DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Thursday 26 August 2021

MZEE ALIYEMBAKA MSICHANA WA KAZI KUFIKISHWA MAHAKAMANI

MZEE SADALLA JUMA SADALLA ALIYEMBAKA MSICHANA WA KAZI KUFIKISHWA MAHAKAMANI VUGA ,UNGUJA JUMATATU 31 AGOSTI 2021.


Juhudi za kukomesha Ubakaji na udhalalishaji visiwani Zanzibar hatimaye Mshitakiwa Sadalla Juma Sadalla mwenye umri wa miaka 74 mkazi wa  Bububu,Unguja,atafikishwa mahakamani Vuga,Unguja siku ya jumatatu 31 Augosti 2021 kwa makosa ya kumbaka msichana wake wa kazi mwenye umri wa miaka 15 (jina limeifadhiwa). Mshitakiwa Sadalla Juma Sadalla alifikishwa mahakamani mara ya mwanzo siku ya 18 Augosti 2021 na kusomewa mashataka yake.na kesi hiyo imepangiwa tena tarehe 31 Augosti 2021 katika mahakama ya Vuga mjini Unguja. Katika juhudi la kukomesha vitendo vya ubakaji na udhalalishaji viwani Zanzibar,serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na vyombo vya ulinzi vinajitahidi kuwafikisha mbele ya sheria wale wote watakaotenda makosa hayo ya ubakaji na udhalalishaji.

Mshitakiwa Sadalla Juma Sadalla alilalamikiwa na wanaharakati visisiwani Zanzibar kuwa ni mzoefu katika vitendo vya ubakaji pamoja na udhalalishaji na alipombaka msichana wake wa kazi mwenye umri wa miaka 15 ,alikuwa yupo huru  na alipanga kuondoka unguja kukimbia kesi hiyo baadhi ya majirani zake walisika lakini vyombo vya usalama viliwahi kumshika na hatimaye kumpeleka mahakamani.
Mshitakiwa Sadalla Juma Sadalla yupo mahabusu kwa kuwa shitaka la kuba,udhalalishaji halina dhamana .
Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Hussein Ally Mwinyi imepania kukomesha vitendo vyote vya Ubakaji na udhalalishaji,pamoja na madawa ya kulevya vinakoma kabisa visiwani Zanzibar.


 

No comments: