Rayvanny azitaja kolabo zake zilizokuwa tayari
Msanii Rayvanny ametaja kolabo zake na wasanii wa nje ambazo zipo tayari.
Muimbaji huyo, ambaye yupo nchini Sweden kwa ziara yake ya muziki, amemuambia mmoja wa watangazaji wa nchi hiyo kua, tayari ameshafanya kolabo na msanii mkubwa kutoka Nigeria, Afrika Kusini na Kenya.
“Nina kolabo na msanii mkubwa kutoka Nigeria, ingawa kwa sasa siwezi kutaja jina lake. Lakini pia kuna kolabo Afrika Kusini, na Kenya ukiacha Bahati, kuna mwingine Khaligraph Jones kutoka Nairobi,” amesema Ray.
Kwa msanii wa Afrika Kusini tayari muimbaji huyo kutoka WCB ameshafanya kolabo na Dj Maphorisa tangu mwezi Disemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment