Kupitia Mamlaka ya mapato Tanzani serikali imesema imeanza utekelezaji wa kukusanya kodi ya majengo kwa kutumia mfumo mpya wa ukusanyaji kupitia njia ya ununuzi wa umeme ,utekelezaji huo utaanza rasmi Agosti 20,2021 na unafanyika chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kushirikiana na TANESCO ukihusisha mita za aina zote za umeme.
Kwa njia hii ya ukusanyaji wa kodi kila mnunuzi wa umeme atakatwa kiasi cha Tsh. 1000 kwa mwezi kwa nyumba ya kawaida na Tsh.5000 kwa mwezi kwa kila sakafu ya ghorofa ,kwa wale wanaotumia mita za ankara watalipia kodi hii kwa pamoja katika Ankara ya mwezi.
No comments:
Post a Comment