DEAL PLUS

Karibu DEALPLUS BLOG uweze kupata habari za Michezo, Siasa, Afya na Burudani kutoka ndani na nje ya nchi.

Breaking


Monday, 23 August 2021

WAFANYAKAZI WA RADIO5 ARUSHA WAGOMA (HAWAJALIPWA MSHAHARA MIEZI 6)

UKIISIKILIZA RADIO5 ARUSHA KWA SASA KUPITIA MASAFA YA 91.3 DAR NA PWANI AU 105.7 ARUSHA AU UKIISIKILIZA ONLINE UTAKUBALIANA NA UKWELI KWAMBA WAFANYAKAZI WAMEGOMA NA VIPINDI VINAPIGWA MUZIKI TU KWA MUDA SASA...

Habari za wakati huu

Sisi ni Wafanyakazi wa Radio5 Arusha iliyo chini ya TAN COMMUNICATION MEDIA ambayo inamilikiwa na Familia ya Mzee LOWASSA.
Tumeamua kuandika ujumbe huu kwakuwa Tumechoka sasa.

Kampuni hii imekuwa Ikiwanyanyasa Wafanyakazi kwa miaka mingi mpaka sasa imekuwa mbaya zaidi:-

1. Kampuni Hailipi Wafanyakazi kwa Wakati na Mpaka sasa Huu ni miezi 6 Hawajalipa Wafanyakazi na Wanatulazimisha kuingia Kazini bila kujua Tunakula Nini, Tunaishi Wapi, Tukiumwa Tunajitibu Vipi, Tunasafirije kuja Kazini, Watoto wetu Wanasomaje, Familia zetu zinazotutegemea Tunazimudu Vipi, NK.

2. Hatuna Bima ya Afya, Tangu Radio hii iwe chini ya Lowassa 2007 Hakuna Mfanyakazi amewahi kukatiwa Bima ya Afya na Mikataba inasema tutapewa Bima ya Afya ila Haijawahi kutokea

3. Makato ya HIFADHI ZA JAMII HAYAFIKI KWENYE MIFUKO HUSIKA NA TUNAKATWA. Kampuni hii Haijawahi kupeleka hata Sh. 10 ya Makato wanayokata wafanyakazi na Tumekuwa Tukilalamika Miaka yote, Tushaenda Idara ya Kazi na NSSF Kulalamika Kwenye Ofisi zao za Arusha ila Wanakuja Ofisini wanaonana na Uongozi WANAHONGWA Wananyamaza (Kwenye Hili Viongozi wa IDARA YA KAZI na MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII Tunaomba Rais SAMIA SULUHU HASSAN Awawajibishe maana Wana Michezo Hatari sana na ni WALA RUSHWA

4. Kampuni inaingiza Fedha Nyingi sana kwa mwezi sababu tuna Matangazo Makubwa lakinj Haitujali, Radio hii Haitoi Fursa kwa Wafanyakazi hata Mikopo midogo midogo Hakuna

5. Uongozi wa Radio5 ni Mbovu kiasi kwamba Kila siku Radio inaelekea Kufa (Tulikuwa Tunasikika Mikoa 22 sasa Tumebaki Arusha na Dar tu na Usikivu ni Mbovu kiasi kwamba Hata Wasikilizaji Hatuna, Radio mara leo ipo hewani kesho Haipo, Vipindi Havina Ubora sababu Wafanyakazi wengine wanashindwa kufika kazini HAWANA NAULI) Cha Kushangaza Tunapiga Kelele kila siku Hawasikii 
MF. Bobb Lowassa ambaye ndiye anasimamia Radio ANA MIAKA MITATU (3) Hajakanyaga Radio5!!!!

6. Kampuni Haina Usafiri (Radio 5 Haina hata GARI MKWECHE Kwa ajili ya Wafanyakazi na Hawatoi Nauli japo Mkataba unasema Kampuni ina Gari za Usafiri na pia Wafanyakazi watakuwa wanapewa NAULI)

7. Uongozi hautaki VIKAO NA WAFANYAKAZI, Ni zaidi ya Miaka Mi-4 sasa Wafanyakazi tumekuwa tunaomba Kukutana na Viongozi wetu haswa MD Lakini Hawataki

MAOMBI YETU:-
1. TUNAOMBA MZEE LOWASSA Aingilie Kati Hii Kampuni Inakufa na Wafanyakazi wanadai Stahiki zao Muhimu Hakuna wa Kuwasikiliza

2. Tunaiomba Serikali Kuingilia Kati Idara zake Muhimu ambazo zinakuwa Hazitimizi wajibu wao Kama IDARA YA KAZI na MIFUKO YA HIFADHI ZA JAMII 

UJUMBE HUU TUMEANDIKA WAFANYAKAZI WA RADIO5 (Wafanyakazi 11 Kwa Niaba ya Wenzetu na Hatuwezi Kutaja Majina yetu ila ni Uhalisia kwamba Tunateseka)


No comments: