DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Wednesday, 25 August 2021

MRITHI WA BABU WA LOLIONDO AZIDI KUFANYA MAKUBWA NA KUPONYA WATU


Siku moja baada ya gazeti hili kuandika kuhusu kuwapo kwa mtoto Yunis Ogot (2) anayetibu kwa sala na maombi katika Kijiji cha Bukama wilayani hapa, uongozi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bukama umezungumzia huduma hiyo ukiahidi kuichunguza.
Paroko wa Parokia ya Bukama, Padri Cleophace Adek alisema wameanza uchunguzi wa kiimani kujiridhisha na huduma zinazotolewa na mtoto hiyo.

“Hadi sasa mambo na maelezo mengi yanayotolewa na mtoto huyo yanaonyesha kuna uwezekano mkubwa ni kweli ametokewa na Bikra Maria,” alisema Padri Adek.
Kuhusu alivyopata taarifa, Padri hiyo alisema wazazi wa mtoto huyo walienda ofisini kwake kumueleza kuwa amekuwa akitokewa na Bikira Maria, hivyo kuhitaji mwongozo wa kitu gani kifanyike.

“Uongozi wa jimbo uliruhusu kuanza kwa uchunguzi na mchakato wa ujenzi wa goroto unaendelea hadi sasa,” alisema Padri Adek.
Kuhusu tiba na maombi yanayotolewa na mtoto huyo, Padri Adek alisema kanisa limeagiza izingatie taratibu na kanuni za kiimani.
“Maji yanayoombewa na mtoto huyo lazima yaletwe kanisani kupata baraka za paroko,” alisema Padri Adek.
Kijana mmoja ambaye padri huyo alimtaja kwa jina la Yohana Garigo, mkazi wa kijijini hapo aliyepooza kwa muda mrefu alisema amepona baada ya maombi ya mtoto huyo.Hata hivyo Padri Adek alisema suala la kupona linahusiana na imani ya anayeombewa.

Watu wajue kuwa anayetibu na kuponyesha ni Yesu pekee na huyu mtoto ni mjumbe tu aliyetumwa. Ili mtu apone ni lazima atubu ili malengo yatimie,” alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Juma Chikoka ametembelea eneo anakotoa huduma mtoto Yunis na kuagiza wahusika kuzingatia tahadhari za kujikinga na Uviko - 19.
Pamoja na tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya korona, Chikoka pia aliagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua tajadhari za kiusalama kutokana na eneo hilo kutembelewa na watu wengi wakiwemo wanaotoka nje ya nchi.

“Serikali haiwezi kuingilia zaidi ya kuhakikisha ulinzi na usalama wa wote wanaofika kwa ajili ya sala na uponyaji,” alisema mkuu huyo wa Wilaya ya Rorya

No comments: