DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Monday 19 June 2017

VYAKULA TULAVYO VINATUMALIZA

Leo napenda kuchukua fursa hii kueleza kwa mapana na marefu suala la vyakula na namna ambavyo vimekuwa chanzo kikuu cha maradhi sugu yanayotukabili leo, ambayo mengi mwisho husababisha vifo.

Tukumbuke kwamba uzima wa mtu unategemea sana kinga aliyonayo mwilini, kinga ambayo hujengwa na ulaji wa vyakula vyenye virutubisho vya aina mbalimbali. Kwa namna ambavyo Mungu ametuumba, mwili unapaswa kujilindi wenyewe dhidi ya maradhi ya kila aina. Ukiwa na kinga imara ya mwili siyo rahisi kuugua mara kwa mara

Magonjwa yanayojitokeza haraka pale kinga ya mwili inapokuwa chini, ni pamoja na kuugua malaria mara kwa mara, kifua kikuu, kutokwa na majipu, kutokwa uvimbe wa ajabuajabu katika mwili, kupatwa na mkanda wa jeshi, kupatwa na saratani na magonjwa mengine ya maambukizi.
Huo ni mfano wa kundi moja la magonjwa ya maambukizi, lakini hata magonjwa mengine hatari kama shinikizo la damu, magonjwa ya moyo, magonjwa ya viungo, kisukari, macho, na mengine mengi, huwa ni matokeao ya ulaji wa vyakula visivyo sahihi au uachaji wa ulaji vyakula muhimu

CHANZO CHA KUSHUKA KWA KINGA YA MWILI.
Ili uwe na kinga imara ya mwili, ni lazima uwe unakula mlo kamili unaojumuisha matunda, mboga za majani, nafaka na vyakula vingine vya asili, kwa sababu kila unachokula kina faida yake mwilini. Lakini siyo tu kula chochote kinachoitwa ‘chakula’, bali ule kilichosahihi na kilichosahihi.
Katika maisha tunayoishi sasa, hasa mijini, idadi Kubwa ya watu hawali kabisa vyakula sahihi, badala yake wanakula vyakula ambavyo si tu ni hatari kwa afya zao, bali pia hudhoofisha kinga ya asili ya mwili na hivyo kuufanya mwili kubaki dhaifu na unaoweza kupatwa na ugonjwa wowote.

Chanzo kikuu cha kushuka kwa kinga ya mwili kunasababishwa na ulaji wa vyakula visivyo sahihi ambavyo ndivyo vinavyopatikana kwa wingi kila mahali, hasa sehemu za mijini. Vyakula visivyofaa ndivyo vinavyotangazwa na kunadiwa kwenye vyombo vya habari kuwa bora.

VYAKULA HATARI VINAVYOLIWA KILA SIKU
Kuna orodha ndefu sana ya vyakula hatari ambayo huliwa kila siku, kuanzia asubuhi hadi jioni. Vyakula hivi yumkini huliwa kwa takriban maisha yote ya mtu na huonekana ni vya kawaida. Baadhi ya vyakula hivyo ni kama vile unga wa ugali, mkate, chips na juisi.

UNGA WA UGALI
Unga wa ugali unaotumiwa na watu wengi nchini ni sembe nyeupe. Chakula kikuu katika kaya nyingi zinazotumia ugali kama mlo wa kila siku huwa ugali mweupe uliotokana na mahindi yaliyokobolewa na kusafishwa, kisha kusagwa na kutoa unga safi mweupe. Kwa mtizamo wa macho na ladha ya mdomoni, wengi wanaamini kuwa ugali wa aina hii ndiyo mzuri na unaotakiwa kuliwa.
Ulaji wa ugali wa aina hii hauna faida yoyote mwilini, kwani hauna virutubisho, kwa sababu vilishaondolewa vyote wakati wa kukoboa. Virutubisho muhimu vya muhindi viko kwenye kiini chake, hivyo unapokiondoa unakuwa umeondoa lishe muhimu. Ndiyo maana hata panya hawali mahindi yaliyokobolewa.

No comments: