DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Monday 9 August 2021

ASKOFU GWAJIMA AZUNGUMZIA SUALA LA YEYE KULISHWA SUMU KISA SAKATA LA CHANJO YA CORONA

 


Askofu wa kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima mbaye pia ni mbunge wa jimbo la Kawe jijini Dar es salaam amekanusha madai kuwa amelishwa sumu kutokana na msimamo wake kuhusu chanjo ya UVIKO -19.

Akizungumza jana Jumapili Agosti 8, 2021 wakati wa ibada kanisani kwake kuwa hajalishwa sumu nahakuna wa kumnywesha sumu na hatotokea.

"Wanataka kusingizia watu, labda kusingizia kwamba serikali imeninywesha sumu. Niwahakikishie kwamba hakuna serikali imemnywesha sumu Gwajima kwa kuwa serikali ndiyo inasema chanjo ni hiari. Suala la afya ya mtu linapaswa kulindwa na mtu mwenyewe. Labda nitoe changamoto kwa wanaojiita watalaam waje walete andiko linaloonyesha kemikali zilizopo kwenye chanjo", amesema Gwajima

No comments: