DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Thursday, 4 May 2017

YUSUPH MLELA AWAGEUKIA WATAFSIRI FILAMU

Yusuph Mlela awaonya Wanaotafsiri filamu za nje

Muigizaji wa filamu za Bongo Yusuph Mlela amefunguka na kudai kwamba wapo tayari kupambana na mtu anayetafsiri filamu za nje kwa lugha ya Kiswahili na kuziuza kwa bei rahisi, ili kunusuru soko la filamu  la ndani lizisije kufa.

Mlela ameongeza kuwa wao kama wasanii wasipoonyesha juhudi za kupigania soko la filamu basi kizazi chao kitakuwa hakijaonyesha juhudi zozote za kupambana na maharamia hao ambao ndio chanzo cha kazi za sanaa za bongo kushuka na kwamba watu hao wanafanya kazi bila kufuata utaratibu.

Mlela ameendelea kufunguka mbele ya kamera za eNewz kuwa zoezi la kumdhibiti mtu anayedurufu kazi za wasanii halijaanza sasa na kwamba muda mrefu  harakati za kumdhibiti mtu huyo zilikuwa zikifanyika ila kwa kuwa zoezi limepatiwa nguvu zaidi litafanikiwa.

No comments: