DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Thursday 14 October 2021

TBS YAIFUNGIA JUISI YA CERES NA KUIONDOA SOKONI KWA MADAI YA KUWA NA SUMU NDANI YAKE

 

Kutokana na juisi ya tufaa ‘Apple’ iliyotengenezwa na kampuni ya Afrika Kusini ya Ceres kudaiwa kuwa na kiwango cha juu cha sumu, Tanzania inaungana na mataifa mengine saba kuiondoa sokoni.

Akizungumza leo Oktoba 14, 2021 Mkurugenzi wa udhibiti ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Lazaro Msasalaga amesema suala hilo linafanyiwa kazi.

Amesema kila bidhaa inayoingia nchini hupimwa na hivyo ikiwa itabainika toleo hilo lipo ndani ya nchi itaondolewa haraka na utaratibu mwingine wa kuichunguza utafanyika.

“Tunalifanyia kazi, toka jana tunakusanya taarifa tuone kwamba ziliingizwa na nani kama zipo na iwapo tutazibaini utaratibu utafanyika kubaini ziliingizwa lini na nani anahusika,” amesema Msasalaga.

Amesema juisi za Ceres ni salama na hazina shida isipokuwa mtu hatakiwi kununua toleo tajwa ambapo wao ‘TBS’ wanalifuatilia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Oktoba 11 na Jumuiya ya soko la pamoja la nchi za mashariki na kusini mwa Afrika (COMESA) imetaja matoleo sita yaliyotolewa kati ya Juni 14 na 30 kwa Barcode 6001240200018 (Ceres Apple 4x6x200ml).

Comesa imesema miongoni mwa maeneo ambayo yameathirika zaidi na toleo hilo ni DRC Congo, Seychellies, Zambia na Zimbabwe :Chanzo Mwananchi 

gusa link hiyo hapo chini kupata radha na burudani ya mziki wa kila aina kwa muda wote

                                           http://stream.zeno.fm/0vpamwqrg98uv


No comments: