DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Sunday, 30 July 2017

DALILI ZA HOMA YA INI NA NJIA ZA UENEAJI

Homa ya Ini ni ugonjwa unaoambukizwa kwa njia ya virusi ambavyo vikishaingia mwilini hushambulia ini kabla ya kugeuka maradhi sugu.Virusi hivyo vinaitwa HBV (Hepatitis B Virus).
Virusi hivyo husambazwa kwa njia ya damu au majimaji mengine ya mwilini, mfano mate au jasho. Watu takriban 1,000,000 wanapoteza maisha duniani kote kutokana na ugonjwa wa Homa ya Ini (Hepatitis B).
Ugonjwa huu kama haujatibiwa hutengeneza uvimbe katika ini na kusababisha kansa ya ini na baadaye Kifo.
JINSI UNAVYOAMBUKIZWA:
Katika maeneo hatari zaidi duniani, Virusi vya Hepatitis B (HBV) kwa kawaida husambazwa kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakati wa kuzaliwa au kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine hususan nyakati za utotoni.
Kama ilivyo kwa Ukimwi, Virusi vya Homa ya Ini pia huambukizwa kwa njia ya kujamiiana, mate, jasho na mwingiliano wowote ule wa damu.
Njia kuu za maambukizi :
-Kujamiana bila kinga
-Kunyonyana ndimi 'denda'
-Mama mwenye ugonjwa kumwambukiza mtoto wakati wa kujifungua
-Kuchangia damu isiyo salama
-Kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kuchangia miswaki
-kuchangia taulo na mwenye ugonjwa huo
-kubadilishana nguo au kukumbatiana wakati mkiwa mnavuja jasho.
Tafiti za kitaalamu zinaonesha kuwa virusi hivyo ni hatari kuliko hata vya Ukimwi kwa sababu vinaweza kuishi nje ya mwili wa binadamu (yaani nje ya mfumo wa damu) kwa siku saba. Virusi vya Ukimwi (VVU) havina uwezo wa kuishi nje ya mfumo wa damu hata kwa dakika moja.
Kutokana na usugu wa HBV, maana yake ni kwamba kama kirusi kipo kwenye ngozi, kitaendelea kuwa hai kwa siku saba na katika kipindi hicho mtu anaweza kuambukizwa kwa njia ya damu au jasho.
Kwa wastani kirusi cha HBV kikishaingia mwilini, hupevuka ndani ya siku 75, hata hivyo upo uwezekano wa kupevuka kati ya siku 30 hadi 180. Ndani ya siku 30 mpaka 60, mtu mwenye HBV anaweza kugundulika ikiwa atapimwa.
Mtu mwenye Homa ya Ini ana wastani mdogo wa kuishi kuliko mwenye Ukimwi. Kwa maana hiyo, mwenye maambukizi ya Virusi vya Homa ya Ini hufariki dunia haraka kuliko mwenye VVU.
DALILI ZA UGONJWA HUU:
Watu wengi hawaonyeshi dalili yoyote. Kwa maana hiyo mtu anaweza kuishi na HBV na kusababisha maambukizi kwa wengine bila kugundulika.
Hata hivyo, watu wengine husumbuliwa na homa kali na dalili ambazo hudumu kwa wiki kadhaa. Dalili hizo ni:
-Uchovu
-Kichefuchefu
-Mwili kuwa dhaifu
-Homa kali
-Kupoteza hamu ya kula
-Kupungua uzito
-Maumivu makali ya tumbo upande wa ini
-Macho na ngozi kuwa vya njano
-Mkojo mweusi
Kwa wagonjwa wengine, Virusi vya Hepatitis B hukua hadi kusababisha ini kuharibika kabisa (cirrhosis of the liver) au saratani ya ini (liver cancer).
UGONJWA HUU HAUNA TIBA:
Mpaka sasa Homa ya Ini haina tiba, vilevile hakuna dawa maalum za kurefusha maisha. Ugonjwa huo ukishafikia kiwango cha ini kuharibika au kupata saratani ya ini, maana yake kinachofuata ni kifo.
KINGA:
-Chanjo
-Kutumia kinga wakati wa kujamiana
-Kuacha kuchangia vitu vya ncha kali kama sindano, wembe n.k
-Kutochangia miswaki
-Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu
-Kutochangia damu isiyo salama
KUNDI LIPI NI HATARI ZAIDI?
Asilimia 80-90 ya watoto wachanga ambao huambukizwa katika kipindi cha mwaka wa kwanza tangu kuzaliwa, Homa ya Ini hukua mpaka kufikia kuwa sugu na hatimaye kifo.
Asilimia 30-50 ambao huambukizwa kabla ya kufikisha umri wa miaka sita, Hepatitis B hukua mpaka kuwa sugu na baadaye ni kifo.
Asilimia 90 ya watu wazima wanaopata HBV, virusi hivyo hutoweka ndani ya miezi sita. Yaani uimara wa ini husababisha virusi hivyo kupotea.
Asilimia tano kushuka chini ya watu wazima wanaopata maambukizi ya HBV, virusi hivyo vya Hepatitis B kugeuka sugu na hatimaye kifo.
Asilimia 15-25 ya watu wazima ambao walipata maambukizi utotoni na hatimaye Hepatitis B kuwa sugu, hufariki dunia kutokana na matokeo ya ini kuharibika kabisa au kwa saratani ya ini.
TANZANIA IPO KUNDI HATARISHI
Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), Kusini ya Jangwa la Sahara ndiyo eneo hatari zaidi. Tanzania ni moja ya nchi zilizopo katika eneo hilo. Kiwango cha hatari Kusini ya Jangwa la Sahara kinalingana na kile cha Mashariki ya Bara la Asia.
Ripoti hiyo inaonesha kuwa watu wengi walipata maambukizi nyakati za utotoni na kwamba kati ya asilimia tano mpaka 10 ni waathirika sugu.