DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Saturday, 23 September 2023

AJALI YA ROLI YAUA WATU 9

 


 

WATU tisa wamefariki dunia mkoani Mbeya baada ya  dereva wa lori lenye namba za usajili BCE 9384/ABX8675 kushindwa kulimudu gari lake kwenye mtelemko mkali  wa Mbalizi na kwenda kuigonga gari ya abiria na yenye namba za usajili T.636 DQY aina ya Mitsubishi Rosa .

 Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoani Mbeya,Benjamin Kuzaga amesema kuwa tukio hilo limetokea Septemba 22 mwaka huu majira ya saa 11.40 jioni  katika eneo la mteremko wa Iwambi wilaya ya Mbeya Vijijini  mkoa wa Mbeya .

Kamanda Kuzaga amesema kuwa gari  yenye namba za usajili BCE 9384/ABX 8675 aina ya Howo mali ya kampuni ya Horn Afric Motors ltd ya nchini Zambia ikitokea Mbeya kuelekea Tunduma likiendeshwa na dereva Mohamed Abilah (47) Mkazi wa Zambia .

Aidha Kuzaga ameeleza kuwa gari hilo iliigonga kwa nyuma Gari yenye namba za usajili T.636 DQY aina ya Mitsubishi Rosa ikitokea Mbeya mjini kuelekea mbalizi ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva ,Elly Mwakalindile (41)mkazi wa Iyunga na kusababisha vifo vya watu Tisa ambapo kati yao wanaume watano na wanawake wanne.

Aidha  kamanda Kuzaga amesema kuwa katika ajali hiyo watu 23 walijeruhiwa kati  ambapo kati yao wanaume 13 na wanawake 10 ni majeruhi  na wanaendelea kutibiwa katika  Hospitali Teule ya Ifisi iliyopo Mji Mdogo wa Mbalizi na wengine wamehamishiwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

 Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali Teule ya Ifisi Mbalizi ambapo miili ya marehemu 07 imetambuliwa huku miili ya watu 02 ikiwa bado  haijatambuliwa.

Chanzo cha ajali hii ni Dereva wa lori kushindwa kulimudu gari lake kwenye mteremko mkali na kwenda kuigonga kwa nyuma Gari ya abiria na kuwa Dereva wa lori amekamatwa na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa madereva ambao wanapita katika Mkoa wa Mbeya kwenye milima na miteremko mikali kuhakikisha wanakagua magari yao kabla ya kuanza safari na wamiliki wa magari wasiruhusu magari yao kuendeshwa na madereva hao ili kuepusha ajali.

No comments: