, ila inakupunguzia kujiamini kwani kila wakati utahisi watu wanasikia harufu yako ya mdomo. Lakini tatizo hili linatibika kirahisi sana kwa wataalamu wengi wamekwisha lifanyia uchunguzi. Lakini tatizo hili linatibiwa na Juisi hii kirahisi.

#MANDALIZI NA UTENGENEZAJI
chukua Asali kijiko 1 cha chakula
chukua na Mdalasini wa india kijiko1 cha chakula
changanya vyote kwa pamoja Ratio ikiwa sawa na uuache mchanganyiko wako kwa mda kama nusu saa hivi sio mbaya kama ikizidi

Au
Changanya mdalasini wa india na asali moja kwa moja kwenye lita moja na uwe unatumia kila uamkapo asubuhi na kabla ya kulala vijiko vitatu.

NB: ijapokuwa hii ndio tiba bora kabisa kwa ugonjwa huo ila tiba zingine ni kama vile, kunywa maji mengi sana, Kuswaki mara kwa mara, kula kifungua kinywa chenye afya, kutumia bazoka

NB: Asali ya nyuki wadogo ni bora zaidi kuliko nyuki wakubwa

Pia kuna njia nyingine kama vile kunywa maji mengi zaidi ya lita mbili kwa siku na kuepuka ulaji mfululizo.
Vilevile unaweza kutumia kokwa la parachichi katika kutibu tatizo la harufu mbaya mdomoni. Kokwa la parachichi(avocado) halitibu matatizo ya meno pekee bali hutibu pia na tatizo la harufu mbaya kinywani.
Njia uandaaji na matumizi kama yaleyale ya kuondoa tatizo la meno.ila kwa faida ya wale ambao hawakubahatika kusoma chapisho lililopita la NJIA RAHISI YA KUTIBU TATIZO LA MENO BILA KUNG'OA  nitaelezea kwa faida yao.

JINSI YA KUANDAA HILO KOKWA KUPATA DAWA.

chukua kokwa la parachichi likatekate katika vipande vidogovidogo kisha vianike juani kwa siku kadhaa hadi vikauke 
Kisha visagesage na kupata unga Wa hilo kokwa

            MATUMIZI

Chukua maji ya moto bilauli moja kisha changanya na unga Wa hilo kokwa kijiko kimoja cha chai kisha funika hadi maji yapoe na kuwa ya uvuguvugu.

Baada ya hayo maji kupoa piga pafu moja sukutua kwa muda Wa kama dakika mbili  kisha tema na piga pafu jingine na usukutue tena na baada ya dakika kama tatu tema tens.Fanya hivi Mara tatu (yaani pafu tatu) asubuhi kabla hujapiga mswaki na jiaoni pia kabla ya kulala.

Fanya hivyo kwa siku 5-8 mfululizo na baada ya hapo tatizo lako la harufu mbaya mdomoni litakuwa limeisha sambamba na matatizo ya meno.

No comments: