DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Thursday 27 July 2017

DALILI ZA UPUNGUFU WA DAMU MWILINI




Upungufu wa damu ni tatizo linalosababishwa na kupoteza damu nyingi, kupungua kwa uzalishaji wa chembe hai za da damu na uharibifu wa chembe za damu kutokana na matatizo na magonjwa mbali mbali seli mundu, ujauzito, hedhi nzito, kurithi, magonjwa sugu na Lishe duni yenye ukosefu wa madini ya folic, chuma na vitamini B12.

Dalili zifuatazo zinakuwezesha kutambua kama una tatizo la upungufu wa damu hivyo kukusaidia kuwahi hospitali au kubadili mfumo wa chakula ili kuepuka madhara makubwa ya baadae.

Kushindwa kupumua vizuri
Vidonda kwenye ulimi au mdomoni
Sehemu nyeupe ya jcho kuwa bluu
Ngozi kuwa na rangi ya kijivu
Kucha kuwa dhaifu
Kusikia hasira na kuhamasika haraka
Kuchoka sana kuliko kawaida
Maumivu makali ya kichwa
Kupungua kwa uwezo wa kufikiria
Kusikia kichwa chepesi pale unaposimama
Miguu na mikono kuwa ya baridi sana
Uchovu wa mara kwa mara

MATIBABU
Upungufu wa damu hutibiwa mapema kwa kubadili lishe pamoja na kuongeza lishe yenye vitamini C na B12 pamoja na madini ya Chuma kutokana na visababishi vya tatizo. Mara nyingine vidonge na sindano zenye lishe hizi huweza kutumika hosipitali ambamba na matibabu ya tatizo linalosababisha na iwapo mgonjwa yuko katika hali mahututi huweza kuongezewa damu.

Usisahau kugusa hapa 
https://m.youtube.com/channel/UCE_uPKWhk-R-pLqPWFYdCEA/sounddream?sub_confirmation=1