DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Friday 15 October 2021

WAJUE WACHEZAJI WATANO WA AFRIKA WALIOKARIBIA KUTWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA (Ballon d'Or)


q

Tangu kuanzishwa kwa tuzo hizo mwaka 1956, ni mwafrika mmoja tu George Weah ambaye sasa ni rais wa Liberia, aliyewahi kutwaa tuzo hiyo, mwaka 1995. Lakini wapo wachezaji kadhaa wa Afrika waliokaribia kabisa kuibeba tuzo hiyo, lakini pengine uwepo wa Lionel Messi (Argentina) anayekipigia PSG aliyetwaa mara 6 na Cristiano Ronaldo (Ureno) wa Manchester United aliyetwaa mara 5 umepunguza fursa kwa waafrika wengi.

a

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

George Weah (kulia) akikabidhi tuzo yake ya Ballon d'Or aliyoitwaa mwaka 1995 wakati huyo akiichezea AC Milan kwa Rais wa Liberia wakati huo, Ellen Johnson Sirleaf. Ilikuwa June, 2013 kwenye mchezo maalumu wa amani. Weah ni Rais wa sasa wa Liberia na muafrika pekee kutwaa Ballon d'Or.

Nyota hawa wawili katika kipindi cha muongo mmoja uliopita wamekuwa watawala wa soka, wakibadilishana hii tuzo wao wawili. Katika miaka 14 iliyopita tangu 2008 ni mwaka 2019 pekee alitwaa Luka Modric wa Croatia na klabu ya Real Madrid, huku mwaka jana haikufanyika, lakini miaka mingine yote wamekuwa wakibadilishana.

Roger Milla, Abedi Pele, Nwanko Kanu, Jay-Jay Okocha, El Hadji Diouf na Yaya Toure haya ni majina makubwa kabisa katika soka la Afrika hakuna shaka kuhusu uwezo wao, lakini katika miongo miwili iliyopita, wafuatao ni wachezaji watano kutoka Afrika ambao walikaribia kabisa kutwaa tuzo hii ya Ballon d'Or

5 Didier Drogba (Ivory Coast)

Drogba

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Didier Drogba ni mchezaji mkubwa Afrika, ana tuzo 4 za mchezaji bora wa Ivory coast na tuzo 2 za mchezaji bora wa Afrika. Mwaka 2006 ulikuwa mwaka mzuri kwa Drogba akitwaa ligi kuu mara mbili mfululizo akiwa na Chelsea akitoa mchango mkubwa kwa timu hiyo. Drogba aliingia 10 bora ya tuzo ya Ballon d'Or na mwaka uliofuata aliingia tano bora licha ya kushindwa kuitwaa tuzo hiyo.

Mwaka 2007, alimaliza nafasi ya nne kwenye Ballon d'Or nyuma ya Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na mshindi wa tuzo hiyo, Kaka. Mwaka huo alikaribia kutwaa tuzo ya dunia lakini alishindwa hata kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika, tuzo iliyokwenda kwa Frederic Kanoute, kutoka Mali.

4: Riyad Mahrez (Algeria)

Mahrez

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mahrez ni moja wa vipaji vikali kwenye historia ya soka Algeria, akiiongoza timu yake ya taifa kutwaa kombe la AFCON mwaka 2019.

Nahodha huyo wa Algeria ana kipaji kikubwa cha soka, akionekana kama dhahabu kuwahi kutokea kwenye soka la nchi hiyo. Mbali na kuwika na kutwa amataji akiwa na Manchester City, lakini soka lake la mwaka 2016 liliisaidia kuipa Leicester City taji la kihistoria la Ligi kuu England. Msimu huo alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa ligi hiyo

Kwa mafanikio hayo, Mahrez aliingia 10 bora ya tuzo ya Ballon d'Or na kumaliza nafasi ya 7 ambayo wengi walimtabiria angeingia 5 bora. Hata hivyo kwa nafasi hiyo, ni mafanikio makubwa kwake.

