DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Sunday, 22 August 2021

GWAJIMA NA JERRY SILAA KUWEKWA KIKAANGONI


SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai ameagiza wabunge Askofu Josephat Gwajima na Jerry Silaa kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi na heshima ya muhimili huo

Wabunge hao wote wa chama tawala- Chama Cha Mapinduzi (CCM), endapo watakaidi kufika mbele ya kamati hiyo ambayo inaongozwa na mwenyekiti wake, Emmanuel Mwakasaka, watachukuliwa hatua za kisheria.

Taarifa ya kitengo cha mawasiliano na uhusiano wa kimataifa wa Bunge iliyotolewa leo Jumamosi, tarehe 21 Agosti 2021, imeeleza Gwajima ambaye ni mbunge wa Kawe atatakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Jumatatu ya tarehe 23 Agosti 2021, saa 7:00 mchana katika ubunge 229 wa Bunge, Dodoma.

Silaa yeye atafika mbele ya kamati hiyo kesho yake yaani Jumanne ya tarehe 24 Agosti 2021 saa 7:00 mchana katika ukumbi 229 wa Bunge.

taarifa hiyo haikueleza tuhuma za wabunge hao, lakini katika siku za hivi karibuni, Gwajima ambaye ni Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, ameonyesha msimamo wake hadharani wa kupinga chanjo ya corona.

Askofu Gwajima amekuwa akitumia siku za Jumapili kuzungumza na waumini wa kanisa lake, lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam kuwashauri wasichanje chanjo hiyo kwani ina madhara huku akisema yupo tayari kupoteza ubunge kama atalazimishwa kuchanjwa chanjo hiyo ili kuruhusiwa kuingia bungeni.

No comments: