KONDOMU ni kifaa/ zana iliyotengenezwa mahususi kuvalisha uume au kuwekwa ukeni wakati wa kujamiiana.Nazo hubana kutokana na umbile la uume au uke.
Kondomu hizi zipo za aina tofauti kutokana na muda na vipindi zilipotengenezwa, nazo ni kama ifuatavyo:-
Awamu ya I – zilizotengenezwa kwa mimea.
Hizi zilitengenezwa mahususi kama kinga dhidi ya maambukizo ya vimelea vya ugonjwa wa kaswende [ugonjwa wa kifaransa]
Awamu ya II – kutokana na utumbo wa kondoo.
Dr. Condom alifahamika kama mgunduzi wa kondomu hizi, naye alikuwa ni dakatari wa Mfalme Charles II.
Alimshauri Mfalme kutumia kama kinga kutokana na magonjwa ya zinaa kutokana na tabia yake ya kuwa na wanawake wengi nje ya ndoa yake.
Awamu ya III – kutokana na mpira
Hizi zilitengenezwa kwa urahisi na kwa wingi na zikawa ndizo pekee zenye uwezo wa kudhibiti mimba hadi miaka ya 1960 vilipogunduliwa na vidonge vya majira.
JE KONDOMU NI SALAMA?
Tunaelezwa kuwa kondomu hutengenezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba haziwezi kuruhusu kitu chochote kupita.
Lakini tafiti mbalimbali zilizofanyika zinaonyesha kuwa kondomu zaweza kuvuja kutokana na mazingira halisi ya utengenezaji wa latex.
Wengine wanadai kuwa ili kuzifanya imara, kondomu zimetengenezwa kwa kupishanisha pande mbili ili kuziba udhaifu wa kila upande.
Hata hivyo watengenezaji wanasahau kuwa mazingira ya matumizi ya kondomu katika ngono hayalingani na majaribio waliyofanya ya kujaza maji au hewa ili kupima kama maji na hewa vinapita.
Katika tendo la ngono ipo misuguano ya namna mbalimbali inayosababisha kubadilisha mazingira ya kondomu na kuidhoofisha.
Kutokana na tafiti hizo imefahamika kuwa kondomu hazina uwezo wa kuzuia mbegu za kiume kupenya wakati wote.
Upana wa kipenyo cha mbegu ni makroni 5 wakati upana wa kipenyo cha kirusi cha ukimwi ni makroni 0.1
Kwa maneno mengine mbegu ya kiume ni kubwa mara 50 ya kirusi cha ukimwi.
Vile vile tafiti zimeonyesha kuwa kondomu haina uwezo wa kuzuia maambukizo ya magonjwa ya zinaa vikiwemo virusi vya ukimwi kwa kiwango cha asilimia mia moja.
Hivyo tunaweza kusema kuwa, kondomu si salama kwa asilimia mia moja.
Kondomu zina kiwango cha kushindwa cha kati ya asilimia 10 na 15 na wengine wanasema hata asilimia 20.
Wasambazaji na wahamasishaji wa matumizi ya kondomu hawapendi kusikia ukweli huo na wanafanya jitihada kubwa ya kuficha ukweli huo.
Matangazo yatolewayo kupitia mabango ya barabarani, katika televisheni, radio na hata magazeti yanawarubuni watu yakiwaaminisha kuwa kondomu humkinga mtumiaji kwa kiwango cha asilimia 100%
Huko ni kukengeusha ukweli na kukiuka maadili ya kitaaluma.
Wengi kama sio wote wateteao matumizi ya kondomu hufanya hivyo kwa sababu ya maslahi ya kifedha na kibiashara.
Tukiongozwa na dhamiri safi, lazima tukiri ukweli uliopo na tuwaeleze watumiaji, ili tusijekuwa sababu ya kifo chao.
Kila kondomu inaposhindwa [itumikapo] kama kinga dhidi ya maambukizo ya virusi vya ukimwi ] humaanisha kifo.
Udhaifu wa kondomu Kiufundi,Matumizi, Kimazingira
Udhaifu wa kiufundi
Wasambazaji wanatueleza kuwa kondomu zilizotoka kiwandani zikiwa na ubora unaotakiwa zikitumika wakati wote na kwa usahihi zina uwezo wa kukinga kwa kiwango hadi cha asilimia 97.
Zisipotumika vizuri zina kiwango cha kushindwa cha asilimia 14.
Kiwango cha kushindwa kwa kondomu kuzuia maambukizo ya magonjwa ya zinaa hutofautiana kutokana na aina ya magonjwa ya zinaa.
Kondomu zaweza kuzuia kwa kiwango fulani maambukizo ya magonjwa ya zinaa yanayosafiri kwa njia ya ute, lakini haziwezi kuzuia magonjwa ya zinaa yanayoambukizwa kwa mgusano wa mwili kama vile "herpes" na "human papillomavirus"; au magonjwa yanayoambukizwa kutokana na vidonda au malengelenge yaliyoko kwenye via vya uzazi kama vile kaswende.