3: Sadio Mane (Senegal)

mane

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Sadio Mane ni miongoni mwa magwiji wa soka Afrika na Senegal. Katika tuzo za Ballon d'Or Mane alimaliza nafasi ya 23 mwaka 2017, nafasi ya 22 mwaka 2018 lakini mwaka 2019 ulikuwa mwaka mzuri aliokaribia kutwaa tuzo hiyo akishika nafasi ya 4. Kama isingekuwa kulikosa kombe la AFCON Senegal ilipofungwa na Algeria kwenye fainali huenda angekuwa mwafrika wa kwanza tangu George Weah kutwaa tuzo huyo ya Ballon d'Or.

Hata hivyo Mane ana muda wa kutwaa tuzo hiyo kama atafanya vyema akiwa na Klabu yake ya Liverpool na timu yake ya Senegal kwenye mashindano mbalimbali yajayo. Anahitaji tu kura za kutosha

2: Mohamed Salah (Egypt)

Salah

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Kwa sasa Salah anaonekana kama mchezaji bora duniani, kiwango chake katika misimu mitatu iliyopita akiwa na Liverpool, kinadhihirisha ubora wake na namna anavyoweza kuingizwa kwenye orodha ya magwiji wa soka kutoka Afrika.

Aliiongoza Misri katika kombe la dunia 2018 na amefanikiwa kumaliza kwenye sita bora ya tuzo ya Ballon d'Or mara mbili mfululizo kuanzia mwaka 2018. Mwaka 2018 alishika nafasi ya 5, na mwaka 2019 akawa wanne.

Ana nafasi nyingine msimu mwaka 2022 kutwaa tuzo hiyo ya Ballon d'Or kama ataendelea na kiwango chake cha sasa akiwa na Liverpool pamoja na Misri, ambayo inatarajiwa kuwemo kwneye mataifa matano yatakayofuzu kombe la dunia mwakani.

1: Samuel Eto'o (Cameroon)

etoo

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Inawezekana huyu ndiye mchezaji bora wa Afrika kuwahi kutokea, licha ya majina mengine mengi kuwepo kama Roger Milla, Abedi Pele, Nwanko Kanu, Jay-Jay Okocha, El Hadji Diouf na Yaya Toure. Eto'o ameshinda makombe mawili ya AFCON akiwa na Cameroon. Ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara nne, na anatajwa ndiye muafrika aliyekaribia zaidi kutwaa Ballon d'Or.

Katika maisha yake ya soka, ameorodheshwa kwenye tuzo ya Ballon d'Or mara 10, ikiwa ni mara nyingi zaidi kuliko muafrika mwingine yoyote. Kwa mara ya kwanza Eto'o kuingia kwenye orodha hiyo ilikuwa mwaka 2004 alipomaliza wa 15, na katika miaka 8 iliyofuata hakuwa anakosa kwenye orodha ya juu ya wanaowania tuzo hio.

Alimaliza nafasi ya 10 kwenye Ballon d'Or ya mwaka 2005, mwaka 2006 alimaliza wa 7, 2007 akawa wa 30, 2008 wa 17, kabla ya mwaka 2009 akiwa na kiwango kikubwa kabisa kuingia 5 bora. Kufunga na kiwango bora kila mwaka akiwa na nyota kama Ronaldinho, Deco na Messi aliyekuwa anachipukia, E'too wa Barcelona na baadae Inter Milan iliyotwaa ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2010 alikuwa moto wa kuotea mbali. Wengi walimuona kama alistahili kutwaa tuzo hiyo katika wakati wake.

                                                                chanzo. BBC

Gusa link hiyo kwa ajili ya kupata burudani ya Muziki muda wote wote na Dealplus online radio
                                      https://onlineradiobox.com/tz/dealplus/?cs=tz.dealplus&p=1

No comments: