Professor Jay ataja sabubu za wanasanii 'Kufulia
Mbunge wa Jimbo la Mikumi, Joseph Haule ‘Professor Jay’ amefunguka na kusema kuwa wasanii wengi wa Tanzania wamekatishwa tamaa ya kuendelea kufanya kazi za sanaa kwa kukosekana Sheria ya hati miliki.
Rapa huyo amebainisha hayo muda mchache alipotoka katika kikao cha Bunge na kusema serikali inapaswa kuzingatia kilio hicho cha wasanii kwa kusimamia kuwepo kwa hati miliki ili kuweza kuongeza pato la taifa kupitia kazi za wasanii.
“Kilio kikubwa cha wasanii wa Tanzania sasa hivi ni kuhusu masuala yao ya hati miliki na ukiangalia Sheria ya hati miliki namba 7 ya mwaka 1999 imeonekana kuwa na mapungufu makubwa sana, kiasi kwamba wasanii watanzania hawapati kile kinachostahili, hawapati jasho lao linavyotakiwa na wasanii wa Tanzania wamekata tamaa lakini kiukweli kabisa takwimu na tafiti zilizofanywa na ‘Lulu Art Promoters’ inaonyesha kwamba wasanii wa Tanzania na sanaa ya muziki pekee yake inachangia zaidi ya asilimia 1 ya pato la taifa”. Alisema Mbunge huyo
Aidha, Prof. Jay aliendelea kwa kusisitiza kwamba “Muziki ni nyanja muhimu sana, kiukweli ikitupiwa jicho na kuweza kupewa kipaumbele wasanii wanaweza wakupata kile kinachostahili ili kuongeza pato kubwa katika taifa letu.” Alisisitiza Prof. Jay
No comments:
Post a Comment