DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Friday 23 June 2017

MADHARA YA ULAJI WA CHIPS

Chips Kwa kiswahili fahasa hufahamika kama vibanzi lakini kwa jina maarufu ni chips. Hiki ni chakula ambacho hupendwa na watu wengi sana hasa pale unapotaka kupata chakula cha haraka na cha bei nafuu basi mawazo yako yatawaza vibanzi.
Chips au vibanzi licha ya kuwa hupikwa kwa vianzi ambavyo vina kiwango kikubwa cha sukari, lakini pia hupikwa kwa kutumia mafuta mengi na hivyo kufanya mafuta yanayoingia mwilini kusababisha matatizo mbalimbali.
Hatari kubwa ipo kwa watu wanaokula chips mara kwa mara lakini hawafanyi mazoezi kwani wanakuwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo. Ukifanya mazoezi mara kwa mara yanasaidia kuyeyusha mafuta ndani ya mwili wako na hivyo kukuondoa katika hatari hiyo.
Vijana wengi sasa wanaugua magonjwa mbalimbali yanayotokana na mafuta kukusanyika kwenye miili yao ambayo kwa kiasi kikubwa huchangiwa na kutokufanya mazoezi.
Mbali na vyakula kama chipsi kusababisha magonjwa ya moyo, lakini pia hupelekea mtu kuwa mnene na kuwa na uzito mkubwa ambao mwisho wa siku husababisha magonjwa kama shinikizo la damu, magonjwa ya Kwa kiswahili fahasa hufahamika kama vibanzi lakini kwa jina maarufu ni chips. Hiki ni chakula ambacho hupendwa na watu wengi sana hasa pale unapotaka kupata chakula cha haraka na cha bei nafuu basi mawazo yako yatawaza vibanzi.
Chips au vibanzi licha ya kuwa hupikwa kwa vianzi ambavyo vina kiwango kikubwa cha sukari, lakini pia hupikwa kwa kutumia mafuta mengi na hivyo kufanya mafuta yanayoingia mwilini kusababisha matatizo mbalimbali.
Hatari kubwa ipo kwa watu wanaokula chips mara kwa mara lakini hawafanyi mazoezi kwani wanakuwa katika hatari kubwa ya kupata magonjwa ya moyo. Ukifanya mazoezi mara kwa mara yanasaidia kuyeyusha mafuta ndani ya mwili wako na hivyo kukuondoa katika hatari hiyo.
Vijana wengi sasa wanaugua magonjwa mbalimbali yanayotokana na mafuta kukusanyika kwenye miili yao ambayo kwa kiasi kikubwa huchangiwa na kutokufanya mazoezi.
Mbali na vyakula kama chipsi kusababisha magonjwa ya moyo, lakini pia hupelekea mtu kuwa mnene na kuwa na uzito mkubwa ambao mwisho wa siku husababisha magonjwa kama shinikizo la damu, magonjwa ya miguu, figo, moyo, shinikizo la damu, kisukari na saratani za aina zote.
Imeelezwa kuwa, sahani moja ya chipsi kavu huwa na mafuta yanayokaribia nusu kikombe cha chai ambayo ni sawa na ujazo wa mililita 250.
Hayo yalisemwa jana na Mtaalamu wa Masuala ya Chakula na Lishe wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Ulumbi Kilimba, alipokuwa akizungumza na gazeti hili ambapo alisema walaji wengi wa chipsi wapo katika hatari ya kutengeneza sumu kwenye miili yao bila kujua.
“Chipsi ni chakula hatari, sahani moja ya chips kavu ina mafuta ujazo wa mililita 250, na kwa jinsi ilivyo watu wengi hupendelea kula chipsi mayai, kuku, soseji au hata kwa mishikaki maana yake ni kwamba kiwango hicho cha mafuta huzidi kwa sababu na vyenyewe huwa vimekaangwa,” alisema.
Alisema jambo la kusikitisha ni kwamba wafanyabiashara wengi wamekuwa hawazingatii umuhimu wa kutumia mafuta mara moja katika kukaanga vitu hivyo.
“Kwa hali halisi jinsi ilivyo huko mitaani wafanyabiashara huwa wanapikia mafuta kwa zaidi ya mara mbili na hivyo kuzidisha hatari zaidi.
“Wanazidisha hatari kwa sababu… kawaida mafuta yanapaswa kupikiwa mara moja. Kadri unavyounguza mafuta ndivyo ambavyo ule mfumo wa mafuta masafi ambayo yanatakiwa kwa mwili wa mwanadamu unabadilika na kuwa machafu, maana yake ni kwamba unapopikia mafuta zaidi ya mara mbili tayari yanakuwa yametengeneza sumu ambayo haitakiwi mwilini,” alisema.
Mtaalamu huyo alisema mafuta ambayo yanakuwa yametumika kukaangia vyakula zaidi ya mara mbili hubadilika na kutengeneza utando mweupe ambao huweza kuonekana iwapo mtu atayatazama kwa macho yake.

“Ule utando mweupe utakaouona unatoa ishara kwamba mafuta hayo hayafai kwa matumizi ya binadamu, lakini watu wanataka kufanya biashara hivyo huendelea kuyatumia bila kujali au pengine kutokujua kwamba wanaziweka afya za walaji katika hatari ya kupata magonjwa hayo,” alisema.
Ulumbi alisema pamoja na kiwango hicho cha mafuta ambacho huingia mwili kwa ulaji wa sahani moja pekee ya chipsi kavu, mlaji hula chumvi nyingi iliyopo ndani ya nyanya maalumu iliyosagwa (tomato).

“Ile ‘tomato sauce’ jinsi ilivyotengenezwa ina chumvi nyingi, sasa umekula mafuta mengi jumlisha na hiyo chumvi nyingi na ninavyofahamu walaji wengi wa chipsi hupendelea kushushia na kinywaji chenye sukari nyingi maana yake unakuwa umetengeneza sumu ndani ya mwili wako kwa mara moja,” alisema.
Alisema takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wagonjwa wanaougua magonjwa yasiyokuwa ya kuambukiza nchini inaongezeka, hata hivyo hali hiyo inaweza kuepukwa iwapo watu watazingatia ulaji unaofaa.
“Wengi hatuzingatii ulaji wa chakula bora, tunakula mradi tule na hatuzingatii kupima afya zetu hili ni tatizo. Wakati umefika tubadilike kwa sababu wagonjwa wanaongezeka,” alisema.
Mtaalamu huyo wa lishe, alisema utafiti uliowahi kufanyika nchini hivi karibuni unaonesha kuwa kati ya watu 100 wenye umri wa kati ya miaka 25 na kuendelea tisa kati yao tayari wanaugua ugonjwa wa kisukari huku wawili wakiwa hawajijui kuwa wana maradhi hayo.
“Kila mwaka duniani watu milioni 12 hugundulika kuwa wana saratani na asilimia 60 ya magonjwa ya saratani yanasababishwa na mfumo mbovu wa maisha hasa ulaji usiofaa.
“Wenzetu wazungu ni wajanja si kwamba hawali chipsi, wanakula lakini wanazingatia ‘menu’ ya sahani yao, kwamba inakuwa na viazi kidogo, mboga mboga nyingi lakini sisi kwetu ni kinyume watu wanapenda tomato kwa wingi,” alisema.
Alisema ulaji wa mbogamboga ni jambo la msingi kwani huenda kusaidia kurahisisha mfumo wa umeng’enywaji wa chakula tumboni.