Hali hiyo inatokana na:
Watengenezaji wameruhusu udhaifu wa kiufundi kama zao la kiwandani lililotengenezwa na kazi ya mikono ya binadamu [acceptable quality limit] kwa kiwango Fulani kwa nchi mbalimbali.
Mfano, Marekani kiwango kilichokubaliwa ni asilimia 99.6 kwa kutoruhusu kondomu kuvuja.
Uingereza asilimia 97, Uholanzi asilimia 96. 5. Hivyo katika kila idadi ya kondomu itumikayo kwa wakati mmoja kuna kiwango cha kuvuja kati ya asilimia 0.4 (USA); 3% (Britania); 3.5% (Holland).
Kondomu huzeeka
Kwa kadiri zisivyotumika kwa muda mrefu ndivyo hivyo zinaaendelea kuzeeka.
Kwa hiyo mtumiaji kondomu wa miaka 3 au 4 baada ya kondomu hiyo kutengenezwa yumo katika hatari zaidi kuliko anayetumia kondomu mara tu baada ya kutoka kiwandani.
Utafiti mmoja umeonyesha kuwa kiwango cha kupasuka kwa kondomu kiliongezeka kutoka 3.6% kwa kondomu mpya hadi 18.6% kwa kondomu zilizotumika miaka kadhaa baadaye.
Kondomu hupasuka.
Kiwango cha kupasuka hutegemea aina ya kilainisho kilichotumika na aina ya kondomu. Kwa mujibu wa tafiti 15 zilizofanywa na "Contraceptive Technology" yalionyesha kuwa katika kondomu 25,184 zilizotumika 4.64% zilipasuka.
Ingawaje kondomu za latex zinaonekana kuwa na kiwango kidogo sana cha kupitisha virusi vya ukimwi, hatari kubwa ya matumizi yake imo katika uwezekano wa kondomu kupasuka, kuteleza na kuteleza.
Kwa hiyo hata kama ni virusi vichache tu vinaweza kupenya, kiwango cha maambukizo kitakuwa kikubwa kadiri kondomu zinavyosambazwa kwa wingi na kadiri watu wanavyojihusisha na vitendo vya ngono wakiamini katika matumizi ya kondomu.
Udhaifu katika matumizi
Matumizi mabaya: yaani kutovaa vizuri, kuvaa nje ndani, aina ya ngono, urefu wa muda wa ngono, pia kutokana na uelewa mdogo hasa kwa wasojua kusoma na kuandika na wale wakaao mbali na mijini.
Kuteleza na kuvulika kutokana na hali ya uume kuwa mdindifu au la; upana au wembamba; mrefu au mfupi.
Pia kutokana na tendo la ngono na hali ya mtumiaji na mazingira ya matumizi.
Kutokana na umri wa mtumiaji, kama ni mtoto, kijana, mtu mzima au mzee.
Kutumia kondomu ambazo muda wake umepita. Mfano wanaotumia gizani , katika hali ya ulevi, kutokujua kusoma, kuchunguza na kugundua kama muda wake umepita.
Mazingira ya kingono yakishawekwa, watu wanatawaliwa na mihemuko ya juu ya ngono kiasi kwamba hawawezi kuchunguza tarehe ya ukomo wa matumizi ya kondomu.
Ingawa watengenezaji wanashauri kutotumia kondomu iliyobadilika rangi au iliyokauka, tabia za watumiaji hazina nafasi ya kuzingatia ushauri huo.
Lengo la mtumiaji laweza kusababisha matumizi kuwa mabaya. Mtu mwenye virusi vya ukimwi, anajiwekea lengo kwamba hataki kufa peke yake, atafanya jitihada za kutokutumia vizuri ili mwenzake [ambaye anaamini hajaambukizwa] aweze kuambukizwa ili, "nisife peke yangu".
Vilevile katika siku hizi za dawa za kupunguza makali ya kuzaliana virusi vya ukimwi, mtu anaweza kuonekana mwenye afya nzuri kabisa, na anaweza kumshawishi mwenzake kuachana na kondomu kwa vile "wanaaminiana".
Kwa hiyo mambukizi yanaweza kuwa makubwa kutokana na kutowadhibiti wale waliokwisha ambukizwa.
i.udhaifu wa kimazingira
Huu unatokana na hali zifuatazo:- kibinadamu, kimaumbile na Kibinadamu.
Udhaifu wa kondomu waweza kusababishwa na usafirishwaji, yaani muda unaotumika kusafiri kutoka sehemu zinapotengenezwa hadi mahali zinapotumika;
ii. Kimaumbile
Vyombo vya usafirishaji na usalama wa vyombo hivyo;
Kondomu zinazosafirishwa katika meli, zikiwa baharini kwa miezi kadhaa kabla hazijafika katika nchi lengwa na katika hali ya joto ndani ya makontena zinakuwa na kiwango hafifu katika ubora wake
No comments:
Post a Comment