DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Thursday 1 March 2018

NYIMBO 15 ZA BONGO ZAFUNGIWA KWA KUKIUKA MAADILI

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imepokea orodha ya nyimbo zisizokuwa na maadili kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).
Nyimbo hizo zilitolewa na wasanii na kusambazwa katika vyombo mbalimbali vya utangazaji na mitandao ya kijamii.
Kutokana na nyimbo hizo kuwa na maudhui ambayo ni kinyume na kanuni za Huduma za Utangazaji (Maudhui) 2005, mamlaka hiyo imeviagiza vyombo vya habari kusitisha nyimbo hizo.
Orodha ya nyimbo hizo ni kama ifuatavyo:-
1. Hallelujah – Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz
2. Waka waka – Nasib Abdul a.k.a Diamond Platinumz
3. Kibamia – Aberdnego Damian a.k.a Roma Mkatoliki
4. Pale Kati Patamu – Emanuel Elibariki a.k.a Ney wa Mitego
5. Hainaga Ushemeji – Amani Hamisi a.k.a Manifongo
6. 6I am Sorry JK – Nicas John Mchuche a.k.a Nikki Mbishi
7. Chura – Snura Mushi a.k.a Snura
8. Tema mate tumchape – Hamad Ali a.k.a Madee
9. Uzuri Wako – Juma Musa Mpolopoto a.k.a Jux
10. Nampa Papa – Gift Stanford a.k.a Gigi Money
11. Nampaga – Barnaba Elias a.k.a Barnaba
12. Maku Makuz – Emanuel Elibariki a.k.a Ney wa Mitego
13. Nimevurugwa – Snura Mushi a.k.a Snura
14. Bongo Bahati Mbaya – David Genzi a.k.a Young Dee
15. mikono Juu – Emanuel Elibariki a.k.a Ney wa Mitego
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania imevitaka vituo vyote vya utangazaji kuacha mara moja kurusha nyimbo hizo, na kueleza kuwa kituo kitakachobainika kukiuka katazo hilo, kitachukuliwa hatua kali za kisheria.