DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Friday 7 July 2017

SABABU KUU ZA MAUMIVU WAKATI WA TENDO LA NDOA.

Ni kawaida kwa wanawake kuhisi maumivu wakati wa kujamiiana. Katika matukio mengi hali kama hizo, hutokana na mwanamke kutolainika sawasawa, hali hii inaweza kutatuliwa kwa urahisi kwa kuongeza muda wa kumchezea mwanamke(foreplay) au kutumia vilainishi vya ziada. Hata hivyo, iwapo maumivu hayakuweza kupungua.
hizi hapa  ni baadhi ya sababu, ambazo husababisha maumivu wakati wa tendo la ndoa:

Kukakamaa kwa misuli ya uke (Vaginismus): hali hii inasababishwa  na mkazo katika misuli ya uke inayotakana na hofu ya maumivu au majeraha.

Matatizo ya shingo ya kizazi: Wakati mwingine uume unaweza kuingia ndani zaidi hivyo kugusa shingo ya kizazi. Iwapo mwanamke ana maambukizi huisi maumivu mara shingo ya kizazi inapogusana na uume.

Matatizo katika mfuko wa uzazi: Matatizo kama fibroids yanaweza pia kuwa sababu ya maumivu wakati wa ngono.
Maambukizi ya uke: aina yoyote ya maambukizi ya uke kama vile maambukizi ya fangasi inaweza kusababisha maumivu wakati wa kujamiiana.

Kuumia uke: majeraha kutokana na sababu kadhaa mfano kuchanika wakati wa kujifungua au kuongeza njia katika msamba wakati wa kujifungua.

Endometriosis: Hii ni hali ambayo inasababisha tishu za
mji wa mimba kukua nje ya mfuko wa uzazi, na hivyo kuchochea maumivu wakati wa kukutana kimwili.

Maambukizi kwenye funga nyonga(PID): Viungo kwenye nyonga vinaweza kupata maambukizi hivyo kusababisha
maumivu wakati wa ngono.

Matatizo ya ovari: Matatizo haya ni pamoja na uvimbe kwenye mfuko wa mayai (ovarian cyst) wanakuwa waliokoma siku(Menapause): Wakati wanapokuwa wamekoma siku zao maumbile yao yanasinyaa na kuwa kavu, hivyo kuchochea maumivu wakati wa tendo la ndoa

Magonjwa ya zinaa: magonjwa ya zinaa kama malengelenge (herpes), masundosundo n.k, yanaweza kusababisha maumivu wakati wa ngono.

Ukosefu wa ute ute sehemu za siri ambao husaidia kupunguza msuguano wakati wa tendo hilo. Mara nyingi uteute huo hutokana na maandalizi ya kutosha ambayo huweza kufanyiwa mwanamke na mwenzi wake.

Pia kuhisi maumivu hayo huweza kuashiria uwepo wa vijiuvimbe vidogovidogo kwenye njia ya uzazi 'fibroid' hivyo ni vyema kuwaona wataalam wa afya kwa uchunguzi zaidi unapohisi hali hiyo.

Mwisho: inawezekana uume(uboo) wa mwenzi wako ni mkubwa kuliko kina chako ambapo hupitiliza na kufika  sehemu ambazo hazitakiwi kifikiwa na uume hivyo hupelekea maumivu.

No comments: