Mhindi ni zao maarufu kwa chakula hasa nchi za Africa mashariki na maeneo mengine. Imezoeleka kuwa katika mmea wa mhindi lile zao yaani mahindi yenyewe ndo yana manufaa kwa matumizi ya binadamu ukiondoa majani ambayo hutumiwa kulishia wanyama.
Leo ningependa kukushirikisha msomaji wangu wa Mdukuzi blog katika kuyafahamu magonjwa ambayo hutibiwa kwa kutumia mmea wa mhindi. "Nadhani mnakumbuka kile kitendawili cha utotoni kuwa Babu kalala ndani ndevu ziko nje" sasa hizo ndevu kama inavyooneka katika picha hapo juu huponya magonjwa kadhaa ambayo huwakera sana watu katika jamii tunayoishi. Magonjwa hayo ni kama ilivyoorodheshwa
1:Ugonjwa wa Figo.
2:Ugonjwa wa kibofu.
3:Ugonjwa wa kukojoa kitandani
4:Matatizo ya njia ya mkojo.
Matumizi.
Chukua ndevu za kutosha (nyingi) za mahindi machanga chemsha ndani ya maji Lita moja hadi mbili kisha Chuja na utumie glass mbili kwa Siku kwa muda wa siku 5-8 na hapo tatizo lako litakua limeisha kama sio kupungua makali.
Pia unaweza kuziloweka hizo ndevu kwenye maji kwa muda wa dakika 15-20 kisha ukatumia kama ilivyoelekezwa hapo juu.